:embarrassed: Kuna baadhi ya watu wenye elimu ya juu Tanzania ambayo waliipata kutokana na wazee wao masikini kuwalipia wasome, pili kutokana na kukaa usiku kucha wakisoma na kukalili ili wafaulu mitihani. lakini wakisha faulu mitihani ya kukalili , wanasahau kabisa nani aliwapa uwezo wa kwenda chuo kikuu, wanasahau kabisa kwamba ni pesa za walipakodi wakiwemo wazazi wao ndizo zilitumika ili waweze kupata hiyo elimu. Matokeo yake ni kwamba wakisha faulu na kupewa hizo shahada, wanasahau kabisa walikotoka, badala yake wanatumia hiyo elimu kuwaghalibu waliowasomesha, wanatumia hiyo elimu kulidanganya taifa, wanatumia hiyo elimu kuliibia taifa na wananchi.
Hii ni kweli ya huyu Chenge, amesahau kabisa nani alimpa hiyo elimu na ni pesa za nani zilitumika kumuelimisha, matokeo yake analaghai, analiibia taifa, anamtilia kinga mkewe baada ya kuwaua hawala zake na kudai eti ni yeye ndiye alisababisha ajali.
Huyu Chenge pamoja na wasomi wengine wengi waliomo CCM, wametumia mbinu, wizi na jeuri wakashinda uchaguzi kwa kutumia karatasi za kura za bandia - kama zile ambazo Makamba na JK walipeleka Shinyanga na kudai itangazwe kuwa CCM ilishinda wakati hata wana CCM wa Shinyanga walijua wazi kuwa CHADEMA ilishinda.
Nasikitika kusema kuwa sasa hivi Tanzania inaongozwa na wezi, wahuni, mafisadi na walaghai. Washukuru kuwa watanzania ni waoga na wapole, hawawezi kuchukua hatua kama za Kenya au Ivory Coast, wapowapo tu, wanalalamika na wakati viongozi wanaendelea kula nchi kwa mikataba yao mbalimbali ya wizi na ufisadi.
Acha waendelee, iko siku hayo yote wayatendayo pamoja na wake za na watoto wao, yatawatokea puani siku moja. KUMBUKA: "MWOGA UKIMFUKUZA ATAKIMBIA, AKISIMAMA BASI UJUE KUNA MAWILI, KUFA AU KUPONA"