Saudi Arabia seeks death penalty in Khashoggi murder case

Saudi Arabia seeks death penalty in Khashoggi murder case

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,377
Mwendesha Mashtaka anataka adhabu hiyo itolewe kwa Washtakiwa 5 kati ya 11 waliohusika na mauaji ya Mwandishi wa habari, Jamal Khashoggi

Mwendesha Mashtaka Msaidizi, Shalaan al-Shalaan amesema Khashoggi aliuawa katika ubalozi wa Saudi Arabia nchini Uturuki Oktoba 2 baada ya kuchomwa sindano ya sumu

Mwili wake ulikatwa katwa na kutolewa nje ya ubalozi huo ambapo mtu mmoja ambaye hajafahamika alikabidhiwa lakini hadi sasa haijafahamika ulipo mwili huo

Amesema Mwandishi huyo aliuawa baada ya majadiliano kuhusu kurudi kwake Saudia kushindikana na amri ya mauaji ilitolewa na aliyekuwa akiongoza majadiliano

Aliongeza kuwa Kiongozi huyo majadiliano ndiye aliyetumwa kumrudisha Khashoggi nyumbani na amri ya kumrudisha ilitoka kwa Mkurugenzi wa zamani wa Intelijensia, Ahmed al-Asiri

Aidha, ameeleza kuwa hana ufahamu wowote kama Mtoto wa Kifalme anayeongoza taifa hilo, Mohammed bin Salman alihusika
====

Saudi Arabia’s public prosecutor is seeking the death penalty for five out of 11 suspects charged in the murder of journalist Jamal Khashoggi, his office said on Thursday, as the kingdom tries to overcome its biggest political crisis in a generation.

Khashoggi, a royal insider turned critic of Saudi policy, was killed in the country’s Istanbul consulate on Oct. 2, after a struggle, by a lethal injection dose, deputy public prosecutor and spokesman Shalaan al-Shalaan told reporters.

His body was dismembered, removed from the building and handed over to a “local cooperator”, whose identity has not been confirmed, he added. The whereabouts of Khashoggi’s remains are unknown.

Shalaan said the Washington Post columnist was murdered after “negotiations” for his return to the kingdom failed and that the killing was ordered by the head of a negotiating team sent to repatriate Khashoggi after he decided it was unfeasible to remove him from the consulate.

Shalaan said the order to repatriate Khashoggi had come from former deputy intelligence chief General Ahmed al-Asiri, who was sacked last month following an initial investigation.

Asked if Saudi Crown Prince Mohammed bin Salman played a role in the murder, he said: “He did not have any knowledge.”

Turkish President Tayyip Erdogan has said the order for the operation came from the highest level of Saudi leadership but probably not King Salman, putting the spotlight instead on his 33-year-old heir Prince Mohammed.

U.S. President Donald Trump has suggested ultimate responsibility lies with the prince as de facto ruler.

Riyadh initially denied any knowledge of Khashoggi’s disappearance, then offered contradictory explanations including that he was killed in a rogue operation. The case has sparked a global outcry, opened the kingdom to possible sanctions and tarnished the image of Prince Mohammed.

Some details provided on Thursday again contradicted previous versions, none of which mentioned a drug-induced death and one of which called the killing premeditated based on information provided by Turkish authorities.
 
Mtoyo:Nataka niwe usalama wa taifa...


Baba:Mwanangu fikiri kabla ya kuchagua kazi
 

Ofisi ya Mwendesha Mashtaka Mkuu nchini Saudi Arabia imemaliza uchunguzi wake juu ya nani aliyeamuru kuuawa kwa mwanahabari Jamal Khashoggi na kufikia kikomo kuwa haikuwa Mwanamfalme Mohammed bin Salman.

Uchunguzi huo umebaini kuwa mauaji hayo yaliamuriwa na afisa mwandawizi wa idara ya usalama wa taifa ya Saudia ambaye alipewa kazi ya kumshawishi Khashoggi kurejea Saudia. Mwanahabari huyo ambaye alikuwa kinara wa kumkosoa Bin Salman alikimbia Saudia mwaka 2017 na kuhamia Marekani.

