Sehemu ambazo kamwe huruhusiwi kuzitembelea duniani

Uswiss

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2016
Posts
840
Reaction score
2,169
Najua kwamba ungefurahi sana kuona ukiizunguka dunia unavyotaka, utembelee fukwe zote duniani, hoteli na sehemu nyingine nyingi. Labda unasema kwamba kuna siku ukipata pesa utafanya starehe kwa kutembelea sehemu mbalimbali ili kuendelea kuona uumbaji wa Mungu.

Ndugu yangu, nakutakia mafanikio mema lakini kumbuka kwamba hata uwe na pesa kiasi gani, kuna sehemu ambazo hutotakiwa kutembea, ni hatari na sehemu nyingine ni kwa sababu serikali haitaki wewe kutembea huko.

Hizi ni sehemu ambazo KAMWE HURUHUSIWI kutembelea hata kama utakuwa na kiasi kikubwa cha fedha.

KISIWA CHA NYOKA

Hiki ni kisiwa kilichokuwa nchini Brazil, kina msitu mkubwa na kina nyoka wengi kuliko sehemu yoyote duniani. Watu wengi wamekuwa wakikatazwa kutembelea kisiwa hicho kutokana na hatari kubwa iliyokuwepo huko na hata wale watu ambao wamekuwa wakienda huko kisiri wamekuwa wakifa kwa kuumwa na nyoka hao hatari.

SEHEMU YA KUPANGILIA NA KULIPUA MABOMU

Hii ni sehemu iliyopo nchini Marekani ambayo hutumika kutengenezea mabomu ya nyuklia zaidi ya elfu moja na kuyajaribia huko. Hata ukiangalia ardhi yake haipo na muonekano mzuri kutokana na mabomu hayo ya nyuklia ambayo yamekuwa yakijaribiwa kila siku.
Serikali ya Marekani imewakataza watu kwenda huko kutokana na hatari iliyokuwepo na hata wale wanaoishi huko ambao ndiyo watengenezaji wakubwa wa mabomu hayo wamekuwa wakiishi kwa tahadhari kubwa.

MAKUMBUSHO YA VATICAN

Ukienda nchini Vatican ambapo ndipo makao makuu ya Kanisa la Roma, kuna sehemu ambayo ndiyo uhifadhi nyaraka mbalimbali za siri, za miaka mingi nyuma na hata zile za kipindi hiki.

Hakuna mtu anayeruhusiwa kutembelea huko, kuna ulinzi mkali ambao umekuwa kwa saa ishirini na nne. Kinachowafanya watu kutoruhusiwa kuingia huko ni wizi, wanahofia watu wanaweza kuingia na kuiba au kuchoma moto nyaraka hizo ambazo zimekuwa muhimu sana.

CHUMBA CHA MALKIA

Unaweza ukashangaa lakini ndiyo ukweli. Hakuna mtu anayeruhusiwa kuingia katika chumba cha Malkia wa Uingereza, Elizabeth II zaidi ya baadhi ya wanafamilia na yeye mwenyewe.

Kwa nje, chumba hicho kina ulinzi mkubwa, askari wamekuwa wakitembea kuhakikisha hakuna mtu anayeingia japokuwa mwaka 1982, mtu aitwaye Michael Fagn alifanikiwa kuingia na ilipogundulika, haraka akatolewa na kupelekwa polisi.

CHUMBA NAMBA 39

Hiki ni chumba cha siri nchini Korea Kaskazini. Chumba hicho ndicho chenye siri kubwa juu ya mabomu ya nyuklia yanayotengenezwa huko. Hakuna mtu ambaye anaruhisiwa kutembelea huko zaidi ya rais mwenyewe, Kim Jong-un na baadhi ya wakuu wa jeshi kwani kumejaza siri kubwa ambazo kama zitagundulika basi wanaweza kupigwa muda wowote ule.

CHERNOBYL

Hii ni sehemu ndogo nchini Ukraine. Tarehe 26/4/ 1986 kulikuwa na ajali mbaya ya bomu la nyuklia ambalo lilijilipua huko. Maji yakaathirika, ardhi na vitu vingine.

Hakuna mtu anayeishi huko kwa sasa na yeyote anayetaka kutembelea ni lazima aombe ruhusa kutoka katika serikalini na hata kwenda huko, hupewa mavazi maalumu kwani mpaka leo hii ile sumu ya nyuklia bado ipo.
 
[emoji116]
CHERNOBYL-1.jpg
Vatican.jpg
Room-39.jpg
Nyoka-1.jpg
Nyoka-2.jpg
CHERNOBYL-4.jpg
 
Ongezea na closed cities. miji ambayo huruhusiwi mgeni kwenda mpaka kibali na wala huwezi kuipiga picha lakini ipo!!.
Entrance_to_ozersk.png
 
Asante kwa elimu mkuu,ila hicho kisiwa cha nyoka na sehemu ya kulipulia mabomu havina majina yake halisi?
 
Kuna visiwa huko india vinaitwa himalayas islands,kule wanaishi watu ambao hawajawahi kutana na binadamu wengine,wao wanaishi kivyao,hawana maendeleo wanaishi ki communalism kama kina bushmen ,kule ukienda wanakuua ,wapo kama wale cannibals wa kwenye movies za cannibal holocaust,,,

Serikali ya india imekataza watu kwenda huko
 
naomba mwenye maelezo zaidi ya chenobly atuwekee ulikuwa je mpka kinu kikapata ajali?
baada ya ajali mambo yapoje huko?
 
Back
Top Bottom