hippocratessocrates
JF-Expert Member
- Jul 1, 2012
- 3,598
- 1,545
"Ameongea kwenye majukwaa, mashuleni hata vikao vya ndani ya CCM."
Jukwa gani ulishamwona EL kasimama kuhutubia? Labda sema aliongea huko monduli na kanisani tutakuelewa!
So what he said is true then, right?
Alikua ni PM tu, hakua na ultimate powers to run this country.
Huyu huyu Mheshimiwa Lowassa ambaye amekuwa kwenye nafasi za maamuzi kwenye uongozi wa serikali kwenye awamu zote nne. je Kuna hata legacy moja au harufu ya muenekano wa kumuendeleza mtanzania au kumuondolea umasikini Mtanzania ameweza kuutolea muono au kufanya kwa matendo ktk nafasi yake ya maamuzi.EL amekua akipiga kelele mpaka sauti kumkauka kwamba vijana wasio na ajira ni bomu linalosubiri kulipuka. Ameongea kwenye majukwaa, mashuleni hata vikao vya ndani ya CCM. Vurugu zote zinazoendelea leo ni kutokana na umasikini na kukosekana kwa fursa [ opportunities] kwa vijana wengi nchini. Ajira hamna, vikwazo visivyo na maana katika ujasiriamali, manyanyaso na kujuana kumepelekea suala dogo kuyumbisha nchi. Amani tunayoichukulia for granted inaanza kuyeyuka nchini mwetu.
Licha ya kwamba kuna udhaifu wa serikali yetu wa kutochukua hatua mapema kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kutokufuatutilia madai halali yanayolalamikiwa na waislamu, sera za CCM za divide and rule, ni wazi kwamba sakata hili limechocheka kwa kiasi kikubwa na vijana wanaokaa vijiweni kwa kukosa ajira.
Lowassa angekuwepo haya yasingetokea.
Siyo mshabiki mkubwa wa Mjenga, hasa baada ya sakata la Mwangosi, lakini leo hebu soma hii masterpiece yake leo
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/340157-ya-mbagala-na-bedui-aliyekojoa-msikitini.html
Umenena kweli,hakuna mwenye haki hata mmoja mbele za Mhukumu wa waliohai na wafu;yaani Mwenyenzi Mungu.Mnyonge mnyongeni haki zake mpeni EL kama ana makosa yake lakini anayo yasema yana ukweli ndani yake,hakuna bina damu aliye kamilika kila mtu ana mapungufu yake.
madai validi ya waislam ni yapi ambapo wakristu hawana? Au wakristo hawana tena wanachohitaji?
EL amekua akipiga kelele mpaka sauti kumkauka kwamba vijana wasio na ajira ni bomu linalosubiri kulipuka. Ameongea kwenye majukwaa, mashuleni hata vikao vya ndani ya CCM. Vurugu zote zinazoendelea leo ni kutokana na umasikini na kukosekana kwa fursa [ opportunities] kwa vijana wengi nchini. Ajira hamna, vikwazo visivyo na maana katika ujasiriamali, manyanyaso na kujuana kumepelekea suala dogo kuyumbisha nchi. Amani tunayoichukulia for granted inaanza kuyeyuka nchini mwetu.
Licha ya kwamba kuna udhaifu wa serikali yetu wa kutochukua hatua mapema kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kutokufuatutilia madai halali yanayolalamikiwa na waislamu, sera za CCM za divide and rule, ni wazi kwamba sakata hili limechocheka kwa kiasi kikubwa na vijana wanaokaa vijiweni kwa kukosa ajira.
Lowassa angekuwepo haya yasingetokea.
Katika ccm hakuna mtu mwizi kumzidi EL.
wewe umetumwa na nani kuja kumsafisha mtu? Au chimpumu na mnazi zinakuchanganya? Kuwa smart na unacho post.
jk,lowasa,na mtoa mada ni majanga mengine kwa taifa!!!