Kwa mujibu wa msemaji wa ofisi hiyo, Khashoggi alidungwa sindano ya sumu baada ya purukushani kuibuka ndani ya ofisi ndogo za ubalozi wa nchi hiyo jijini Istanbul, Oktoba 2, 2018.

Watu 11 tayari wameshafunguliwa mashtaka kutokana na mkasa huo na waendesha mashtaka wanataka watano kati yao kupatiwa adhabu ya kifo. Uchunguzi unaendelea kwa watu wengine 10 ambao wanshukiwa kushiriki mauaji hayo.

Katika mkutano na waandishi wa habari, Naibu Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Saudia Shalaan bin Rajih Shalaan amesema mwili wa Khashoggi ulikatwa katwa ndani ya ubalozi baada ya kuuawa.

Vipande hivyo vya mwili vilikabidhiwa kwa mshirika wao ambaye ni raia wa Uturuki nje ya ubalozi. Tayari picha ya kuchora ya mshirika huyo imetolewa na uchunguzi unaendelea kujua vipande hivyo vya mwili vilipelekwa wapi.

Bwana Shalaan hata hivyo hakuwataja wale ambao wamefunguliwa mashtaka juu ya tukio hilo.


"Uchunguzi wetu umebaini kuwa aliyeamuru mauaji ni kiongozi wa timu ya ushawishi aliyetumwa Istanbul na Naibu Mkurugenzi wa Usalama Generali Ahmed al-Assiri kumtaka Khashoggi kurudi nyumbani," amesema Shalaan.

"Mwanamfalme bin Salman hakuwa na taarifa yeyote ya kilichokuwa kinaendelea," alisisitiza.

Mwanamfalme Mohammed, ambaye ni mtoto wa Mfalme Salman ndiye anayetawala nchi ya Saudia kutokana na baba yake kuwa mgonjwa amejitetea kuwa hakushiriki kwa namna yeyote ile. Na pia amesema mauaji hayo ni "kosa kubwa la jinai ambalo halina utetezi".

Wakosoaji wake hata hivyo wanasema kuwa uwezekano ni mdogo sana kuwa hakuwa na taarifa juu ya operesheni hiyo.

Watu 21 waliokamatwa kutokana na tukio hilo wamekuwa wakionekana katika shughuli mbali mbali za kiusalama za Saudia. General Assiri na kigogo mwengine Saud al-Qahtani wamefutwa kazi kutokana na tukio hilo.

Shalaan amesema Qahtani amezuiwa kutoka nje ya Saudia na anaendelea kuchunguzwa. Hata hivyo hakusema chochote kuhusu Generali Assiri.Rais wa Uturuki, Recep Tayyip Erdogan amesema "amri ya kumuua Khashoggi imetoka kwenye mamlaka za juu kabisa za serikali ya Saudia" lakini haamini kuwa ilitolewa na Mfalme Salman.Waziri wa Mambo ya Nje wa Uturuki Mevlut Cavusoglu hata hivyo amesema baadhi ya kauli za Shalaan haziridhishi.

"Wanasema mtu huyu aliuawa sababu alipambana, lakini mauaji hayo yalipangwa kabla," aliwaambia waandishi. "Tena,wanasema mwili wake ulikatwa katwa...lakini hili si jambo la kukurupuka. Vifaa vya kutekeleza hilo na watu wa kulifanya waliingizwa nchini na baadaye kutekeleza."Maafisa wa Uturuki awali walisema kuwa mmoja wa maafisa usalama 15 wa Saudia walioingia Uturuki kumuua Khashoggi alikuwemo mtaalamu wa kuchunguza sababu ya vifo ambaye aliingia nchini humo na msumeno."Wale ambao walitoa amri na kuchochea watajwe na mchakato huu usizibwe," amesema Cavusoglu na kuongeza kuwa Uturuki "itatoa mwangaza wa mauaji haya katika hatua zote."


BBC
 
Watu walivo wanafiki hawakawii kusema kua adhabu ya kifo iko kinyume na haki za binadam
 
Chief prosecutor anajaribu kuficha majambo katika hili, waonyeshe hivyo vipande vya mwili vilipo pia ubalozi mzima ukamatwe na kushitakiwa haiwezekani mtu auwawe ndani ya ubalozi tena wa nchi yake bila wao kufahamu lolote.
 
Back
Top Bottom