Sayansi ya hali ya hewa haiaminiki

Uliza_Bei

JF-Expert Member
Feb 17, 2011
3,216
988
Nimekuwa nikifuatilia utabiri wa hali ya hewa kwa muda wa miaka 10 sasa lakini nimeamua kuacha kuuamini baada ya utabiri wake mwingi kutokuwa sahihi. Watakuambia Tabora kutakuwa na mvua na vipindi vya jua! Mara kutakuwa na upepo mkali baharini! Na mvua za mafuriko walizotutangazia hadi sasa tusione,badala yake jua kali. Labda waseme radar ya Mramba wanayotumia haifai: vinginevyo nimeacha rasmi kuwaamini: nawaona watabiri tu kama shehe Yahaya alivyokuwa. Waje waseme kwanini tuwaamini.
 
Bado ulikua unawaamini hawa jamaa! Mwaka huu unaweza kuwa na jua kali sana kwa sababu utabiri wao huwa kinyume wala usihangaike mkuu
 
Hawanana lolote hawa,they are just being used by the Freemasons to create fear among the people,shame on them.(Quote,"Nimekuwa nikifuatilia utabiri wa hali ya hewa kwa muda wa miaka 10 sasa lakini nimeamua kuacha kuuamini baada ya utabiri wake mwingi kutokuwa sahihi. Watakuambia Tabora kutakuwa na mvua na vipindi vya jua! Mara kutakuwa na upepo mkali baharini! Na mvua za mafuriko walizotutangazia hadi sasa tusione,badala yake jua kali. Labda waseme radar ya Mramba wanayotumia haifai: vinginevyo nimeacha rasmi kuwaamini: nawaona watabiri tu kama shehe Yahaya alivyokuwa. Waje waseme kwanini tuwaamini.[/QUOT
 
Bado ulikua unawaamini hawa jamaa! Mwaka huu unaweza kuwa na jua kali sana kwa sababu utabiri wao huwa kinyume wala usihangaike mkuu

Alaa kumbe wewe ulishaachana nao kitambo...nimechelewa lakini nimeamua tayari
 
Hawanana lolote hawa,they are just being used by the Freemasons to create fear among the people,shame on them.

Kweli nimeamini wanawatisha watu ili kundi fulani litumie mwanya huo kuonea wengine
 
Siyo Waongo hii ni Natural Science ambayo kila tukio lina Explanation hapa ni Fizikia na Mathematics calculations Mnaoidharau Meteorology ni Vilaza wa Masomo ya Science na misingi yake. Hawaelezi kwa misingi ya Super Natural ya S. Yahya
 
aiseee babaangu hawa jamaa huwa wanaona mbali wanacho tabiri kitatokea mwaka 3 ijayo
 
Siyo Waongo hii ni Natural Science ambayo kila tukio lina Explanation hapa ni Fizikia na Mathematics calculations Mnaoidharau Meteorology ni Vilaza wa Masomo ya Science na misingi yake. Hawaelezi kwa misingi ya Super Natural ya S. Yahya

Kweli kabisa ni elimu ya kweli, uzuri wa Tanzania ni kuwa hatupo kwenye eneo lenye matukio sana, lakini kwa nchi za ulaya na marekani hiyo kitu ya kutabiri hali ya hewa ni serious sana na ndio maana kila saa kwenye habari zao lazima waonyeshe hali ya hewa kwani huwa inabadilika kila muda
 
Sema sayansi ya hali ya hewa kwa Tanzania haiaminiki...nchi zingine inafanya kazi tu...tujiulize kuna nini Tanzania?
 
They always dont get right, baada ya kutafuta kwanini mnaanza kuwatetea, sababu utabiri sahihi ulitakiwa kuzingatia errors na assumptions zote. Wamewataka watu wachukue tahadhari ya mvua kubwa kumbe wanaamanisha jua kali sasa mnataka tusiseme sababu hatujui hisabati na fizikia.

Mbona nchi nyingine wanapatia, kipindi fulani nilikuwa nagunga nyundo Delhi na huko ndio nilijifunza umuhimu wa utabiri wa hali ya hewa manake sometimes unaambiwa kesho kutakuwa na ukungu mpaka saa nne msitoke na ndege hazitotua halafu inakuwa kweli ngoja huku uone, sio Dr. Mhita wa Dr. Kijazi balaa tu.

Hawa jamaa wangekuwa effective wangeleta faida kubwa sana kwa sekta ya kilimo, leo hii wakulima wanalia hasara kila mahali kutokana na kujua ni aina gani ya mazao wapande wapi na kwa wakati gani. Matokeo yake watu wa kibaha wanalalamika mahindi yao yameungua kwa jua.
 
Siyo Waongo hii ni Natural Science ambayo kila tukio lina Explanation hapa ni Fizikia na Mathematics calculations Mnaoidharau Meteorology ni Vilaza wa Masomo ya Science na misingi yake. Hawaelezi kwa misingi ya Super Natural ya S. Yahya

anayetoa utabiri 90% inakua kinyume chake huku mathematics na physics anazo bomba ndo unasema wasioamini ni vilaza au kilaza mwenyewe unayeendelea kuamini vitu ambavo havitokei japo vinasemwa!,kujua kwamba wanakosea wala haihitaji kujua physics na hesabu kama unavodai prof.wa hesabu na physics.
 
Back
Top Bottom