Uncle Jei Jei
JF-Expert Member
- Jan 7, 2011
- 1,684
- 2,156
Ukisikiliza hutuba zake kiongozi wetu mkuu na Raia namba moja wa nchi yetu tukufu, kuna neno analipenda zaidi la kwamba yeye ni msema kweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu! Taratibu naanza kuamini kauli yake kwani watu wa kweli mara nyingi wanashinwa kuficha hisia zao hadharani tofauti kabisa na watu waliozoea kusema uongo na ambao wanaishi kwa unafiki unafiki
Wakati ACT inaanzishwa yalisemwa mengi kuwa huenda kikawa tawi la chama fulani lakini nguvu nyingi zilitumika kukataa hilo. Mara vuuupu! Zitto Kabwe akaibuka na cheo ambacho nacho kikaleta minong'ong'o miongoni mwa wadau.
Sasa kwa mwenyekiti wake kukabidhiwa ilani ya chama kingine na kutumwa na mamlaka ya juu kabisa kwenda kuisimamia na kuitekeleza kuna haja ya kupinga tena yaliyosemwa!?
Hongera Rais kwa kutuonyesha sura halisi ya wanaojiita wapinzani! Natamani na Mh. Zitto Kabwe ateuliwe wizara ya Nishati na madini maana na yeye ni msomi mzuri tu na mbobezi wa uchumi ili ubishi uishe kabisa! Naamini ataitendea haki wizara atakayo pewa