kimsboy
JF-Expert Member
- Oct 17, 2016
- 8,992
- 17,892
Saudia yanunua mfumo wa makombora kutoka Israel
Saudi Arabia imeripotiwa kununua mfumo wa ngao ya makombora kutoka utawala wa Kizayuni wa Israel, katika hali ambayo ripoti zinasema tawala mbili hizo zipo mbioni kuweka wazi na kuimarisha uhusiano wao.
Duru za ngazi za juu za kidiplomasia zimeiambia tovuti ya habari ya Imarati ya Khaleejonline kwamba, utawala wa Aal-Saud umefanikiwa kununua mfumo huo wa ngao ya makombora kutoka Tel Aviv kutokana na upatanishi wa Marekani.
Awali utawala wa Kizayuni wa Israel ulikuwa umekataa kuuuzia utawala wa Riyadh mfumo huo wa makombora ukidai kuwa hauwezi kufunga mkataba wowote wa mauzo ya silaha na nchi za Kiarabu eti kwa kuwa huko ni kuhatarisha maslahi yake katika eneo.
Inaarifiwa kuwa, makubaliano hayo ya mauzo ya mfumo huo wa makombora wenye kugharimu makumi ya mamilioni ya dola yataanza kutekelezwa mwezi Disemba, baada ya Saudia kukamilisha malipo
Vyanzo vya habari vimedokeza kwamba, Saudia imenunua mfumo huo kwa shabaha ya kujikinga na makombora ya balestiki yanayovurumishwa kila uchao na wanaharakati wa Ansarullah wa Yemen.
Mwaka uliopita, gazeti moja la Kizayuni lilifichua kuwa, katika mkataba wa mabilioni ya dola wa ununuzi silaha baina ya Marekani na Saudia, baadhi ya mashirika ya uundaji silaha ya Israel yalianishwa kuwa yangestafidi na makubaliano hayo.