Asali ya limao
Member
- Dec 27, 2018
- 60
- 105
SURA YA KWANZA
MLANGO WA TANO
MIAKA MITATU BAADAE
TSS HQ-DAR ES SALAAM
Nchi ilikuwa imetulia na kurejea katika hali yake ya utulivu kama ilivyokabidhiwa na waasisi wa taifa hili pindi walipoamua kung'atuka katika nafasi zao na kuwa kama wananchi wengine, watu walikuwa bize kuinua uchumi wao na nchi kwa ujumla, kwasababu amani na ulinzi vili tamalaki ijapokuwa ilikuwa imesalia miezi kadhaa kabla ya uchaguzi mkuu wa raisi, wabunge na madiwani, katika idara nyeti ya ujasasi kulikuwa na kikao kilichokuwa kinaendelea.
"jamani nimewaiteni hapa kuwaelezea mambo machache ijapokuwa kuna mengi tu tumekuwa tuki habarishana mara kwa mara ila siyo kwamba ndiyo iwe mazoea, ijapokuwa bahari imetulia haina maana ndiyo tujisahau na kukiachia chombo kielee maana hatujui ni muda gani na wimbi la namna gani litatuyumbisha, hasa ukiangalia mwakani mwezi wa kumi na mbili ni mwezi utakaofanyika uchaguzi mkuu niwaombe tu kama ni umakini uwe mara mbili ya vile tuliokuwa nao mwanzo" aliongea Chifu huku akiweka kituo na kupiga funda kubwa la maji kisha akawatazama watu waliokuwa mle ndani katika nyuso zao kisha akamgeukia jenerali na kisha akampa ishara atoe neno.
'kwanza nitoe pongezi kwako wewe mkurugenzi wa idara ya ujasusi. kwa maana bila mbinu zako nadhani hivi sasa tungekuwa tunaongelea mengine, nasema hivi nikiwa na uhakika kwamba mbali na kuwa ulinzi umeimarishwa kila mahali kiasi kwamba ukidondosha noti ya elfu kumi hata ukirudi kesho yake unaikuta kama ulivyoidondosha, kama nilivyosema mwanzo jicho letu halitasinzia kuhakikisha haturudi kule tulipokuwa" aliongea jenerali huku akiwatazama wajumbe walioko ndani ya chumba kile kisha akagandisha macho yake katika uso wa chifu aliyeishia kutabasamu na kukubaliana na kile kijana wake anacho kizungumzia.
"nashukuru kama na wenzangu kama mmeweza kuliona hilo nina imani kabisa sasa hivi tunaongea lugha moja na hakuna kati yetu atakayeleta uzembe katika upande wake, hatutakuwa na uvumilivu kwa kiongozi yeyote atakayeufanya usingizi wetu uwe kitendawili, baada ya kusema hivyo nadhani tungeendelea kutekeleza majukumu yetu ipasavyo ikiwa kama hakuna mwenye swali" kufikia hapo akaupisha ukimya uliomeza fikra za viongozi wale wa vyombo vya ulinzi na usalama,ndani ya dakika moja waliafikiana kikao kile kiishie pale na baada ya dakika mbili simu yake ilitekenya kwenye mifuko yake akaitoa na kuipokea.
"ubavu wa yule msaliti umeonekana mwanza, amekuwa mama ntilie mitaa ya kiwanda cha soda.......tunasubiri neno moja kutoka kwenye kinywa chako akapate malipo yake Butimba" ilizungumza sauti nzito huku ikisubiri kinywa cha mtu aliyekuwa upande wa pili.
"nalitambua hilo ila hatuna haraka naye, bado tunafatilia nyendo zake ili tuweze kupata samaki mkubwa huyu ni dagaa tu muda ukifika nitakupa maelekezo" alizungumza Chifu kwa utulivu
"sawa mkuu tunaendelea kuzitazama nyayo zake na ripoti itakufikia mezani mkuu kama ataonyesha mabadiliko yoyote hatutakuwa wavumilivu ila atakuja kuwatapika kwa lazima ni hayo tu" ilisema sauti ya upande wa pili
"lets wait and see, ila hakikisha unapozichunguza nyayo zake hakikisha hatambui, unajua upo kimkakati na utambue unazifata nyayo za jasusi aliyebobea, be carefully ofisa.....titititi" simu ilikatwa na kumfanya mtu yule ashushe pumzi nyingi, na kunyoosha mikono yake juu ya meza kubwa ya ofisi na ya kisasa.
