Sasa wameshona vitenge vinavyofanana, wanazidi kunichanganya

Sasa wameshona vitenge vinavyofanana, wanazidi kunichanganya

JembePoli

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Posts
1,324
Reaction score
1,000
Juzi nilikuja na bandiko langu la wachumba zangu wawili ambalo mode wamelibadili na linasomeka (nimuoe yupi anaenipenda au ninaempenda)

Samahani sikuwasalimu hamjambo wote..! Mniwie radhi.

Nashukuru kwa ushauri wenu kwani nimeanza kuufanyia kazi lakini wakati mchakato wa kubaki na mmoja ili hatimaye ni Pause kuna kitu nimekigundua, jana wakati natoka mzigoni mchumba wangu wa kwanza alinitaka nimpitie ninapotoka kazini na wakati asubuhi ninapokwenda kazini ni kawaida huwa nampitia mchumba wangu wa pili na namuacha kazini kwake mimi naendelea (jiografia ya tunapokaa ni raisi kupitiana).

Lakini kilichonishangaza huyu wa pili sio kawaida yake kuvaa nguo za vitenge vilivyoshonwa (nilimsifia tu kuwa alipendeza, na alipendeza kweli) lakini nilikuja kuchoka zaidi pale nilipotoka job na kwenda kumpitia mchumba wangu wa kwanza kuona nae kavaa nguo za vitenge (huyu ni kawaida yake) kinachonishangaza ni kufanana kwa kitenge chenyewe walichoshona na mshono pia unaweza sema ni sare lakini kubwa ni wote wameVaa siku moja!?

Sina raha nahisi wamejuana na dalili ndio hizi wananionyesha.

Nipo kazini lakini sina mzuka wa kazi kuna rafiki yangu hapa ofisini yeye anajua ishu yote kanishauri niwagonganishe kwa mmoja nimpigie simu mwingine nitume msg lakini eneo la tukio Liwe ni hilo hilo moja, akiwa na maana kwanza nitajua kama wanafahamiana (walikuwa wakinizunguka tu).

Pili nitakuwa na nafasi pana ya kuwa na mmoja ambae nitatumia nafasi ya Moyo wangu kutimiza azma yangu ya kuwa na mmoja kwa yule ninaempenda sana,na hata kama wanajuana nitakuwa na options mbili.

1~ Kuwabwaga wote (japo hii sipendi itokee labda wao ndio waniache km watakuwa wameamua)

2~ Kumuangukia mmoja Kati yao (ni kuwakatiri kwa kumkana mwingine).

Jamaa kaniambia yupo tayari kuniratibia mpango mzima kama niko tayari.

Ndugu zangu kwanza mjue hii sio story ya kutunga au ya kusadikika hata mnapotoa ushauri mjue mnashauri kitu kitakachoenda kutokea.

Ahsanteni.
 
Naomba nikuulize kitu kimoja then nitakuja na ushauri mzuri wa kujenga.

question: Kwa nini huyo anayekupenda wewe humpendi?
 
Naomba nikuulize kitu kimoja then nitakuja na ushauri mzuri wa kujenga.

question: Kwa nini huyo anayekupenda wewe humpendi?

Sorry sio kama simpendi nisinge kuwa nae mpaka hii leo ila tu kuna mambo madogo madogo ambayo yanampunguzia lakini ki binadamu yanalekebishika...nikimlinganisha na huyu wa pili ambae vitu vingi hasubili maelekezo labda tu akwame ni mtu anaeweza kujiendesha ki maisha shida yake ni kisirani.
 
Wakristo sio wazinzi kama wewe,

chagua mmoja wewe mwenyewe sio ualike watu wakuchagulie.

Sawa mkuu nakubaliana na wewe kweli wakristo sio wazinzi hata mimi nikishapata nikifunga ndoa Sita taka tena kuwa kwenye hili joto Moyo ambalo linaninyima hata raha/uhuru wa kufanya kazi
 
Acha kuwacheza shere wadada wa watu

Mkuu madameX hata mimi pia nimechoka kuwa kwenye hii situation ndio maana bado niko kwenye mchakato wa kumuacha mmoja Kati yao bila kumuumiza.
 