Ccm inatakiwa kukaa chini na kusema jamani haya sasa basi. Wasipofanya hivyo wataumia wao na watoto zao. Sie maskini hatuna cha kupoteza.
Uzi huu unaweza kuwa ba ukweli lakini chokochoko za dini zimeanza muda mrefu na aliyezipalilia na kuziivisha vizuri ni JK na magamba yake wakati wa kampeni baada ya kuishiwa sera na kuzidiwa na cdm. Suala la ajira kwa vijana ni secondary na chuki za kidini ni primary.
Kwangu mimi naona suala la ajira ni PRIMARY, kwa sababu vijana tungekua na ajira na elimu ya kutosha CCM wangetudanganya vipi ?
EL amekua akipiga kelele mpaka sauti kumkauka kwamba vijana wasio na ajira ni bomu linalosubiri kulipuka. Ameongea kwenye majukwaa, mashuleni hata vikao vya ndani ya CCM. Vurugu zote zinazoendelea leo ni kutokana na umasikini na kukosekana kwa fursa [ opportunities] kwa vijana wengi nchini. Ajira hamna, vikwazo visivyo na maana katika ujasiriamali, manyanyaso na kujuana kumepelekea suala dogo kuyumbisha nchi. Amani tunayoichukulia for granted inaanza kuyeyuka nchini mwetu.
Licha ya kwamba kuna udhaifu wa serikali yetu wa kutochukua hatua mapema kwa vitendo vya uvunjifu wa amani, kutokufuatutilia madai halali yanayolalamikiwa na waislamu, sera za CCM za divide and rule, ni wazi kwamba sakata hili limechocheka kwa kiasi kikubwa na vijana wanaokaa vijiweni kwa kukosa ajira.
Lowassa angekuwepo haya yasingetokea.
Siyo mshabiki mkubwa wa Mjenga, hasa baada ya sakata la Mwangosi, lakini leo hebu soma hii masterpiece yake leo
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/340157-ya-mbagala-na-bedui-aliyekojoa-msikitini.html
haya yanayotokea hayana uhusiano na ukosefu wa ajira. Ni upungufu tu wa ufahamu na maarifa kadhaa. Ni sawa na kutaka kutuaminisha kuwa hili ni Taifa la kiislam kwani wanaosumbua huko ni wao pekee. Hakuna wakristo wasio na ajira? Wamevunja cha mtu? Tatizo ni mbegu ya chuki na utengano inayopandikizwa kisiasa kwa mgongo wa imani
Sasa huyo Lowasa angekuwa 'visionary' kama unavyomuita wewe, asingefanya ufisadi na kuitumbukiza nchi kwenye mkenge wa Richmond na Dowans.
Au labda katika hilo swala la Richmond na Dowans, alikuwa bado hajawa 'visionary'??
Machafuko yanayotokea sasa sio matokeo ya vijana kukosa kazi, ila ni matokeo ya Kikwete kupandikiza udini na kuupalilia.
Hebu angalia, maandamano na vurugu hizi zinazoendelea sasa, zinafanywa na vijana wanaodai ajira ??
Vurugu hizi zilipangwa rasmi kabisa ili zitokee, na kwa bahati mbaya sana zikapata kisingizio cha 'mtoto kukojolea quran'.
Vurugu hizi ni za kidini, na sio za kiuchumi. Watu kuchoma makanisa sio vurugu za kiuchumi.
Au wewe na Lowasa mnadhani kuwa watu wakichoma makanisa ni ishara ya kukosa ajira ??
Au wewe ukikosa ajira utaenda kuchoma kanisa ??
Ushauri kwako na kwa Lowasa ni huu:-
- Acheni ufisadi ili nchi ineemeke kwa utajiri iliyonao, na hakutakuwa na ukosefu wa ajira.
- Mshaurini mwenzenu Kikwete akemee na kuchkua hatua za kukomesha udini hapa Tanzania, badala ya kukimbilia Oman wakati nchi yake inaingia kwenye machafuko ya kidini.