POLICE CENTRAL-DAR ES SALAAM
saa 8:15 mchana.
"ndugu waandishi wa habari, tumewaalika leo, kuapa taarifa mbalimbali zinazohusu hali ya usalama wa raia na mali zao vile vile hatua madhubuti tutakazo chukua na zilizochukuliwa, jeshi la polisi kanda maalum ya dar es salaam kwa takribani mwezi mmoja uliopita tuliendesha oparesheni ya kuwabaini, kuwatia nguvuni, kuwahoji na kuwafikisha katika vyombo vya sheria wahalifu hao, nipende kusema hadi hii leo tumefanikiwa kuwakamata wahalifu wapatao kumi na saba(17) na muda wowote watafikishwa mahakamani." alimeza kamanda wa polisi kanda maalum ya Dar es salaam Chacha Msamalo kimincha.
"hilo ni moja mbili, ndugu waandishi wa habari na wananchi wa Dar es salaam kwa takribani wiki mbili zilizopita tulikuwa tukisumbuliwa na wimbi la uporaji mali kwa kutumia silaha na mauaji, huku lawama kubwa tukielekezewa sisi kwenye mitandao mbali mbali ya kijamii kwa ukubwa wa jambo hili, jeshi la polisi kanda maalum ya Dar es salaam kwa kushirikiana na vyombo vingine vya dola tuliweza kuwakamata watu wanane, tumewafanyia mahojiano ya kina na waliwataja watu wawili kama viongozi wao wanaowafadhili kiuchumi na silaha za kufanyia uhalifu kuwa ni SAIDI BANDIKA,mfanyabiashara na mmiliki wa timu ya mpira wa miguu iitwayo Sungura na ndugu Elvyn byashalila, mbunge wa afrika mashariki na mwenyekiti wa makampuni ya Embetogwa yanayojishulisha na utengenezaji wa bidhaa mbalimbali."
"watuhumiwa hao kwa nyakati tofauti tofauti kuanzia sasa watafikishwa katika vyombo vya sheria vile vile nitoe rai kwa wananchi wote kwa ujumla kuweza kushirikiana na jeshi la polisi katika kufichua na kupambana na uhalifu bila kuoneana aibu, na pia nitoe onyo kwa wote wanaojishughulisha na uhalifu kuwa tutakabiliana nao na watapata wakati mgumu sana, Asanteni kwa kunisikiliza" alimalizia taarifa yake kamanda yule wa polisi, mweusi na mkakamavu mwenye macho makali na sauti nzito.
taarifa ile ya kamanda wa polisi ilizua gumzo katika mitandao ya kijamii huku kila mtu akifatilia picha mjongeo zilizokuwa zikiwaonesha wahalifu wale waliotajwa wakiwa katika ulinzi mkali ikiwa ni pamoja na miongponi mwao kufikishwa mahakamani siku hiyo kujibu tuhuma mbali mbali zinazowakabili.
MWANZA
IGOMA STREET
"oyaaa sista weka kama jana ila maharage usiweke kabisa, zingatia ujazo wa nyama na mchuzi uwiane" aliongea kijana mmoja aliyekuwa amechafuka mavazi yake kwa oili na grisi kiasi cha kumfanya ajulikane kiwepesi kama fundi gereji.
"hizo nyama kuwiana na mchuzi buchani wanalitambua hilo, nyama ni mbili hutaki katafte watakaokuwekea utakavyo" alijibu mdada yule aliyekuwa ndani ya vazi la ushungi na dera na punde akaingia kijana mwingine mwenye mwili wa kawaida na kisha kuagiza ugali kwa dagaa wa kukaangwa, baada ya mtu wa kwanza kumaliza kula, kulipia nakutoweka mghahawani pale mwanamke yule alijisogeza mezani pale huku akiwa na shauku ya kujua kimemleta nini kijana yule ambaye dhahiri shairi ilionesha wanajuana
"Bosco umefata nini huku" alianza mwanamke yule kwa udadisi
"nimetumwa na mkuu kukuuliza umefikia wapi kwenye ule mpango" alikoroma mtu yule huku akiendelea kusukumia matonge ya ugali mdomoni
"bosco nisiwe muongo hii nchi kwasasa wame activate usalama masaa ishirini na nne, hatua pekee niliyopiga ni ya ukusanyaji wa habari ambayo imepelekea hatua ya utekelezaji kusuasu.......alikatishwa kwa ishara na kijana yule.
