SAUT mnakwama wapi?

Kinkunti El Perdedo

JF-Expert Member
Nov 28, 2020
4,475
11,019
Hili suala la matokeo ya wanafunzi limekuwa kero kubwa sana kwa wanafunzi, yaani si ajabu chuo kupanga ratiba ya sup uku wanafunzi hawajui matokeo yao kupitia SAUT-OSIM.

Wanafunzi katika kozi mbalimbali inafika kipindi wanaingia semester ya pili ya masomo uku hana matokeo ya semester ya kwanza,wakiingia kwenye OSIM kuangalia ni incomplete, sup ambazo hazina kichwa wala miguu na carry za ajabu ajabu hata course work results hakuna. Ma-lecturer nao lawama kwa wanafunzi kuwa hawaonekani kwenye system hivyo yeye haimuhusu ni juu ya mwanafunzi kufuatilia kwa IT, huyu nae IT anafanya kazi kama hisani wakati ni wajibu wake anapanga muda wa kuwahudumia wanafunzi vile anavyo taka yeye bila kujali ratiba zao za vipindi ikitolewa quiz au test basi imekula kwa mwanafunzi lecturer haelewi kitu.

Na kwanini taarifa za wanafunzi zinakuwa zinachanganya sana yaani kwamfano mwanafunzi anasoma BAMC one ,stream one au stream two lakini unakuta aliye stream two jina liko stream one aliye stream one jina liko stream two.

Lakini kwenye penati za wanafunzi walio chelewa kulipa ada na michango mingine ya chuo wako makini kweli kweli hakuna kinacho haribika ila matokeo ya wanafunzi na taarifa zao ndo zinabadilika badilika kila wakati, matokeo leo yapo kesho hayapo,mnawachosha wanafunzi kufuatilia kila mara matokeo yao na kuacha vipindi vikiendelea boresheni mifumo yenu kama ilivyo bora kwenye mifumo ya kifedha. Kilichotokea kwa wanafunzi wa PR sote tunakijua licha kwamba mlifanya nao kikao cha hovyo kabisa na tuko makini kufuatilia hatua kwa hatua mpaka kujua mwisho wake.

"Taswira halisi ya taifa hujengwa na wenye taifa lao"

IMG_20200618_090541_8.jpeg
 
Kuna rafiki yangu wa SAUT Mwanza naye analalamika hili suala. Wajirekebishe.
 
Back
Top Bottom