samsun
JF-Expert Member
- Feb 9, 2014
- 7,386
- 5,968
Wakuu natumai ni wazima,kama kichwa cha habari kinavyosema " sasa tunaenda kwenye maisha halisi" ndiyo tunaenda kwenye maisha halisi ya watanzania tunayostahili kuishi.
Mahoteli hayana wateja,kinachofuata ni kupigwa mnada kama walikopa au kuuza kwa hiyari yao kama hawadaiwi,huku mengine yakibadilishwa matumizi.
Nyumba,viwanja na magari yanauzwa kwa wingi sana kipindi hiki na mbaya zaidi vinauzwa kwa bei ya "kutupa" msemo ambao tungeutumia miezi 10 nyuma,lakini kwasasa pamoja na kuuzwa kwa hiyo bei ya "kutupwa" bado hakuna wateja na vinazidi kushuka bei na bado watu hawafiki bei.
Sasa ndio ninaposema tunaenda kwenye maisha halisi,Dar ilikuwa si rahisi kwa wewe mwenzangu na mimi kuingia kwenye Hotel za nyota 2,3,4,5,lakini kwasasa wale wateja waliokuwa wanawapa viburi vya kupandisha bei kila asubuhi hawapo tena.
Nani atakaye ficha Petrol kwa sasa,eti ili bei ipande wakati kodi aliyolipa tu imeshamvuruga kichwa ........Kipindi cha nyuma alifanya hivo kwa vile mafuta yenyewe hayakulipiwa kodi stahiki ,na watu pesa ya kujazia magari yao petroli wanayo kwahiyo wateja walikuwa wengi na pesa walikuwa nazo,ndio maana walikuwa na jeuri ya kuyaficha.
Nani anayepandisha bei kiholela sasahivi,wakati kwanza wateja wenyewe wa kuwamulika kwa tochi,na wakati huo huo anapigania ile kodi aliyolipa irudi ........... Lakini miezi 10 nyuma walifanya hivo kwanza,hawakulipa kodi stahiki,pili wateja ni wengi mno wanagombea biashara yake.Kwahiyo watu walilinga kwavile waliingiza pesa WASIZOZITOLEA JASHO.
NI KWELI HALI NI NGUMU,NA HII NDIO HALI TULIYOTAKIWA KUWA NAYO TOKEA ZAMANI KWASABABU TULIKUWA TUISHI MAISHA SIO YETU,LAKINI SASA TUNAELEKEA KWENYE MAISHA HALISI YA MTANZANIA.