Saudia yaifungia Al Jazeera ya Qatar

Serikali ya Saudia imesimamisha urushaji matangazo na kufunga ofisi za kanali ya televishani ya al-Jazira inayomilikiwa na Qatar nchini humo.

Taarifa iliyotangazwa leo na viongozi wa Saudia imewataka wafanyakazi wote na waandishi wa habari wa kanali hiyo ya Qatar wenye uraia wa Saudia ambao wanaishi nje ya nchi, kurejea nyumbani haraka iwezekanavyo.

Kufuatia hali hiyo, serikali ya Qatar nayo imejibu mapigo kwa kusimamisha safari za Shirika la Ndege la Qatar Airways kwenda nchini Saudia, sambamba na kuwataka raia wanaoishi nchini Saudia kurejea nchini.

Kadhalika Wizara ya Mambo ya Nje ya Qatar imetangaza kuwa, uamuzi wa Saudia, Imarat, Bahrain, Misri na Libya wa kukata mahusiano na Doha, kamwe hautoathiri kwa namna yoyote maisha ya kawaida ya raia wake au watu wanaoishi ndani ya ardhi hiyo (Qatar.)

Kauli hiyo imetolewa kufuatia uamuzi wa nchi hizo za Kiarabu kutangaza mapema leo kukata mahusiano yao na Qatar ambapo serikali ya Doha imesema kuwa, uamuzi huo umechukuliwa kwa pupa na kwamba madai yaliyochukuliwa na Saudia dhidi yake hayana msingi wowote.

Source: Parstoday.sw
Qatar lazima watakuwa wadogo.
 
Hi
Hapana, aljazeera ndio inaumia kukosa coverage ya Saudia maana yake yameshuka kwenye ukubwa wa masafa na kuna matangazo watayakosa kutoka Saudia, commercials.
hilo pia lipo , lakini wa wananchi wa saudi pia wanakosa habari
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Hizi nchi bwana zinachekesha,nadhani Qatar akichukua hatua wataumia zaidi wengine, hapo ataebaki salama ni Emirate tu lakini nchi zingine zinaihitaji sana Qatar, ikiwa doha wakiamua kuwatimua raia wote wa Egypt, Bahrain,Yemen, saudia na uae, nani ataathirika? Egypt, Yemen, na Bahrain wataumia zaidi kwa sababu Qatar hahitaji chochote toka nchi hizo zaidi ya nchi hizo kujaza wafanyakazi Qatar, wanapotaka Qatar akate uhusiano wake na Iran, wakati Iran ndio anailisha Qatar, nasikia fly dubai,etihad,na fly emirate wanakata safari za doha, Qatar air wana ndege zaidi ya 300 hawana wasiwasi tena wataongeza route zaidi duniani na hayo makampuni ndio yatapungukiwa safari, hii vita sioni dalili ya doha kusalimu amri
 
Wanachezeshwa hawajielewi au wanaelewa sema hamna namna washasetiwa tayari angalia wanavyokwaruzana wao kwa wao.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Mr Hero Hiyo comment yako hapo juu usije uka i edit.... Hawa Qatar mda si mrefu watasalimu amri.... Qatar naitengemea 40% ya chakula kutoka Saudia Arabia.... Saudia amesha funga mpaka wake hamna tena kupitisha chakula kueleke Qatar.... Baadhi ya Mashirika ya ndege yamesha wapiga ban hatatumia tena viwanja vyao.... Wasaudia, wenye maduka makubwa hapo qatar wamesha anza kuyafunga wanaondoka.... Hapo raia wa Qatar watengemee mfumoko wa bei.... Hali hiyo raia watataka wa badilishiwe uongozi hapo ndiyo itakuwa mwisho wa Qatar...

Bei ya chakula qatar ni ghali raia wanapanda ndege hadi saudia ambako bei ya vitu vipo bei rahisi...Syria ya pili hiyo inakuja...
 
Tatizo ni ukoo wa kifalme saudi arabia. Huu ukoo pesa yao ni ndefu wakitaka wanaweza kulifanya bunge letu lipitishe sheria ya wanaume wote Tanzania kufuga midevu
mchague na maneno ya kuropoka!...sio wote kina mudy Tz
 
Back
Top Bottom