Jahface kotto
Member
- Jun 3, 2016
- 26
- 8
Wadau naomba mnifahamishe nataka kujua. Schizophrenia ni nini na wanatambulika vipi watu waliokuwa nayo hapa duniani?
Mnamo tarehe 06/06/2006 nilipata maono nikiwa kule UESPANYA. Maono ya REVELATION. Na baada ya hayo maono kuna siku nilokuwa nimekaa kwenye PARK fulani nikiwa naota JUA kama ilivyokuwa desturi ya watu tunaoishi huku.
Nikiwa nimekaa kwenye bench naota JUA huku nikiwa naliangalia ghafla nikajihisi kitu nisichokijua bila ya kukiona kikitoka ndani ya JUA na kunipiga kwenye paji langu la uso na kujihisi km kimefumua kwa nyuma kwenye kisogo, kisha wkt huo huo nikaanza kusikia sauti ikoongea nami toka ndani ya JUA ikiniambia kuwa yeye ni MUNGU mkubwa mwenye namba 666 na amependezwa nami, kwahiyo kuna kitu anataka niuambie ulimwengu. Kwa kweli nilishangaa sana tukio hilo!
Sauti iliniambia mambo mengi kwakweli siwezi kuyaelezea hapa yote. Baada ya hapo hiyo sauti ikawa inanitokea kila mara lakini safari hii hiyo sauti ikawa naisikia kutoka ndani ya kichwa changu sio kutoka nje. Yaani sio km mfano wa kusikia sauti kutoka kwa mtu unaeongea nae, hapana, hiyo sauti nilikuwa safari hii nasikia ndani ya kichwa changu.
Baadae nikaja kusafiri na kwenda kuishi Ujerumani na sasa hivi nna miaka kumi tangu niwe na hilo tatizo cha ajabu ile sauti bado nnayo tu.
Nimejaribu kwenda hospitari lkn bila ya vipimo kwa kusikiliza maelezo yangu tu wakaniambia kuwa nna hiyo SCHIZOPHRENIA. Sasa basi bado najiuliza ni nini hiyo SCHIZOPHRENIA, na kama ni ugonjwa, je kuna uwezekano mtu kupata ugonjwa toka ndani ya JUA? Na cha ajabu madoctor wameniambia kuwa nisimwambie mtu yeyote kuhusu hili tatizo.
Tafadhali waungwana naomba mnishauri nifanye nini ili hii sauti initoke kichwani maana naona wazungu wameshindwa. Pia naumia sana sababu sauti inaniambia mambo mengi ambayo mengine hayapaswi hata kutambulika kwa binaadamu anaendelea kushi hapa duniani!
Asanteni natumaini mtanisaidia!
==============================
MAJIBU

maelezo ya ki layman from wikipedia.
Skizofrenia" ni ugonjwa wa akili unaosababisha fikira na hisia zisizo za kawaida.Watu wengi walio na ugonjwa huu husikia yasiyokuwemo ([kuota njozi]). Watu hawa huwa na woga na makisio yasiyoeleweka. Watu hawa pia wanaweza kuamini mambo ya kiajabu na yasiyoeleweka . Watu hawa wanaweza kuzungumza na kuwaza bila mantiki. Watu hawa huwa na ugumu wa kuhusiana na watu wengine inavyofaa au kudumisha kazi. Dalili kwa kawaida huanza katika ujana baada ya umri wa miaka 16.
Vipengele kadhaa muhimu vinaweza kusababisha skizofrenia. Vipengele hivi ni pamoja na uhusiano wa kijamii na mtu aliye na hali hii, mazingira ya hapo awali ya mtu, mfumo wa neva unaodhibiti mwili na akili ya mtu, na taratibu za kiakili na kijamii. Baadhi yadawa, zikiwemo dawa za kuagiziwa na daktari, zinaweza kusababisha dalili au kuzifanya mbaya zaidi. Utafiti wa hivi sasa unaangazia jukumu la mfumo wa neva ingawa hakuna mtu aliyepata kisababishi hata kimoja cha kiogani kilichojitenga. Miungano mingi ya dalili zinazoweza kutokea imepelekea mjadala kuhusu iwapo ugonjwa huu ni hali moja au hali nyingi tofauti. Neno "skizofrenia" linatokana na maneno mawili ya Griki yanayomaanisha "kugawanya" na "akili". Hata hivyo, skizofrenia haimaanishi "akili iliyogawanyika" wala kusababisha watu kuwa na nafsi nyingi (au "zilizogawanyika"). Watu wengi hushindwa kutofautisha skizofrenia na hali kama hizo
Matibabu hasa ni kwa kutumia dawa ili kupunguza dalili kuu. Dawa hizi husitisha nyendo katika sehemu za ubongo zinazochakata kemikali inayoitwa dopamine. (Baadhi ya dawa hizi pia husitisha shughuli katika sehemu ambazo huchakata kemikali inayoitwaserotonin.) Matibabu ambayo pia ni muhimu ni pamoja na therapi ya kiakili, usaidizi katika kutafuta na kudumisha kazi na pia marekebisho ya kimahusiano. Katika matukio makubwa ambapo kuna hatari kwa mtu binafsi na watu wengine, mtu anaweza kuhitaji kulazwa hospitalini. Hatua hii inaweza kuchukuliwa kwa idhini au bila idhini ya mtu huyu. Hata hivyo, matukio ya kulazwa hospitalini siku hizi yamepunguka na kuwa nadra ikilinganishwa na hapo awali.
Skizofrenia hudhaniwa kuathiri hasa michakato ya kiakili, lakini pia huchangia matatizo ya muda mrefu pamoja na mwenendo na hisia. Watu walio na skizofrenia wana uwezekano wa kuwa na hali zingine pia, zikiwemo mfadhaiko na wasiwasi. Takriban asilimia 50 ya watu walio na skizofrenia hutumia madawa ya kulevya wakati mmoja maishani mwao. Matatizo ya kijamii kama vile ukosefu wa kazi kwa muda mrefu, umaskini na ukosefu wa makao hutokea mara nyingi. Kwa wastani, watu walio na skizofrenia hufa miaka 12 hadi 15 mapema zaidi ya wale wasio na hali hii: Watu walio na skizofrenia wana matatizo ya mwili mengi zaidi, na wana kiwango cha uwezekano wa kujiua cha asilimia 5 zaidi ya watu wa kawaida.