kisasangwe
JF-Expert Member
- Feb 16, 2010
- 292
- 52
Sikiliza nikwambie!.Hakuna sheria na agizo la kiislamu linalopitwa na wakati na wala hakuna iliyoanza mwaka 47 na 1970.Maagizo yanayoanzia kwa Allah s.w hayana mwanzo wala ukomo.
Nyinyi kwenye forums na magazeti munaong'ang'ania Saudia iachie uendeshaji wa gari huru kwa wanawake wala hamuelewi lengo kuu na hao walioanzisha ajenda hii.Wanawake na wanaume wa Saudia na kote kwengine wala hawana akili ya kupinga hekima ya Muumba wao.
Kwa kifupi nitoe fununu la kile ninachojua mimi mwenyewe.Katika Uislamu kuna kitu kinaitwa sitara ya mwanamke.Hii sitara ni mada pana sana wahadhiri wa kiislamu wanaweza wakatoa darsa mpaka ukasinzia bila kfikia mwisho.Katika sitara gari inaweza ikawa kitu kimojawapo kinachoondoa hiyo sitara.Inapoondoka kunapatikana kitu kinaitwa fitna na hii ikija nchi na dunia haikalilki.Waislamu kwa wakristo huonja chungu yake.
Wanaopinga uislamu hupendelea kuanza na kuleta fitna kwanza kabla kutumia makombora ya kutoka angani ili kurahisisha kazi.Katika uislamu wanawake ni watu muhimu sana na msingi kila jambo.Hivyo ukiweza kuwavuruga wao kwanza utakuwa umewaweza wanaume wao wa kiislamu.
Ukiwa na muda kidogo jisomee tafsiri ya Qur'an surat Ahzaab:59 na Surat Nnuur aya za 30 na 31.Vile vile jisomee mada ya Hijabu.
Wasomi wa kiislamu wa Saudia ndio wanaoelewa hayo.Wafalme na ndugu zao wanaweza wakajaribu kuridhia matakwa ya maadui lakini bado watakuwa hawajaufaa ulimwengu kwani fitna ikija itatukumba sote waislamu kwa wakristo.Mfano wa fitna inavyoenea angalia mizozo ya Libya na Iraq.
mhhhhh hapo hapo kwenye red sasa. umuhimu wao huwa kwa kina nani hasa?
napita tu