Sasa nimeamini kuwa kweli Mh. Rais ni msema kweli na daima ukweli huweka mambo wazi

Uncle Jei Jei

JF-Expert Member
Jan 7, 2011
1,684
2,157
Ukisikiliza hutuba zake kiongozi wetu mkuu na Raia namba moja wa nchi yetu tukufu, kuna neno analipenda zaidi la kwamba yeye ni msema kweli na msema kweli ni mpenzi wa Mungu! Taratibu naanza kuamini kauli yake kwani watu wa kweli mara nyingi wanashinwa kuficha hisia zao hadharani tofauti kabisa na watu waliozoea kusema uongo na ambao wanaishi kwa unafiki unafiki

Wakati ACT inaanzishwa yalisemwa mengi kuwa huenda kikawa tawi la chama fulani lakini nguvu nyingi zilitumika kukataa hilo. Mara vuuupu! Zitto Kabwe akaibuka na cheo ambacho nacho kikaleta minong'ong'o miongoni mwa wadau.

Sasa kwa mwenyekiti wake kukabidhiwa ilani ya chama kingine na kutumwa na mamlaka ya juu kabisa kwenda kuisimamia na kuitekeleza kuna haja ya kupinga tena yaliyosemwa!?

Hongera Rais kwa kutuonyesha sura halisi ya wanaojiita wapinzani! Natamani na Mh. Zitto Kabwe ateuliwe wizara ya Nishati na madini maana na yeye ni msomi mzuri tu na mbobezi wa uchumi ili ubishi uishe kabisa! Naamini ataitendea haki wizara atakayo pewa
 
Kama ni mfatiliaji mzuri, hayo maneno "msema kweli ni mpenzi wa Mungu" siku hizi wala huwa hayatumii tena.

Aliyatumia sana pale mwanzoni alivyoingia madarakani lakini siku hizi wala hayagusi.

Hii ni kwasababu ameshagundua watu wanamwona hana tofauti yoyote na walewale tu.

Ukishakuwa mwana CCM kamwe hauwezi kutofautiana Na wenzako ambao ni walaghai, waongo, wabadhilifu, Wezi, wala rushwa nk.
 
Raisi wetu amekuwa wa mipasho.Namshauri awe anajaribu kidogo kutoa maelekezo na kufafanua sera zaidi kuliko hicho ninachokisikia sasa
 
Anasema Chadema wanamwomba awateue, ila Kusema ni Nani anashindwa,

Act sio wapinzani, alishasema hatafanya kazi na wapinzani
 
Back
Top Bottom