Sasa ni wakati muafaka wa nyerere kupewa utakatifu – sitta. Nipashe. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sasa ni wakati muafaka wa nyerere kupewa utakatifu – sitta. Nipashe.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Wamunzengo, Sep 2, 2012.

 1. Wamunzengo

  Wamunzengo JF-Expert Member

  #1
  Sep 2, 2012
  Joined: Aug 2, 2012
  Messages: 810
  Likes Received: 180
  Trophy Points: 60
  Wadau, hebu tulijadilini hili jambo kwa kina bila kuegemea upande wowote hasa kwa kuzingatia mustakabali wa taifa letu. Nimesoma katika gazeti la nipashe la leo hii jumapili, habari yenye kichwa cha habari SASA NI WAKATI MUAFAKA WA NYERERE KUPEWA UTAKATIFU. Hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Uhusiano wa Afrika Mashariki- Samwel Sitta. Nionavyo mimi, habari sio mbaya hasa kama ingekuwa imetolewa sehemu husika i.e. kanisani, lakini kinachonishangaza ni msemaji wa kauli hii kuwa ni waziri katika serikali i.e. Sitta, na anatoa tamko hili akiwa katika ziara ya kiserikali, akitumia kodi za watanzania wote bila kujali dini zao. Anautangazia umma wote bila kujali itikadi zao kidini utakatifu wa Nyerere, hii ina maanisha nini?? Ina maana Sitta anataka umma wa watanzania wote watambue utakatifu wa Nyerere, kivipi?? Utakatifu wa Nyerere unawahusu nini wapagani?? Utakatifu wa Nyerere unawahusu nini waislamu? utakatifu wa Nyerere unawahusu nini wahindu na watu na itikadi zingine?
  Wasiwasi wangu ni kwamba, kama hizi kauli zitaendelea kutolewa hadharani pasipohusika, kuna uwezekano wa kuzua mzozo, maana sio watanzania wote wanaokitambua hicho cheo cha utakatifu, na wala katiba ya Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania haina cheo kinachoitwa mtakatifu.
  Nionavyo mimi pamoja na kauli za kutokuhusianisha dini na serikali bado kuna dalili kuwa udini ulikuwa na nafasi katika utawala wa nyerere, ikumbukwe watanzania walishalazimishwa nyerere kuwa baba wa taifa, sijui kwa nini, kwani haikutosha tu kumpa heshima ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza na Rais wa kwanza waTanganyika na Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania??
  Je ikitokea kwa mfano, Waziri Wa Elimu Shukuru Kawambwa au Waziri Wa Ulinzi Vuai Nahodha akatangaza kuwa imefika wakati watanzania wote watambue ucha mungu wa rais mstaafu al hassan mwinyi hali ya kuwa yupo kwenye ziara ya kiserikali, hiii itapokelewaje na watu wasiokuwa waislamu?Wadau, hebu tulijadilini hili jambo kwa kina bila kuegemea upande wowote hasa kwa kuzingatia mustakabali wa taifa letu. Nimesoma katika gazeti la nipashe la leo hii jumapili, habari yenye kichwa cha habari SASA NI WAKATI MUAFAKA WA NYERERE KUPEWA UTAKATIFU. Hii ni kwa mujibu wa Waziri wa Uhusiano wa Afrika Mashariki- Samwel Sitta. Nionavyo mimi, habari sio mbaya hasa kama ingekuwa imetolewa sehemu husika i.e. kanisani, lakini kinachonishangaza ni msemaji wa kauli hii kuwa ni waziri katika serikali i.e. Sitta, na anatoa tamko hili akiwa katika ziara ya kiserikali, akitumia kodi za watanzania wote bila kujali dini zao. Anautangazia umma wote bila kujali itikadi zao kidini utakatifu wa Nyerere, hii ina maanisha nini?? Ina maana Sitta anataka umma wa watanzania wote watambue utakatifu wa Nyerere, kivipi?? Utakatifu wa Nyerere unawahusu nini wapagani?? Utakatifu wa Nyerere unawahusu nini waislamu? utakatifu wa Nyerere unawahusu nini wahindu na watu na itikadi zingine?
  Wasiwasi wangu ni kwamba, kama hizi kauli zitaendelea kutolewa hadharani pasipohusika, kuna uwezekano wa kuzua mzozo, maana sio watanzania wote wanaokitambua hicho cheo cha utakatifu, na wala katiba ya Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania haina cheo kinachoitwa mtakatifu.
  Nionavyo mimi pamoja na kauli za kutokuhusianisha dini na serikali bado kuna dalili kuwa udini ulikuwa na nafasi katika utawala wa nyerere, ikumbukwe watanzania walishalazimishwa nyerere kuwa baba wa taifa, sijui kwa nini, kwani haikutosha tu kumpa heshima ya kuwa Waziri Mkuu wa kwanza na Rais wa kwanza waTanganyika na Jamuhuri Ya Muungano Wa Tanzania??
  Je ikitokea kwa mfano, Waziri Wa Elimu Shukuru Kawambwa au Waziri Wa Ulinzi Vuai Nahodha akatangaza kuwa imefika wakati watanzania wote watambue ucha mungu wa rais mstaafu al hassan mwinyi hali ya kuwa yupo kwenye ziara ya kiserikali, hiii itapokelewaje na watu wasiokuwa waislamu?
   
