Sayansi ya uchawi na umbile lake

Sayansi ya uchawi na umbile lake

Aise umeenda deep sana kwa Kweli uchawi ni kitu kibaya kabs na hakifai kujifundisha wala kufundishwa
 
Binadamu yeyote yule kama alivyo kiumbe hai wa namna yeyote yule kifizikia ana muda wa kuishi na kufa hata afanye nini.

Ila linapokuja suala la kifo kuna kifo ambacho ni natural death kwa maana ya kifo halisi ambacho hakiepukiki na kifo kilichosababishwa na mazingira ya kichawi, visasi, ajali n.k

Roho zinazokatishwa maisha yake hapa duniani kabla ya muda wake ule rasmi kutimia uendelea kusurvive pasipo mwili unaoonekana kwa macho ya kawaida katika plane ya chini ambayo ni mbingu ya giza totoro (tabaka lililo chini ya mamlaka ya malaika muasi/shetani na jeshi lake)

Roho hizi mara nyingi huendelea kutangatanga bila makao katika plane giza na zingine ni zile ambazo zime-hold ndani yake chuki, simanzi, visasi,maagano n.k

Sasa unapokuwa kama binadamu huna mwili tena umebakia roho na roho yako haijapanda katika plane maalumu ya watu wanaotambulika kuwa wametangulia mbele za haki (waliopumzishwa), unakuwa kwenye mtihani wa shetani ukiwa huna namna ya kujitetea.

Kinachoweza kuiokoa nafsi yako isiteseke au kutumiwa na wachawi katika shughuli zao za kishirikina ( na kunyakuliwa na malaika wenye makazi yao ndani ya tabaka la mwanga) itategemea sana maisha uliyoyaishi pindi ukiwa hai kabla ya kufikwa na mauti hayo (ndiyo maana tunaimizwa muda wote kuishi vyema na kwa upendo, kutowazia mabaya na tusamehe mara kwa mara)

Kiufupi kama unaamini mtu aliumbwa na Mungu basi mwenye kuweza kuichukua pumzi hiyo ni Mungu peke yake na siyo kiumbe mwingine yeyote.

Isipokuwa viumbe hawa tusiowaona wanao uwezo tu wa kufanya mazingaombwe ya kuufanya mwili wako usiwe visible kifizikia ili wakakutumikishe wapendavyo katika ulimwengu wao wa kishirikina mpaka ile siku rasmi ya kifo chako itakapowadia.

Hivyo basi mchawi analitambua vyema hilo kuwa biashara ni mbadilishano kuwa leo anakula yeye kesho analiwa yeye na hana namna ya kulikwepa hilo.
Hii ya kutumikishwa na hao viumbe baada ya kifo bandia au kifo mazingaombwe ndio inayowakuta ndugu zetu wa utajiri wa ndagu (kinga) tribe baada ya kupewa jini limpatie mali kwa miaka 5 then ana muuwa na kuanza kumtumikisha yey mpaka atakapopata natural death SAS swali linakuja kwann waganga hawawaambii ukweli kuwa baadaye ukifa kibao knageuka unatumikishwa wew na mizimu
 
Kuomba viumbe roho "WEMA" msaada funguo ni "kutenda mema" sasa itategemea na medium au njia unayotumia wewe kutenda mema ili uombe mema yatokee katika maisha yako mfano wengine usali katika imani zao wakihusisha miungu, wengine ujali wenye uhitaji nakusaidia wasio jiweza,wengine uishi kwa upendo, n.k

Nani kasema uchawi haufanyi kazi benki au vitani, kote huko uchawi ufanya kazi yake vyema tu na kinachozuia uchawi usionekane kufanya kazi huko ni kwa kuwa uchawi tiyari uko installed maeneo hayo ukifanya kazi yake, sasa kuna haja gani ya kuongeza juu ya
Kama vinalindwa na uchawi, kwa nini basi wanawekeza kwenye njia za kiulinzi za kisayansi katika kulinda na kupigana?

Mfano benki wanaweka csmera, walinzi wenye silaha, vioo vigumu, na control nyingine kwa nini wadingetumia uchawi

Na vitani kwa ninj wanawekeza kwenye teknolojia ya silaha na mafunzo ya kijeshi wakati uchawi ungefanya kazi
 
Umegusia juu juu,wape watu experience in the day of taking oath inakuaje???
JF ni jukwaa la umma hivyo siwezi ongea mambo ambayo naona hayana faida kwa jamii, labda kama wewe unaweza ongea hivyo vya ndani funguka tu uwanja ni wako ila dhumuni langu mie ni kuadilisha kwa kugawa maudhui ninayoona yanafaa kulingana na muktadha.
 
