Chenge kupoteza ubunge 2015? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Chenge kupoteza ubunge 2015?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Rutashubanyuma, Dec 31, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Chenge kupoteza ubunge 2015?
  Thursday, 30 December 2010 21:25

  [​IMG]mbunge wa Bariad Magharibi Andrew Chenge

  Waandishi Wetu
  HUKUMU ya kifungo cha miaka mitatu jela au faini ya Sh700,000 aliyopata mbunge wa Bariad Magharibi Andrew Chenge kwa kosa la matumizi mabaya ya barabara na kusababisha vifo vya watu wawili, inaweza kumkwamisha kugombea tena ubunge katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

  Chenge ambaye ni Mwansheria Mkuu wa zamani wa Serikali na Waziri katika awamu ya kwanza ya uongozi wa Rais Jakaya Kikwete, alitiwa hatiani juzi na mahakama ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Kivukoni-Kinondoni jijini Dar es Salaam, katika hukumu iliyosomwa na Hakimu Mkazi Mfawidhi, Kwey Rusema.

  Hata hivyo Chenge alifanikiwa kulipa faini hiyo, hivyo kukwepa kwenda gerezani na akachiwa huru. Katiba ya Tanzania kifungu cha 67 kifungu kidogo cha (2) (c) kinabainishakuwa mtu hatateuliwa kuwa mbunge:
  "Ikiwa mtu huyo amehukumiwa na mahakama yoyote katika Jamhuri ya Muungano na kupewa adhabu ya kifo au ya kufungwa gerezani kwa muda unaozidi miezi sita kwa kukutwa na hatia ya kosa lolote, vyovyote linavyoitwa, linaloambatana na utovu wa uaminifu.

  " Kinafungu hicho kinatafsiriwa na baadhi ya wadau wa masuala ya siasa kuwa kimemwondolea sifa Chenge kugombea ubunge mwaka 2015. Mbali na kuwa mbunge wa jimbo la Bariad Magharibi, Chenge ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM (Nec) na Kamati Kuu (CC) ya chama hicho na ni Mwenyekiti wa Kamati ya Maadili ya CCM.
  Hata hivyo mbali na maoni ya wadau hao, kitendo cha Mahakama kumwona Chenge ana kosa la kuendesha gari lisilokuwa na bima, linamfanya mwanasheria huyo wa zamani wa serikali kukosa sifa ya uaminifu inayowazuia watu kuteuliwa kuwa wabunge. Lakini watalaamu kadhaa wa sheria waliochambua kifungu hicho cha Katiba, wameeleza kuwa kosa alilohukumiwa Chenge halimwondolei sifa za kuendelea kuwa mbunge au kuteuliwa tena katika uchaguzi mkuu ujao.
  Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Dk Sengondo Mvungi alisema kwa mujibu wa sheria Chenge ataendelea kuwa mbunge kwa sababu hajatumikia kifungo na badala yake amelipa faini.

  Mvungi ambaye ni mtaalamu wa Katiba alisema, “Kama angeenda moja kwa moja kutumikia kifungo asingekuwa na sifa ya kuitwa mbunge na hata uchaguzi ujao asingeweza kugombea tena lakini, kwa sababu kalipa faini tu, hajapoteza ubunge wake.”

  Mtalaamu mwingine wa Sheria Profesa Abdallah Safari alifafanua kwamba kama zingekuwa zinatumika sheria za zamani, kwa hukumu hiyo, Chenge asingeweza kugombea tena ubunge. “Unajua hata sheria mpya ya uchaguzi sijaipitia kuona inasemaje kuhusu suala hili lakini, ninachoweza kukumbuka ni kwamba sheria ya zamani ya makosa yote yaliyokuwa yakihusu ‘mortality’ ulikuwa huwezi kugombea tena. Sasa sijui kwa sheria hii ya sasa,”alisema Profesa Safari.

  Wakili wa Mahakama Kuu, Harlod Sungusia alisema hukumu ya Chenge haina madhara yeyote kwake katika nafasi zake kisasa. Sungusia ambaye alitumia muda wake kukosoa sheria na katiba za Tanzania kuwa ni mbovu alisema kwa mujibu wa sheria, hakimu alifanya kazi yake bila ya tatizo lolote. “Hukumu ilikuwa sahihi wala hakimu hakukosea kuitoa. Kilichopo pale ni kwamba makosa aliyokutwa nayo Chenge si ya kukosa uaminifu hivyo, hayamfutia nafasi yake ya kuendelea kuwa Mbunge,”alisema Sungusia ambaye alisema hakimu pia alitakiwa kuongeza kipengele cha fidia kwa wafiwa.

  Katika maoni yake hayo Sungusia aliishukia katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania akisema ina matatizo na hilo ndilo zao la sheria mbovu zenye kutoa hukumu kama hiyo. “Ndugu zangu tunaposema sheria zetu ni mbovu ni pamoja na hii.

  Katika hilo hakimu alifanya kazi yake kwani yeye hufanya kazi ya kutafisili sheri tu. Lakini ukitazama uhalisia ndipo utagundua kuwa sheria zetu zina matatizo,”alieleza Sungusia. Sungusia alitoa mfano wa mtu aliyeiba Shati kuwa anaweza kutupwa jela hata miaka saba lakini, kosa kama alilokutwa nalo Chenge, likabaki na adhabu ndogo. Mkurugenzi wa Habari na Uenezi wa Chadema Erasto Tumbo alisema hukumu iliyotolewa dhidi ya ya change haina matatizo ingawa alisema imeongeza kilio kwa wafiwa.

  “Hukumu hiyo haina tatizo lolote na hakimu alitimiza wajibu wake lakini, imeongeza kilio mara mbili kwa wafikiwa kwa kuwa watu hao hawatalipwa fidia,”alisema Tumbo. Tumbo alifafanua kwa wafiwa hawatalipwa fidia kwa kuwa gari lililowagonga halikuwa na bima. Mwanasheria maarifu hapa nchini Alex Mgongolwa, alisema kwa sheria zilizopo, Chenge ataendelea kuwa Mbunge kwa sababu ametiwa hatiani kwa makosa ambayo hayahusiani na uaminifu.

  Alisema kama angehukumiwa kwa kosa linalohusiana na uaminifu kama vile wizi au rushwa, nafasi yake ya ubunge katika jimbo la Bariadi Magharibi angeipoteza. Katika kesi hiyo Chenge alishtakiwa kwa makosa manne; kuendesha gari kwa uzembe, kusababisha vifo vya watu wawili, kuharibu mali na kuendesha gari isiyokuwa na bima.

  Awali hukumu dhidi ya kiongozi huyo ilikuwa isomwe Desemba 16, mwaka huu, lakini iliahirishwa hadi jana kutokana na kile ambacho hakimu Rusema alisema kuwa ni Chenge kuwa safarini jijini Mwanza alikoenda kuhudhuria msiba.
  Hatimaye kesi hiyo ilifikia tamati yake rasmi jana baada ya machakato wa kusikilizwa kwake uliochukua karibu miaka miwili kukamilika.

  Ilidaiwa mahakamani hapo kwamba Machi 27 mwaka 2009 katika makutano ya barabara ya Haileselasie na Ali Hassan Mwinyi eneo la Morogoro Store jijini Dar es Salaam, Chenge aliigonga bajaji na kuwaua wasichana wawili waliokuwa abiria kwenye bajaji hiyo; Beatrice Constantine na Victoria George. Kesi hiyo ilifunguliwa mahakama hapo kwa mara ya kwanza Machi 31 mwaka 2009 na kuanza kusikilizwa mwezi Aprili mwaka 2010.

  Akitoa hukumu ya kesi hiyo juzi, hakimu Rusema alisema mahakama imeona Chenge ana hatia katika makosa yote manne na hivyo kumtoza faini ya Sh700,000 ama kifungo cha miaka mitatu jela. "Katika kosa la kwanza na la pili, mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya Sh 250,000 kwa kila kosa au kifungo cha mwaka mmoja jela kwa kila kosa hilo," alisema Hakimu Rusema. Aliongeza "Katika kosa la tatu na kosa la nne, mshtakiwa atalipa Sh 100,000 kwa kila kosa au kifungo cha miezi 6 kwa kila kosa hilo.

  Hivyo, atatakiwa kulipa jumla ya Sh 700,000 kwa makosa yote au kwenda jela miaka mitatu." Kabla ya kusoma hukumu hiyo hakimu Rusema alimpa Chenge ambaye alikuwapo mahakamani hapo nafasi ya kujitetea, lakini badala yake alisimama wakili wake. Akitoa utetezi wa mtuhumiwa huyo wakili Senen Mponda alisema," Hili ni kosa la kwanza kwa mshtakiwa. Mshtakiwa ni kiongozi wa umma na kuhusu bima ilikuwa bahati mbaya.