Sorry sio kama simpendi nisinge kuwa nae mpaka hii leo ila tu kuna mambo madogo madogo ambayo yanampunguzia lakini ki binadamu yanalekebishika...nikimlinganisha na huyu wa pili ambae vitu vingi hasubili maelekezo labda tu akwame ni mtu anaeweza kujiendesha ki maisha shida yake ni kisirani.

Hapo unanishangaza kabisa, mara useme humpendi na sasa hivi unasema unampenda.

Nakuomba chunguza moyo wako kwa makini kwa kuwa ni walakini hujui unachokipenda.

nisamehe sana naweza kuwa nimekukwaza ila mimi mwenyewe majibu yako ndo nilikuwa nayafikiria inakuwaje mtu humpendi mtu na unakuwa nae na mahusiano?? kwa vile umenijibu vyema nakuomba usingaike na ushauri wa huku bali nenda kwa chumba chako utulie na uuchunguze moyo wako.

Maana wote hapo naona wana shida tofautitofauti na pengine ingekuwa mimi nikishindwa kupata majibu ya moyo wangu nawaacha wote naanza upya.

Kijana maisha ni mafupi sana kama utajipa stress za namna hii na vilevile ni maisha ni mazuri na marefu kama utaachilia some of the things and make a right decision.

TAFAKARI THEN CHUKUA HATUA.
 
Mkuu naomba urekebishe unapowaita 'wachumba' useme hata wapenzi/marafiki AU unataka kutuaminisha kuwa wote umeshaenda kujitambulisha kwao na kuwavisha pete za uchumba?
 
Wakristo ndoa ni moja tu

Sasa kwa nini unao wawili tayari

Au kanisani kwenu na Mungu wenu anaruhusu ZINAA/NGONO kabla ya kuoana?

Huu unaoufanya na unaotaka kuufanya ni utoto.

Assume ndo mdogo wako au dadako wa kike agonganishwe na wakwale wa mjini kisha wewe ujue ungejisikiaje???
 
Hapo unanishangaza kabisa, mara useme humpendi na sasa hivi unasema unampenda.

Nakuomba chunguza moyo wako kwa makini kwa kuwa ni walakini hujui unachokipenda.

nisamehe sana naweza kuwa nimekukwaza ila mimi mwenyewe majibu yako ndo nilikuwa nayafikiria inakuwaje mtu humpendi mtu na unakuwa nae na mahusiano?? kwa vile umenijibu vyema nakuomba usingaike na ushauri wa huku bali nenda kwa chumba chako utulie na uuchunguze moyo wako.

Maana wote hapo naona wana shida tofautitofauti na pengine ingekuwa mimi nikishindwa kupata majibu ya moyo wangu nawaacha wote naanza upya.

Kijana maisha ni mafupi sana kama utajipa stress za namna hii na vilevile ni maisha ni mazuri na marefu kama utaachilia some of the things and make a right decision.

TAFAKARI THEN CHUKUA HATUA.

Ahsante mkuu nashukuru kwa kunielewa lakini zaidi kwa kunishauri..hizi mambo za kupenda wawili wanaume zinatukuta si unajua unaanzisha uhusiano ukijua nazugia baadae unanogewa.
Ni kama kulamba asali then ukachonga mzinga.
 
Mkuu naomba urekebishe unapowaita 'wachumba' useme hata wapenzi/marafiki AU unataka kutuaminisha kuwa wote umeshaenda kujitambulisha kwao na kuwavisha pete za uchumba?

Sawa mkuu naomba iwe hivyo lakin nieleweke tu sina nia mbaya nao Kati ya hao mmoja wapo anaweza kuwa mchumba mpaka mke kwani ndio lengo langu that's why nikawaita mchumba.
Ahsante kwa kunilekebisha pia
 
Sasa kama umeanzisha uhusiano na baadaye ukanogewa y kuanzisha mwingine??

Vijana tambueni ukimwi upo na ujue na hao mabinti nao wanakuwa na wengine kama wewe unavyofanya.

USHAURI: mapenzi ya amani na upendo ni uwe na mmoja. OVA
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom