Sawa Bwana Chenge! umefanikiwa kutudandanya! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sawa Bwana Chenge! umefanikiwa kutudandanya!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kizito, Jan 1, 2011.

 1. K

  Kizito Member

  #1
  Jan 1, 2011
  Joined: Feb 23, 2008
  Messages: 70
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Sasa Bwana Chenge tunajua Mahakama imekusaidia sana kwa kuwa ilikutaka ulipe laki saba au uende ndani miaka mitatu nawe ukalipa laki saba kama vile mtu anavyolipa nauli ya Daladala.

  Lakini katika hukumu hiyo Sijui nani anapaswa kukata Rufaa. kwa kuwa sisi si wanasheria tunaiona hukumu ni ndogo ingekuwa angalau ukae Segerea miezi miwili ndo wakutoe na uwajibike kulipa faini kwani kulipa Faini hiyo uliolipa maana yake ni kuwa umeyakubali hayo makosa.

  Tumekuona Bwana Chenge ukitoka Mahakani ukicheka kana kwamba umefanya mambo mazuri hiyo haikuwa Nidhamu njema kwa jamii inakujua kuwa wewe unamakosa mengi kuliko hayo uliyohukumiwa kwayo.(angalau ungeonyesha uso wa huzuni kidogo hata kama moyonio ungekuwa umefurahi.

  Kitu kingine Bwana Chenge kuyakubali yale m,akosa inamaanisha kuwa wewe sio msafi (Umegushi Bima) unawezaje kuwaongoza wananchi wa jimbo lako? wakati umegushi hata Bima je matokeo ulishindwa kugushi?

  Chenge najua hapa Mahakamani umetushindwa lakini tutakushitaki kwa Mungu.
   
 2. m

  mzambia JF-Expert Member

  #2
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Jamani mmesahau ya ditopile tumwache huyu chenge
   
 3. m

  mzambia JF-Expert Member

  #3
  Jan 1, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Na mungu ndiye mpangaji wa kila kitu hakuna marefu yasiyo na ncha
   
 4. C

  Chagula Member

  #4
  Jan 1, 2011
  Joined: May 1, 2009
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  :embarrassed: Kuna baadhi ya watu wenye elimu ya juu Tanzania ambayo waliipata kutokana na wazee wao masikini kuwalipia wasome, pili kutokana na kukaa usiku kucha wakisoma na kukalili ili wafaulu mitihani. lakini wakisha faulu mitihani ya kukalili , wanasahau kabisa nani aliwapa uwezo wa kwenda chuo kikuu, wanasahau kabisa kwamba ni pesa za walipakodi wakiwemo wazazi wao ndizo zilitumika ili waweze kupata hiyo elimu. Matokeo yake ni kwamba wakisha faulu na kupewa hizo shahada, wanasahau kabisa walikotoka, badala yake wanatumia hiyo elimu kuwaghalibu waliowasomesha, wanatumia hiyo elimu kulidanganya taifa, wanatumia hiyo elimu kuliibia taifa na wananchi.

  Hii ni kweli ya huyu Chenge, amesahau kabisa nani alimpa hiyo elimu na ni pesa za nani zilitumika kumuelimisha, matokeo yake analaghai, analiibia taifa, anamtilia kinga mkewe baada ya kuwaua hawala zake na kudai eti ni yeye ndiye alisababisha ajali.

  Huyu Chenge pamoja na wasomi wengine wengi waliomo CCM, wametumia mbinu, wizi na jeuri wakashinda uchaguzi kwa kutumia karatasi za kura za bandia - kama zile ambazo Makamba na JK walipeleka Shinyanga na kudai itangazwe kuwa CCM ilishinda wakati hata wana CCM wa Shinyanga walijua wazi kuwa CHADEMA ilishinda.

  Nasikitika kusema kuwa sasa hivi Tanzania inaongozwa na wezi, wahuni, mafisadi na walaghai. Washukuru kuwa watanzania ni waoga na wapole, hawawezi kuchukua hatua kama za Kenya au Ivory Coast, wapowapo tu, wanalalamika na wakati viongozi wanaendelea kula nchi kwa mikataba yao mbalimbali ya wizi na ufisadi.

  Acha waendelee, iko siku hayo yote wayatendayo pamoja na wake za na watoto wao, yatawatokea puani siku moja. KUMBUKA: "MWOGA UKIMFUKUZA ATAKIMBIA, AKISIMAMA BASI UJUE KUNA MAWILI, KUFA AU KUPONA"
   
Loading...