Sasa ni zamu ya ACT Wazalendo kukataa ujinga na kutuonyesha kuwa nyie si wasaka vyeo bali wazalendo kweli

Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
13,530
51,250
Ndugu zangu wa ACT-Wazalendo

Fanyeni mfano wa CHADEMA, achaneni na ujinga wa serikali ya umoja wa Kitaifa huko Zanzibar!.

Serikali ya umoja wa kitaifa inaweza kupatikana tu katika uchaguzi huru, wa haki ambao maamuzi ya wananchi kweli yameheshimiwa
Serikali ya umoja wa kitaifa haiwezi kupatikana pale ambapo maamuzi ya wananchi yemepinduliwa kijeshi, kwa kura za maruhani, kwa kura za lumbesa, kwa kutesa, kupiga na kuua wananchi.

Huu siyo muda wa viongozi kugawana vyeo,au kukaa katika meza za madhalimu kula. Huu ni muda wa kupaza sauti, kukataa dhulma kwa nguvu zote!. Haiwezekani chama kipeleke majina ya uhalifu dhidi ya binadamu ICC halafu chama hichohicho kikae na wahalifu haohao serikali hiyohiyo iliyopatikana baada ya uhalifu mkubwa wa binadamu.

Kama ACT itafanya ujinga huo, tutaipuuza, tutaidharau, na viongozi wake wote watakaoshiriki haramu hiyo tutawadharau moja kwa moja kwa sababu wanawaza matumbo yao na si mustakbali mwema wa watu wa Zanzibar na Tanzania kiujumla

Wenzenu CHADEMA jana wamesimama kiume na wamelinda heshima ya chama chao, na imani yetu kwao imeongezeka mara dufu!. Sasa nyie ACT msituangushe!. Waacheni CCM na serikali zao zilizopatikana kiharamu, sisi tuendelee kudai tume huru ya uchaguzi na Katiba mpya

Achaneni na mambo ya kuuliza kura za maoni kwa wanachama wenu, Kisaikolojia tunajua mnataka kuhalalisha haramu haalfu mkwepe lawama kuwa wananchama walisema tuingie!. Hell no hiyo ni janja ya nyani na wananchi hatukubali!

Wananchi tunataka
1. Waliohusika na kutesa watu, kuua raia na kuvuruga uchaguzi washughulikiwe kwa njia zote za kisheria
2. Tunataka uchaguzi urudiwe
3. Tunataka tume huru za chaguzi
4.Tunataka katiba mpya iliyo bora

Sisi wananchi tuko tayari kwa mazungumzo na hatimaye maridhiano ya kitaifa, lakini mazungumzo hayo lazima yazae vitu vinne hapo juu, Nje ya hapo lazima struggle iendelee hata kama itachukua miaka 1000, lakini lazima tumkatae Shetani wa Ukandamizaji nchini kwa mambo yake yote, siyo tukae tuungane nao kwenye serikali iliyopatikana kiharamu!

Hivi Maalimu Seif huoni hasira kupewa na ZEC asilimia 19 tu ya kura wakati sisi tunajua wewe kwenye uchaguzi huru na haki ungepata asilimia nyingi sana?

Maalim akubaliye kudhulumiwa hugeuka mtumwa!.

Hutoisaidia Zanzibar kwa kucave in, bora uendelee kukataa dhulma, kuliko kuihalalisha
Sisi wananchi hatutokuelewa kabisaa ukikubali ujinga huu!

HAKUNA KUTEPETA, HAKUNA KULEGEA
MKILEGEA TU, WATAWALEGEZA MILELE, KILA BAADA YA MIAKA MITANO WATAFANYA USHENZI HUOHUO!
 
Mimi kama mzanzibar sikubaliani na SUK hata siku moja kwa miaka hii mitano unless uchaguzi urudiwe upya, tumeumiya sana, tumepoteza wapendwa wetu, kamwe siko tayari kuunga mkono majambazi ndani ya SUK. ZEC na ccm ni wauwaji wakubwa Tanzania Zanzibar
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom