Sauti ya Askofu Severine Niwemugizi

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,789
288,013
SAUTI YA ASKOFU SEVERINE NIWEMUGIZI WA KANISA KATOLIKI TANZANIA

Mhashamu Baba Askofu Severine Niwemugizi wa Kanisa Katoliki Jimbo la Rulenge - Ngara ni miongoni mwa Maaskofu wanaopaza sauti katika kutetea haki katika jamii. Tarehe 15 Desemba 2020 ametoa tafakuri kuhusiana na masuala ya haki. Nimeamua kuuchapisha ujumbe wake katika ukurasa wangu kwa faida ya wengi. Endelea kuusoma na kuutafakari!

Mwana Kondoo Ameshinda! Tumfuate!

Askofu Emmaus Bandekile Mwamakula - Kanisa la Moravian la Uamsho Tanzania & Afrika Mashariki.

"Fumbua kinywa chako kwa ajili yake aliye bubu, uwatetee watu wote walioachwa peke yao. Fumbua kinywa chako, uhukumu kwa haki, uwapatie maskini na wahitaji haki yao” (Mith 31:8-9).

Ee Bwana, si kila mtu anaweza kufanya kazi ya kinabii. Kazi ya kinabii inatisha kwa sababu ya gharama yake. Gharama yaweza kuwa kifo, kupoteza kazi, kupoteza marafiki, nk. Kwa kujua gharama hiyo Yeremia alipoambiwa na Mungu amewekwa kuwa nabii wa mataifa alitafuta visingizio ili asipewe jukumu hilo. Alijitetea kuwa yeye hawezi kusema kwa sababu bado ni mtoto. Alisema hivyo kwa sababu ya woga wa kile kiwezacho kumpata kwa kutekeleza jukumu la kinabii. Mungu alimtoa woga akimwambia haendi kusema maneno yake bali yale atakayomwamuru.


Nabii anatumwa na Mungu, wala hajiteui na kujitambua mtu kuwa nabii. Ni Mungu anateua na kutuma manabii juu ya mataifa na falme ili “kung’oa, na kubomoa, na kuharibu, na kuangamiza, ili kujenga na kupanda” (Yer 1:10).

Mazingira ya utume wa nabii yanaweza kutisha, yasiwe rafiki. Lakini kwa Mungu siyo hoja. Wapo wengi dunia hii wanahitaji kusemewa na manabii. Tujalie neema yako Bwana itupe ujasiri wa kupokea jukumu la kuwatetea wasioweza kujitetea, kuwa midomo ya wasioweza kusema. Amina."
 
Hawa maaskofu japo wako wachache lakini sauti zao zinawafikia wengi zaidi ya wale wasifiaji ambao wameshachosha masikio ya wasikilizaji.

Mungu awabariki sana na wasichoke kuendelea kukemea maovu, kazi ya unabii ni ngumu, hata mitume kina Petro walilipwa mauti kwa kazi yao.

#msiogope.
 
Huyo hana tofauti na Bagonza!

Walisimama upande wa shetani kipindi cha corona kwa kufunga makanisa
 
Back
Top Bottom