Inakuwaje leo nyimbo zote ambazo zinaujumbe wa kulenga kuijenga jamii wasanii wake hawapewi air time badala yake nyimbo ambazo majina yake hayana hata maana ndizo zinapigwa masaa 24
Umegundua kuwa ili huyu mfalme wa giza afanikiwe anatafanya juu chini kuharibu familia.........na kama alivyofanikiwa kwenye bustani ya edeni kwa kumtumia mwanamke.......ndivyo anavyoanza tena na hapa dunia ya leo kumtumia mwanamke kudhoofisha kanisa.......unataka kujua anafanyaje......nitakwambia
Jamii ya kisasa inaishi maisha rasmi ambayo yanaendeshwa kwa kutumia pesa.........pesa ndio tiketi ya kupata mahitaji yetu wanadamu........hivyo ili kuzipata inabidi kuhangaika kuzipata.........katika kuhangaika huku ndipo watu hupoteza dira ya familia........kwa kutumia muda mwingi kutafuta pesa......na kuacha familia mbali
Ugumu wa kupata pesa umepelekea wanaume kuhisi kuzidiwa majukumu na hivyo kuwafanya na wanawake pia kusaidia kutafuta pesa.........hivyo kanisa linazidi kudhoofishwa kwa kuwafanya viongozi wa kanisa wasiwe na muda wa kulijenga bali kulidhoofisha kanisa.......
Leo hii wanawake hawambiliki katika kutafuta pesa.......hadi wamefikia hatua hawahitaji tena msaada wa mwanaume..........ni kweli kuna sababu zinapelekea wanawake wasiwe na haja ya wanaume......lakini jambo la kufahamu hapa ni kuwa wapo ambao hawahitaji kwakuwa ni wahanga wa manyanyaso mbali mbali ambayo kiukweli wanayohaki ya kutohitaji mahusiano tena......ila nazungumzia hawa wa kucopy na kupest experience za watu na kuhisi nao ni wahanga watarajiwa.........utawajua kwa kupata watoto wasio na baba.......kuropoka kauli hasi kama "wanaume hakuna siku hizi","Single mothers ndio mpango wa mjini"...na nyinginezo zenye kuashiria kuwa hawana hajaau hawaoni umuhimu wa kuanzisha familia ya baba mama na watoto.......
Kama vile alivyomnyatia eva pale bustani ya eden na kumshawishi kufanya uasi na MUNGU ........ndivyo navyomtumia tena leo hii mwanamke vile vile kuharibu familia ili apate kizazi kisicho na muelekeo ambacho hakitakuwa tayari kumtii MUNGU ila ambacho kitafuata mkumbo katika kushabikia uasi dhidi ya MUNGU..........
Leo wanawake wanaona si sawa kwa wao kulea familia hilo ni jukumu la msaidizi wa ndani......wao wakatafute pesa........hiyo ni ibada......siwalaumu la hasha.......binadamu tumewekewa mtego mkubwa sana hapa na kuushtukia ni kazi........huu mfumo wa maisha umetufanya kuwa watumwa wabkutafuta pesa bila shurti ila kwa lazima.......ndio maana nikasema tutafakari kwanza..........
Familia zinazorota kwasababu walezi au viongozi wake hawapo tena kwenye viti vyao wapo busy kutafuta pesa na katu hawawezi kuacha maana wametegeshewa na huyu mfalme wa giza ambaye ametumia kwa makusudi mfumo wa uchumi kukandamiza ustawi wa familia na jamii kwa ujumla......
Mfumo wa maisha ya kisasa unawafanya wanaume wajione si wanaume mbele ya wake zao.......hivyo kuachia majukumu wanawake.......wanawake kwa kizidiwa majukumu na kuamua kujitafutia hawaoni umuhimu wa mwanaume katika uhusiano.........hii si ajabu imeleta kizazicha wanaume ambacho kimeona wanawake ni chombo cha starehe tu......na wengine kuona wanawake ni wasumbufu bora tu wayamalize wao kwa wao kupitia mahusiano ya jinsia moja..........
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.