"ule mpango umeshahairishwa kwasasa, mpango utakaouona kwenye emaili yako ndiyo wenyewe na unatakiwa kukamilika ndami ya siku tatu mbele, nadhani tumeelewana tutaonana Goma nkutakie kazi njema." aliunguruma tena kijana yule
"sawa nitatekeleza kwa weledi mtoe wasiwasi mkuu" aliongea mwanamke yule kwa sauti ya polepole ambayo hata ukiwa mita mbili huwezi kusikia kunachozungumzwa ila si masikio ya kachero mbobevu Leyla Shigembe kutoka idara ya ujasusi ya jeshi aliyekuwa akijifanya ni mhudumu katika hoteli hiyo natangu mwanzo wa mazungumzo alijifanya yuko bize kuosha vyombo jikoni, vifaa alivyovitega kwa siri vilinasa mazungumzo yale ambayo yalitumwa kwenye ofisi fulani ya siri ndani ya makao makuu ya jeshi.
"watch every steps you hit Diane, mkuu anakusubiri kwa hamu kubwa wewe na kazi yako" alimaliza kusema kijana yule na kupotea eneo hilo kama upepo kuondoka kwake kukamfanya mwanamke huyu kufunga mghahawa wake mapema huku akimdanganya mhudumu yule kuwa amepata taarifa mbaya kuwa dada yake amepata ajari na amekimbizwa hospitali ya mkoa.
"sawa dada uranijulisha kunavokwenda" rafudhi ya kisukuma ilimtoka kachero yule
"mxiuew kama mwema vile kumbe jasusi mkubwa, alinichukulia mimi boya basi wakubwa zake wataitoa taarifa za msiba wako na utabaki na siri yako kaburini mbwa mweusi wewe" alijisemea kimoyomoyo Diane huku akimalizia kufunga virago vyake kabla ya kupotea eneo lile.
MSASANI-DAR ES SALAAM
Saa 12:45 jioni
ndani ya jumba moja kifahari na lenye mandhari mazuri, ghorofa moja ilitosha kuifanya iwe moja ya nyumba kali ndani ya mtaa ule, ndani ya jumba hili kulikuwa na kikao kizito kilichowahusisha wanandoa wawili, vijana wa makamo waliokuwa na miaka takribani miwili tangu wafurahie fungate lao, hawa hawakuwa wengine bali ni Kanali Charz na mkurugenzi msaidizi wa idara ya ulinzi wa raisi ndani ya idara ya ujasusi katika taifa hili.
"nataka uniambie kila kitu na usinifiche hata nukta kama unapenda nyumba hii iendelee kuwa na amani Charz" aliongea kwa utulivu na kumuangalia mmewe aliyekuwa amekalia sofa la mtu mmojja huku akionekana dakika kadhaa nyuma alikuwa amezama katika dimbwi la mawazo, kabla hajamaliza kuchakata sentensi ile alipigwa swali jingine lililomsisimua sana
"tangu umesoma kikaratasi kule kisiwani hujawahi kuwa kanali Charz niliyekuwa namuona kila uchwao kwa miezi kadhaa na hali hiyo imejitokeza baada ya kupapasa koti lako, kikaratasi kile hujataka kunishirikisha ujumbe uliomo ndani ulikuwa unahusu nini?mbali ya kuwa mimi na wewe ni mwili mmoja kiimani ila mwenzangu ukute hujamalizana kidemu chako, tusikilizane kama unaona kwamba kukaa kimya mi suluhisho ni heri tukaachana tu kila mtu akae na siri zake nimechoka mimi." alimaliza na sauti iliyoambatana na kama sauti ya kilio.
"natambua yote unayozungumza ni haki yako na uko sahihi.naomba nikwambie hili suala limetokea wakati na muda ambao mimi na wewe hatujawa kama sasa,sitaki jambo hili liwaingize kwenye picha watu wasiohusika na..........."Itaendelea.