Hii ni hoja iliyoibuliwa na baadhi ya vijana niliokutana nao tena kwa mara nyingine jana jioni hapa mtaani.
Kutokana na uhalisia kwamba wanaume na wanawake wengi wenye umri kuanzia miaka 30 na kuendelea wamekwisha kuzaa watoto kabla ya ndoa, katika mahojiano na vijana kadhaa hapa mtaani jana jioni, wengi ambao hiyo hali imewakumba, wameonyesha nia ya kuoa wanawake tasa au kuolewa na wanaume tasa.
Wamedai kufanya hivyo itasaidia sana kupunguza mikwaruzano na ugomvi katika familia, kwani mama au baba tasa atawaheshimu na kuwathamini watoto hao, kwa sababu watakuwa ndio watoto pekee katika familia. Pia wazazi wengine waliozaa na wale waliooana watapata imani kwamba watoto wao wanalelewa na kutunzwa vema, kutokana na kutokuwepo kwa uhasama na uadui dhidi ya watoto hao ambao ungeweza kusababishwa na watoto watakaozaliwa baada ya ndoa.
Mnalionaje hili wadau?
Jamani someni vizuri basi muelewe nilichoandika - ina maana nyie katika mazoezi, majaribia na mitihani swali la "comprehension" shule ya msingi mlikuwa hamfanyi au hilo swali lilikuwa optional?