Yakini
Member
- Nov 20, 2012
- 75
- 19
Tunajua kila mtu anauhuru wa maoni, na ndivyo ilivyo katika jambo lililotokea ndani ya chadema. Ni wito wangu kwa wadau wote kuendeleza mijadala inayobeba mashiko ya nchi yetu kwa sasa. Nchi yetu inaelekea katika wakati muhimu sana katika kukamilisha mchakato wa Kutengeneza katiba mpya, tunahitaji kujikita katika hilo pamoja na mambo mengine yenye maslahi kwa umma. Nchi yetu ipo katika hali tete ukizingatia rasilimali za nchi yetu zinatumika vibaya na watanzania wanakumbwa na wingu kubwa la umaskini. Sioni kama ni busara kuendeleza mijadala hii na kusahau mambo muhimu yanayoendelea nchini mwetu.