Mkuu unaogopa??????Au upo ule upande mwingine????
 
Ni swali fikirishi kidogo kwa kuwa asiyejua chochote na wala ajayaishi maisha yake kwa kuchagua upande hana chakupoteza wala kuongeza pindi akifa,

Isipokuwa ikiwa hukumu yake itaamuliwa na pande mbili kinzani basi watamjaji kwa kigezo cha matendo yake je yalikuwa mema au mabaya?

Kama itaonekana pengine somo alilopaswa kujifunza akulielewa then atapewa second chance kwa wale wanaoamini reincarnation wanajua ninachomaanisha.

Na kwa namna nyingine mi nafikiri mtu huyu kwa upande mwingine amejiepusha au kajiondosha katika vifungo au shtaka lisilomuhusu na kujali muda wake kuishi kama binadamu/kiumbe hai asiye na ushirika na chochote kile akiishi kama asili inavyotaka hivyo hawajibiki kwa yeyote wala kuwajibika kwa chochote kile pindi akifa yameishia hapo.
Nashukuru mkuu, je huchukua wastani wa miaka mingapi mtu kupata tena mwili yaani kuzaliwa tena katika reincarnation?
 
Hii ya kutumikishwa na hao viumbe baada ya kifo bandia au kifo mazingaombwe ndio inayowakuta ndugu zetu wa utajiri wa ndagu (kinga) tribe baada ya kupewa jini limpatie mali kwa miaka 5 then ana muuwa na kuanza kumtumikisha yey mpaka atakapopata natural death SAS swali linakuja kwann waganga hawawaambii ukweli kuwa baadaye ukifa kibao knageuka unatumikishwa wew na mizimu

Waganga kama walivyo maajenti wengine wa kuzimu lengo lao nikuakikisha kuwa jehanamu kunazidi kufana huku wakipata na faida ya kujitengenezea kipato chao kwa ajili ya maisha yao katika ulimwengu wa mwili, sasa ni mfanyabiashara gani ambaye yupo radhi kumwogopesha mteja wake ili asinunue bidhaa yake?

Kumbuka katika maisha yetu hakuna kitu chenye nguvu zaidi ya desire ila "tamaa ya ndani' au ubinafsi wa nafsi" kuitaji kuwa na vitu vingi au uwezo wa ziada kuliko mwingine au kumiliki na kucontrol wengine.

Unapoenda kwa mchawi kutengenezewa utajiri kwa njia za shirki kuna masharti/maagano ambayo ni lazima ukubali kuyafuata mara nyingi uusisha ibada za makafara.

Baadhi uambiwa kabisa lifespan ya mkataba wake lakini kutokana na tamaa na ile kiu ya kufanikisha jambo lake hawezi hoji zaidi ya hapo, yeye muda huo focus nikufanikiwa tu.

Na kwa kuwa mchawi anaelewa pia kuwa kuzimu ni shughuli pevu na kadri unavyopata mshirika nakum-add kwenye kundi ndivyo ambavyo unajiongezea pointi za umwamba na heshima, basi anakuwa hana haja ya kukutonya kwa wakati huo rungu litakalokupata usoni baadae badaya yake anakolezea tu pale penye tamaa yako.
 
Kumbe ndivo na yy ana rank anapanda uko kuzimu
Na kuna mganga mmoja aliniambia kuwa huu utajiri wa kishirikina ni kuwa kama utakuwa utajiri unaendelea baada ya kufa mmiliki wa kwanza madhara yake yale yanawatafuna hata hawa watakaorithi hili likoje
 
Kuna jamaa kakuomba umdadavulie hapo juu ukamwambia kuna mambo hatakiwi kujua!! Kwanini wewe hufunguki unamtaka tu jamaa ndo atoe nondo??
Jamaa akifunguka itakua poa,mimi nitakua nachangia changia tu.Jamaa ni member pande zile ila anaweza kua hajui,l na umember wake ni wa light layer.Mambo yasiyoonekana kwa macho ya nyama yana layer,s nyingi tu mkuu
 