 2. Songoro

  Songoro JF-Expert Member

  #2
  Sep 2, 2012
  Joined: May 27, 2009
  Messages: 4,136
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 0
  Haina shida,hilo tangazo haliongezi gharama kwa serikali, St nyerere anahitajika kutumika kwenye maombi kuponya wenye matatizo, si unajua miungu mingi isha expire kuna uhaba mkubwa sana!
   
 3. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #3
  Sep 2, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,673
  Trophy Points: 280
  Ngoja kwanza wachangie wanaojiita wazalendo sio wengine tutachangia baadae tusije kuitwa wadini hatukusoma tuna wivu na Kanisa.
   
 4. j

  j joni Member

  #4
  Sep 2, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona mh. Sitta anachanganya madawa vibaya. utakatifu wa kanisa katoliki hautokani na maoni ya watu hata Wakatoliki, bali ni mchakato. Mtu hakifilisika kisiasa atatumia lolote kupata uhalali kisiasa. Nukuu ya mwalimu
   
 5. Nicholas

  Nicholas JF-Expert Member

  #5
  Sep 2, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 25,132
  Likes Received: 2,355
  Trophy Points: 280
  Mzee kadata mziki wa wasio ma -DJ ngoja DJ arudi mzee ata spin infinitely.Kajuaje kuwa wakatoliki wote wanataka Mwalimi apewe huo utakatifu?Mzee hajui kuwa ya wakatoliki awaachie wakatoliki na catholic ni kama FIFA huwa kuingiliwa na state ni issue ndio maana China wana mgogoro nao.Sijui mzee anataka tuambia kuwa akiwa rais atafanya hivyo?Mzee hajui RC sio Anglican church hadi Mfalme awe ndio mkuu wa kanisa.Mzee hajui kuwa hawezi kuwa na envoy ya kwenda vatican dai hilo?Bora Jk na issue ya Madrid.

  6 kaanza pagawa mapema hivi wakati CDM hawaja dismantle.Nimewaabia wengi kwa siasa za bongo si slama sana kuanzisha ligi na CDM, hata wakikulipua, ni salama kuka kimya na waandishi wakiuliza ni bora wapa jibu "Muda muafaka ukifika nitajibu". Na hivyo kufanya CDM wasiongeze dozi hasa kwa mambo ya kudhoofisha kama makosa yaliyofanyika kweli.Akawawaulize CUF, Mkapa, Wassira, Pinda, na wengine.

  Huyu dancer ata dance sana katika kila disco.
   
Loading...