Schule in during Germany East Africa

Kweli ellar
Si ellar. Neno ni "Hel-ler". Hii picha ni Heller 1 ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Zamani ulizipata kwa wingi pale Masoko-Tukuyu. Hii ilikuwa kituoch cha jeshi la "Schutztruppe" (tamka shuts-tru-pe, jeshi lao) na wakati Waingereza walivamia mwaka 1916 Wajerumani walitupa sarafu zao ndogo kwenye ziwa la Masoko ambako watoto walizama chini na kuzi chukua kwa wingi.

soma zaidi: https://sw.wikipedia.org/wiki/Hela
 

Attachments

  • 1561191298266.png
    93.9 KB · Views: 35
  • 1561191312929.png
    93.9 KB · Views: 38
  • 1561191322312.png
    93.9 KB · Views: 29
  • 1561191350737.png
    93.9 KB · Views: 30
  • 1561191378097.png
    93.9 KB · Views: 28
  • Heller DOA.jpg
    49.4 KB · Views: 28
  • Heller DOA.jpg
    49.4 KB · Views: 35
Acha kubisha vitu usivyovijua. Google hata matamshi usikilize. Nimejifunza kijerumani baadhi ya maneno. Kila lugha ina misingi yake kwenye kusoma. Mfano, "r" kijerumani unajua inavyotamkwa?
Sentensi yako ya kwanza nakubali kabisa.
Sasa nakupa darsa bure (sitaki pesa). Silabi "-le" kwenye mwisho wa neno ni kile wanachoita "unbetonte Endsilbe". Unakubali,je? Isipikuwa lahaja chache za kusini ni kamwe "la". Kwa "Schule" kamwe, ninavojua.
Ukipenda kusikiliza matamshi, usiende google (kwao hujui kama ni sauti ya mtu au ya kompyuta),
jaribu hii:https://forvo.com/word/schule/
(Wajerumani wanne wanatamka neno "Schule")

Kuhusu "r" kuna tofauti sana kieneo. Watu wa kusini kama Bavaria na hao wa kaskazini sana wana "r ya ulimi mbele", kama Wahispania, au pia kama Wakenya wengi. Matamshi sanifu ni "r ya shingoni" inayofana na "gh" yetu katika "magharibi", "ghorub" (kama herufi a Kiarabu غ). Sehemu za magharibi kuna pia "r" kama Waeire au Marekani.
 
Hapo nakubaliana na wewe. Sema kujifunza German niliishia njiani kutokana na mambo mengi. Ila nimeangalia hata kwenye youtube "learn German with Jenny" nimeona maneno mengi yanayoishia na "e" yanasikika "a".
Uvyonijibu hapo kuhusu "r" inatamkwa kama "غ" , nimejidhirisha utakuwa vizuri kwenye lugha. Hata hizo link ulizonitumia imesikika direct "e" hapo?
 
Ndo unataka kubishana na Mwanamkiwi aliyelowea na kuoa Ujerumani?!
 
Ilikaa ki-madrasa zaidi.
Haya mavazi tulirithi kwa Waarabu ndiyo mavazi ya enzi hizo. Sikuwahi kumuona marehemu babu mzaa mama lakini picha zake alivaa kanzu ilhali alikuwa Mkristu. Hili lilikuwa Vazi la heshima
 
Hujaleta mfano. Ni zaidi maneno yanaoishia kwa "-er" (kama "Heller") ambako matamshi mara nyingi huelekea kwa "-a". Links nilizotuma zote ni mwisho "-le" kama e nyepesi (pole, si polee).
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…