Kuna jamaa kakuomba umdadavulie hapo juu ukamwambia kuna mambo hatakiwi kujua!! Kwanini wewe hufunguki unamtaka tu jamaa ndo atoe nondo??
Uchawi haufayi kuujua na wala kujifunza huyo akikwambia hivyo anajua kwa hyo kukusaidia kwake anakwambia hivyo ila ukiujua ni majuto tu na huwezi toka inabidi upambane huko huko
 
Uchawi haufayi kuujua na wala kujifunza huyo akikwambia hivyo anajua kwa hyo kukusaidia kwake anakwambia hivyo ila ukiujua ni majuto tu na huwezi toka inabidi upambane huko huko
Mkuu asante sana kunisaidia,jamaa anataka kujua vitu vya sirini saaana ambavyo siri zake azisemwi sababu ya viapo.
 
Uchawi haufayi kuujua na wala kujifunza huyo akikwambia hivyo anajua kwa hyo kukusaidia kwake anakwambia hivyo ila ukiujua ni majuto tu na huwezi toka inabidi upambane huko huko
IShu ni kumtaka jamaa afunguje hiki na kile kwanini asifunguke yeye kama anajua kwa faida ya wengi.

Nelson Jacob lushasi
 
Kumbe ndivo na yy ana rank anapanda uko kuzimu
Na kuna mganga mmoja aliniambia kuwa huu utajiri wa kishirikina ni kuwa kama utakuwa utajiri unaendelea baada ya kufa mmiliki wa kwanza madhara yake yale yanawatafuna hata hawa watakaorithi hili likoje

Ndiyo maana ya maagano, kama mtashindwa kuendeleza masharti yaliyokuwa yakifanywa na mmiliki wa mwanzo ina maana madhara yaliyokuwa yampate ikiwa atavunja makubaliano lazima na nyie yawa-adhibu.

Na kama mtaendeleza mali hizo kwa kufuata na kuzingatia masharti yake basi mmekubali nyie na kizazi chenu kuwatumikia majini hao wanaowapeni mali na mtaendelea kuwatumikia kizazi hata kizazi kwa kuwa wao wanaishi umri mrefu kuliko binadamu, jini mmoja anaweza ishi wastani wa miaka 1000 na zaidi hivyo jiulize ni vizazi vingapi vitamtumikia jini huyo mmoja.

Lakini mara nyingi mali za namna hii utoweka katika mazingira yasiyoweza kuelezeka punde tu anapofariki kifo halisi muhusika kwa kuwa mali hizi si vitu katika uhalisi bali viini macho tu.
 
Nashukuru mkuu, je huchukua wastani wa miaka mingapi mtu kupata tena mwili yaani kuzaliwa tena katika reincarnation?
Reincarnation haibashiriwi kwa miaka bali ni karma, unaweza toka papo hapo na ukaamia katika mwili mwingine wakati huo huo kuna uwezekano waweza kaa benchi hata miaka milioni ujapata mwili unaokufaa kutimizia kusudi lako.

Hata hivyo uwe umerudi duniani mapema au umechelewa kurudi yote ni sawa kwa kuwa kumbukumbu zako zote za nyuma zinakuwa zimefungwa na pale unapozaliwa unaanza kama mtu mpya asiye kumbuka chochote.
 
Safi mkuu, vipi kuna namna ya kuzipata hizo kumbukumbu? Kwa mfano shetani anazo sasa unaweza bargain nae akakupatia?
 
Safi mkuu, vipi kuna namna ya kuzipata hizo kumbukumbu? Kwa mfano shetani anazo sasa unaweza bargain nae akakupatia?
kwanini shetani awe na kumbukumbu zako? katika imani ya kibudhaa au watu wanaofanya meditation hakuna kitu kinaitwa mungu au shetani zaidi ya symbolism isipokuwa ufahamu wetu ndiyo limitation pekee ya kufikia maarifa tunayoyahitaji.

Njia nyepesi yakuzirudisha kumbukumbu zako, nikupitia kuamua maamuzi magumu kama binadamu yakuianza safari ndefu na ngumu ya kiroho kwa kujiweka wakfu (kujitakasa) na kufanya tahajudi kwa dhati.

Kwa namna hiyo ndipo ufahamu ufunguka nakuvunja zile layers au matabaka ya ufahamu (planes) ambazo tunaziita kiimani mbingu ambayo ndiyo mipaka au mageti yanayotudhibiti tuendelee kuishi maisha haya yakujirudia-rudia katika plane ya chini kabisa ya ufahamu.
 
Back
Top Bottom