Usiandike kitu usichokijuwa, kampuni kubwa ndio zina mikataba angalau, lakini kampuni zetu hizi za kuganga njaa lindo la bunduki kwa mlinzi mmoja haizidi laki tatu kwa mwezi ndio pesa inalipwa kampuni kwa mlinzi mmoja mwenye bunduki, kwahiyo lindo lisilohitaji mlinzi kuwa na bunduki ni pungufu ya pesa hiyo.
Ukumbuke kuna gharama za uendeshaji kampuni pia.
Usije ukadhani nina kampuni ya ulinzi bali kuna jamaa yangu ana kampuni yake kwahiyo nafahamu vizuri.