  " "Naomba apunguziwe adhabu ili apate kuendelea na shughuli zake za kuutumikia umma." Awali ilielezwa mahakamani hapo kuwa Machi 27 mwaka 2009 kati ya saa 8.15 na 8.30 usiku katika eneo la Oyesterbay, makutano ya barabara ya Haile Selasie na Ally Hassan Mwinyi, Chenge akiwa anandesha gari binafsi aliigonga bajaji hiyo na kusababisha vifo vya watu wawili. Ilielezwa kuwa Chenge aliigonja bajaji hiyo akiwa na gari aina ya Toyota Hillux Double Cabin wakati akirudi nyumbani kwake akitokea klabu ya British Legion akiwa kwenye mwendo wa kati ya ya kilomita 70 hadi 100 kwa saa.

  Fidelis Butahe na Hussein Issa, Raymond Kaminyoge, Geofrey Nyang’oro
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Suala hili itabidi lirudishwe mahakama kuu kwa ufafanuzi wa ziada nijuavyo mimi ukishafungwa au kutumikia adhabu ya kifungo kinachozidi miezi sita tayari raia huyo amepoteza sifa ya kuwa mbunge sio tu katika kugombea nafasi hiyo .....kama inavyotafsiriwa hapo..............au kusomeka hapo........haiwezekani sifa za kugombea zitofautiane na sifa za baada ya kuwa mbunge...........huo ubaguzi sidhani kama ndiyo ilikuwa ni nia ya waasisis wa katiba hiyo..................
   
 3. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #3
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Hatia ya makosa ya jinai haitofautishi aina ya makosa kama dhana hii inavyojaribu kujengwa hapa................hakuna ubaguzi wa hatia ya jinai kwenye sheria zetu...............kinachoangaliwa ni kifungo alichokitumikia na Mheshimiwa Chenge kwa kubali kulipa faini ya laki saba yamaanisha ametumikia kifungo cha miaka mitatu na hivyo kupoteza sifa ya kuwa Mbunge...........................period..........
   
 4. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #4
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  Hapa pia ninaona kuna upotoshaji kwa sababu waathirika na Chenge bado waweza kumfungulia kesi ya madai kwa kuwasababishia hasara ya kuwapoteza ndugu zao kwa ajali na kuitumia hukumu hiyo hiyo ambayo ilimtia hatiani kwenye makosa hayo.......sijui tafsiri za kuona hukumu ya kesi ya kijinai pia imeshughulikia kesi ya madai imetoka wapi?
   
 5. GWeLa 2003

  GWeLa 2003 Member

  #5
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  bila ya katiba mpya tutaendelea kuona hukumu mfu kwa public figures..chenge
  alitakiwa afungwe jela miaka mi5 na faini ya 700,000/=

  hakuna kiongozi ambaye ameshawahi kupata adhabu kali..bali wanaendelea kuenjoy the
  wholly system..jikumbushe kesi ya Ditopile, liyumba,zombe
   
 6. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #6
  Dec 31, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 157,528
  Likes Received: 415,716
  Trophy Points: 280
  hawa wasomi ni wachovu sana yaani wanataka kusema mwenye nacho amelindwa na sheria zaidi ya asiyenacho.....................yaani kama Chenge angelikuwa hana hela na akaenda kutumikia kifungo hicho basi angelipoteza haki ya kuwa Mbunge lakini kwa vile alikuwa ana hela sheria imembeba ataweza kuendelea kuwa Mbunge.............................

  Hizo tafsiri siyo za kweli hata chembe......................katiba yetu imekataza ubaguzi wa aina zote ikijumuisha ule wa kipato...............Chenge anahadhi sawa na ya mtu aliyetumikia kifungo cha miaka mitatu baada ya kukubali kulipa faini na hivyo hana sifa ya kuendelea kuwa mbunge...............period..............the rest is simply garbage......................
   
 7. GWeLa 2003

  GWeLa 2003 Member

  #7
  Dec 31, 2010
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wanajamvi naomba mnieleweshe kwa hili, tuchukulie chenge asingekuwa na hiyo lakisaba then akafungwa
  maana ndio ingeonekana jinai....kwa mtazamo wangu naona sheria zina favour wenye kipato na c maskini

  kwa maana chenge ashahukumiwa...je hiyo sio jinai? na kakutwa na hatia!1 hakuna uhalali wowote ule wa kumusafisha chenge
  naomba kusaidiwa kwa hili
   
 8. Gama

  Gama JF-Expert Member

  #8
  Dec 31, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 9,224
  Likes Received: 1,411
  Trophy Points: 280
  sheria inapojadiriwa kwa ushabiki hainogi. Kwanza nijuavyo hakukutwa hatia ya jinai. Kwa hiyo sidhani kama ameondokewa na sifa za kuwa mbunge ama kugombea :.........................
   
Loading...