Scolari ameibadilisha brazil

Scolari ameibadilisha brazil

Asanteni kwa mjadala mzuri.
Kuhusu timu kuwa na uwezo mzuri wa kushambulia, wataalam wa mpira wanasema njia nzuri ya 'kujilinda ni kushambulia' Falsafa hiyo imeenea sana kwenye mpira wa sasa. Mfano: Tazama mpira wa Barcelona na Spain: Utagundua kwamba timu hizo zina viungo na washambuliaji imara na wazuri kuliko walinzi. Fikiria beki kama Gerald Pique na golikipa Valdes, hawa watu wawili uwezo wao ni wa kawaida sana, kinachowaokoa ni kwamba timu 'zao', namaanisha Barcelona Cf, au Hispania zinakuwa na washambuliaji na viungo wazuri na hivyo mpira unachezwa zaidi katikati au kwenye lango la wapinzani. Mabeki wanakuwa na kazi ndogo tu ya kuondoa hatari ambazo hutokea mara chache tu!
 
Kuhusu safu ya kiungo ya Brazil, maoni yangu nafikiri mbali ya Luiz Gustavo(nambari 17) mchazaji wa timu ya Bayern Munich, nafikiri wanamhitaji RAMIRES. Wanahitaji mtu mwenye mbio, anayeweza kukimbia na mpira kuanzia katikati ya uwanja. Ukitazama mpira wa Brazil mashambulizi yote yanatokea pembeni, yanatokea upande wa kushoto upande wa Marcelo au upande wa Dani Alves. Tofauti na Brazil timu ya Hispania ina viungo wazurji wa ndani: Bousquet, Xavi na Iniesta.Wanacheza mpira katikati ya uwanja kabla ya kabla ya kupelekea pembeni. Siku hizi ni tumu chache zinaweza kulinda au kuzuia vizuri. Na kwa jambo hilo, ndo maana timu za Mourinho huwa imara sana, kwa sababu huyu bwana anajua kutengeneza ulinzi na kiungo cha timu: Chelsea 2004-2007: Carvalho, Terry, Gallas, Wine Bridge, Cole, Esiel Del Horno, Michael Essien, Claude Makelele, John Obi Mikel, Lampard, Joe Cole:Inter Milan: Lucio, Walter Samuel, Christian Chivu, Cambiaso, Thiago Mota, Maicon: REAL MADRID: Sergio Ramos, Contrao, Marcelo, Sami Khedira, Xabi Alonso, Rafael Veran. Wakati mwingine inategemea na falsafa ya timu au kocha. Kuna timu zinapenda kushambulia;Brazil & Spain. Kuna timu zinapenda kulinda zaidi; Italia & Germany.
 
Brazil ukiwaondoa Thiago Silva,Luis Gustavo na Fred hawana kitu wa kawaida tu
 
Back
Top Bottom