Sasa ni wakati wa kuvipa vyama vya upinzani nafasi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa ni wakati wa kuvipa vyama vya upinzani nafasi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Bra-joe, May 24, 2012.

 1. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #1
  May 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Tanzania tangu uhuru tumekuwa tukiongozwa na Ccm na matokeo yake tumeyaona kuna mabaya na mazuri, kln kwa sasa ccm imetuweka ktk maisha ambayo kila siku tunasema bora ya jana, kwa kifupi ccm haina tena uwezo wa kuleta misha bora na maendeleo kwa watanzania, hivyo basi ni bora tukiweke chama kingine madarakani, na kwa sasa chama kilichojipanga kutuongoza na chenye nguvu ni Chadema, tuwachague Chadema halafu tuwape muda maalumu kuturekebishia nchi yetu, wakishindwa kurekebisha ndani ya huo muda tuwapige chini halafu tuchague chama kingine kitakachokuwa tayari wakati huo. Tukifanya hivyo vyama vya siasa vitajua watanzania tupo vipi. Mabadiliko ni muhimu.
   
 2. M

  MERCYCITY JF-Expert Member

  #2
  May 24, 2012
  Joined: Jan 25, 2012
  Messages: 348
  Likes Received: 197
  Trophy Points: 60
  Wananchi wanatakiwa kuelewa hilo hili kuzuia hizi mbinu za CCM za kuua vyama vya upinzani. CCM wana pesa na ni rahisi sana kuua upinzani kama walivyofanya kwa CUF, kumpa Mbatia Ubunge hili kuua NCCR . Sasa najua mbinu zao zote ni kwa Chadema ndiyo maana wakinaa shibuda wanakuja na yao kama vile wametumwa. Hii ni ile dhana ya CCM kwamba wao ni wa kutawala milele na kwa hilo inabidi wafanye mbinu zote hili waweze kubakia madarakani.
   
 3. Manumbu

  Manumbu JF-Expert Member

  #3
  May 24, 2012
  Joined: Oct 28, 2009
  Messages: 1,751
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  tukijenga utamaduni wa kuwatoa watawala wasiotimiza matakwa ya wananchi utakuwa ni utamaduni mzuri sana na urithi mzuri kwa vizazi vijavyo. hakuna haja ya kuwa na mapenzi na chama cha siasa kama vile ni sehemu ya familia yako. vyama vya siasa vina kazi ya kuwatumikia wananchi. vikichemsha, kama kilivyochemsha ccm kwa sasa, tunabadili uongozi wa nchi!
   
 4. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #4
  May 24, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  kila kitu kina mwanzo na mwisho, mtanzania wa jana si wa leo!
   
 5. Bra-joe

  Bra-joe JF-Expert Member

  #5
  May 24, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 1,559
  Likes Received: 510
  Trophy Points: 280
  Tukifanikiwa kufanya hivyo na amani iliyopo nchini, Tanzania itakuwa bonge la Nchi. E-mwenyezi MUNGU tusaidie.
   
 6. JingalaFalsafa

  JingalaFalsafa JF-Expert Member

  #6
  May 24, 2012
  Joined: Apr 13, 2012
  Messages: 759
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 45
  Unataka tufanye majaribio?
  IMETOSHA....huu ni wakati wa sisi kama wenye nchi kushika nchi yetu wenyewe, na si chama ama upuuzi mwingine.
  UMMA KAMA UMMA, ndio unaostahili kushika taifa letu! Ni UMMA! Democracy has proven failure in Africa, why should we still embrace it? Fool!
  Mungu wetu anaita sasa!
  Mungu wetu anaita.
   
 7. a

  andrews JF-Expert Member

  #7
  May 24, 2012
  Joined: Mar 28, 2012
  Messages: 1,680
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  UNGEMUULIZA MAMAYAKO KWA NINI ALIKUZAA:wacko:
   
 8. m

  mechard Rwizile JF-Expert Member

  #8
  May 24, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 938
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 80
  Huu ndio ukweli, bila kunfanya hivyo, hatutapata nafasi ya kuijenga nchi yetu na kuleta neema kama inavyotakiwa kuwa. Vyama vya siasa vinatakiwa kujua kwamba havina hati miliki ya utawala wa nchi hii.

  Watanzania tunayonafasi ya kukosoa makosa yaliyofanywa huko nyuma. Watanzania tunayo nafasi ya kulinda mazuri ya waasisi wa taifa letu. Watanzania tunayo nafasi ya kuandaa maisha bora kwa ajili ya watoto na wajukuu zetu.

  Kuweza kufanya hivyo, hatutakiwi kubweteka na kulishwa ujinga kuwa CCM wanaweza kujirekebisha kwa sasa. Mfumo wa CCM kuingia madarakani kwa miaka zaidi ya ishirini umejengwa kwa misingi ya rushwa, kulindana na ubadhirifu wa mali ya umma. Mfumo huu hauwezi ukajiua mwenyewe ni lazima umma uchukue jukumu la kujikomboa na kuanzisha mfumo wa kuwapiga chini wanasiasa na vyama visivyo na wasio tetea maslahi mapana ya umma.

  Mwaka 2015 ndio utakuwa mwaka wetu wa kujikomboa, kujiandikisha na kujitokeza kupiga kura.
   
Loading...