sasa tufundishane kupika....... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

sasa tufundishane kupika.......

Discussion in 'JF Chef' started by pauline, Jun 5, 2011.

 1. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #1
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  hii ni mojawapo ya sectors za malavi davi inakyokuwa overlooked ila aparently inasababisha matatizo.....sasa wenye uzoefu tupeane maujuzi humu,tusije tukaachika bure lol.....tufundishane namna nyengine za kupika nyama,wali,mboga za majani na vile vyakula vya asili.....kujua aina moja tu ya upishi inachosha tufundishane varieties jamani..................
  NB.....na wale wengine wenye recipe rahisi rahisi na fupi mnaweza kuongezea hata wakaka wanaoishi kibachela napo wapate maujuzi........mie mpaka leo sijui kupika wali wa nazi ingawa kila siku najitahidi kujaribu lol....nawish by the time naolewa niwe nimejuwa lol................
  [​IMG]
  nimeona hii picha facebook,nikawa mpole mie sjui kama nitaweza kuja siku moja kutandaza meza namna hii........ 196267_1485452194639_1783941010_893784_7589132_n.jpg

  najua siko peke yangu wadada tuzungumze kikike mambo yasiharibike:becky::becky::mwaaah:...naombeni kwa kuanzia mnaojua zile sambusa ile nyama ya ndani ya kusaga wanatia viungo gani/wanapikaje?..........karibuni.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jun 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Hehehehe leo tu nimetoka kuombwa na mkaka mmoja nimfundishe kupika.Tungewekewa jukwaa mi kila siku ningeweka picha na recipe zangu...napenda kucheza na viuongompaka basi wee!Nwy ngoja nipige picha nianze nlivyopika leo...
   
 3. itnojec

  itnojec JF-Expert Member

  #3
  Jun 5, 2011
  Joined: Mar 31, 2011
  Messages: 2,191
  Likes Received: 223
  Trophy Points: 160
  hayaa mloipitia cookery mwageni mambo
   
 4. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #4
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  jamani mnawekaje picha inakuwa kubwa?? mie nikiweka inatokea kadooogo???:confused2::confused2:
   
 5. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #5
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  thanks lizzy we are waiting....:mwaaah:
   
 6. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #6
  Jun 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  IMG382.jpg
  Owkey so leo nimepika Chicken curry ndizi nyama na wali mweupe tu wa kawaida.

  Chicken masala...
  Kiasi cha vitu itabidi nikisie maana mi hua sipimi natumia tu uzoefu.
  Kuku 1/2 kg
  Beans kikombe kimoja
  Mafuta vijiko 3 vya chakula
  Tui la nazi kikombe kimoja
  Nyanya nzima moja au ya kopo nusu kikombe
  Curry vijiko 4 vya chakula
  Chicken masala vijiko 3 vya chakula
  Carrot moja na kitunguu na vipande viwili vya vitunguu swaumu.

  Kwanza chemsha kuku na beans mbali mbali lakini..usisahau chumvi kiasi upendacho.Vikishaiva vichuje umwage maji ya beans ila mchuzi wa kuku uache.Kaanga vitunguu kabla hata havijawa brown weka karoti ulizozikata kwa umbo lolote upendalo.Karoti zikianza kulainika weka kuku wako navitungu swaumu hapo hapo.Binafsi hua sivikaangia na vitunguu ililadha yake isiishe kwenye kukaangwa.Nwy kaanga mpaka kuku nayo ianze kua brown kwa mbali...then tia beans na baada ya dakika mbili weka viuongo vyako vyote.Hapa kama ni mpenzi wa pilipili ndo muda muafaka kuweka. Acha viuonge vikolee mpaka uone vitu vinaanza kung'ang'ania kwenye sufuria weka nyanya zako na uruhusu ziive kidogo kabla ya kuweka ile supu kidogo iliyobaki.Funika kisha uache ichemke kwa dakika tano kabla ya kuweka tui lako la nazi.Koroga mpaka ianze kuchemka tena ili tui lisikatika...onja chumvi...funika kisha punguza moto.Baada ya dakika kama nane itakua tayari.  IMG387.jpg
  Ndizi nyama.
  Mahitaji

  Ndizi nne au tano.
  Viazi vikubwa 8-10
  Nyama ya ng'ombe 1/2 kg
  Kipande cha tangawizi + kipande cha limao
  Nyanya moja + hoho + karoti 1
  Kitunguu
  Royco kijiko 11/2 cha chakula
  Tui la nazi 11/2 kikombe cha chai
  Vitunguu shaumu vipande vitatu
  Mafuta kiasi

  Kata nyama..kamulia kipande kimoja cha limao..kwangulia kipande cha tangawizi na vitunguu swaumu...weka maji kikombe kimoja na nusu+ chumvi kisha chemsha mpaka ilainike.

  Wakati nyama inachemka menya ndizi na viazi vyako kisha vioshe.Chuku nusu ya ndizi na viazi vyako uweke kwenye sufuria unayotaka kupikia.Then katakata nyanya..hoho..vitunguu na karoti zako uweke kwenye mchanganyiko wako uliotanguliza kwenye sufuria.Baada ya hapo chukua ile nyama pamoja na mchuzi umimine juu ya mchanganyiko wako.Weka chumvi na ongeza maji kidogo kisha weka viazi na ndizi zilizobaki.Funika na uweke jikoni.Acha vichemke mpaka vilainike kisha weka royco yako na mafuta.Acha vichemke kwa dakika chache kabla ya kuweka tui lako la nazi.Usisahau kukoroga mpaka ndizi zako zianze kuchemka tena.Punguza moto...funika na uache kwa dakika kumi kabla ya kuipua.

  Kilichobaki sasa ni kupakua na kufurahia tu....usisahau kushushia na maji.Ukiwa na parachichi ndizi zako zitanoga zaidi!!
   
 7. Nyani Ngabu

  Nyani Ngabu Platinum Member

  #7
  Jun 5, 2011
  Joined: May 15, 2006
  Messages: 73,657
  Likes Received: 35,418
  Trophy Points: 280
  We Lizzy usinimalizie chakula...manake wee mlafi sana wewe.
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  Jun 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Nilikupikia wewe???Utakula kuona mwaka huu!!!
   
 9. Nemo

  Nemo JF-Expert Member

  #9
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 80
  Pauline:
  Whoever made this, hongera zake maana its very impressive! Ila mimi personally my biggest problem is quantity, yaani I can make a kick a** meal for 4 people or less, lakini usually fail miserably when chakula kikiwa cha wengi. Taste inakuwaga "mbofu mbofu". Sijui ndio uchoyo au.......:smiling:
  Anyways wacha nisubiri wenye maujuzi yao wakija, so I can learn.
   
 10. Nemo

  Nemo JF-Expert Member

  #10
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 662
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 80
  Lizzy:
  The chicken does look delicious. THanks for the recipe, Ill try it soon enough nikiwa na wageni.
   
 11. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #11
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  uko kama mimi Nemo.....especially ugali nitajitahidi kama ni wa mtu mmoja au wawili zaidi ya hapo ni madudu tu...:becky::glasses-nerdy:
   
 12. pauline

  pauline JF-Expert Member

  #12
  Jun 5, 2011
  Joined: Dec 26, 2010
  Messages: 651
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Thanks lizzy....nitajaribu hio kuku kesho....
   
 13. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #13
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...kwa jinsi ninavypenda chapati,...sijui itakuwaje tu mamsapu akinambia hajui kuzipika.
   
 14. CPU

  CPU JF Gold Member

  #14
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Daaah
  Hii fani mara zote ni mgumu kuielewa ila napenda kula
   
 15. CPU

  CPU JF Gold Member

  #15
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  I opened my teeth now
  :becky::becky::becky:

  Mkuu chapati haina kazi sana, labda chapati za kuwekea makorombwezo mpaka zionekane kama mayai ya Spanish
   
 16. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #16
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  ...zaidi ya zile chapati pale, hakuna chochote hapo ninachoweza msifia mpishi huyu ufundi wa kupika 'mahanjumati'
   
 17. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #17
  Jun 5, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,921
  Likes Received: 83,432
  Trophy Points: 280
  Pauline, hebu ongezea ugali hapo, bamia/mchicha na samaki wa kukaanga :) ili wengine tuweze kujisikia sikia kama tumepata mlo wa uhakika
   
 18. CPU

  CPU JF Gold Member

  #18
  Jun 5, 2011
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,871
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 135
  Kweli KILA MBUYU NA SHETANI WAKE . . .
   
 19. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #19
  Jun 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Chapati haina kazi??Chapati gani unaongelea wewe!??
   
 20. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #20
  Jun 5, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Asante mwaya...usisahau kuleta matokeo!!
   
Loading...