Sasa ni rasmi kuelekea chaguzi za 2019 na ule wa 2020 Watanzania tunaanza ' Kulainishwa ' taratibu

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,571
108,922
Kuna Watu wawili mpaka sasa Mmoja nilimsikia hapa juzi kati na mwingine nimebahatika kumsikia leo ama hakika wameanza kuonyesha jinsi walivyo Wanafiki watupu. Kila nikizikumbuka Kauli zao za ' Kibabe ' kama si za ' Kidekteta ' hawa Watu wawili kuanzia mwaka 2016 hadi hapo 2018 siamini kama leo ni kweli hao hao wamebadilika na kujifanya wana Mioyo ya Kibinadamu na Huruma.

Na kwa ninavyowajua Watanzania sasa hivi watawaamini na kuyasahau Machungu yao yote ambayo kwa 75% yalisababishwa na hawa hawa Watu wawili ambao leo hii wanajifanya ni Malaika wazuri, wanajua Utu na Ubinadamu kana kwamba vile wanataka kutuaminisha kuwa zile Kauli zao hazikuwa zao bali yawezekana waliingiwa tu na ' Mapepo ' na sasa yameshawatoka.

Danganyikeni na Lainikeni nyie ila Mimi An Eagle najua tu ya kwamba hasira zangu nazimalizia November 2019 na October 2020 ili basi iwe Fundisho kwa Wanafiki wengine wote ambao watathubutu Kujitokeza. Tanzania ya sasa siyo ile ya wale wa ' Oya Oya ' waliozoeleka miaka ile bali Watanzania wa sasa wanajielewa tena yawezekana hata kuliko hawa / hao Watu ' Wanafiki ' wawili.

Kudadadeki zenu!
 
Hapo Musa Hassani (Kwa kimakonde)

Kafa nani, lini, kwa sababu gani, Maiti iko wapi sasa na atazikwa wapi, lini na Saa ngapi? Mimi nipo zangu Kwetu hapa nchini Malawi huu ni mwaka wangu wa 23 sasa na huku Lilongwe hakuna Majina hayo sijui ya Musa Hassan bali Majina mengi huku ni ya akina Banda, Muluzi na Lwandamina.
 
Back
Top Bottom