Sasa ni muda wa wewe kuchukua hatua, usipofanya leo hutofanya milele

Makirita Amani

JF-Expert Member
Jun 6, 2012
1,908
3,371
Haijalishi unaishi wapi, haijalishi umeanzia wapi na haijalishi dini yako au kabila lako, kuna kitu kimoja ambacho kiko sawa kwa watu wote, MAFANIKIO YAPO KWENYE MIKONO YAKO MWENYEWE.
Yaani pamoja na yote unayopitia, wewe ndio utakayeamua kama unataka kufanikiwa au la. Hata ungepewa mazingira mazuri kiasi gani na ukapewa kila kitu unachohitaji, kama usipoamua kutoka ndani yako kwamba unataka kufanikiwa huwezi kufanikiwa.

Unaweza kujishawishi kwamba kama ungeanzia kwenye msingi mzuri ingekuwa rahisi kwako kufikia mafanikio, unaweza kujishawishi kwamba kama ungekuwa na kazi bora leo usingekuwa kwenye matatizo yoyote. Yote haya unajishawishi ili tu kuepuka ukweli kwamba mafanikio yapo kwenye mikono yako na ni maamuzi yako binafsi.
Kila mtu anao uwezo wa kufikia mafanikio makubwa. Lakini atafikia mafanikio hayo makubwa kama ataamua kweli kuyafikia.
[h=1]Kama ni rahisi hivi kwa nini watu wengi hawajafanikiwa?[/h] Ukweli ni kwamba njia ya mafanikio sio njia iliyonyooka. Ni njia yenye kona na vikwazo vingi na kila mara inashawishi kupumzika au kuachana kabisa na safari hiyo. Ndio maana wanaweza kuanza biashara watu wengi lakini wachache sana ndio wanaofikia mafanikio makubwa. Vile vile watu wengi wanatamani kufanikiwa lakini wachache ndio wanaofikia mafanikio hayo.
Pamoja na kwamba umeamua kuanza safari ya mafanikio unahitaji mazingira ambayo yatakusaidia usikate tamaa. Unahitaji mazingira ambayo yatakutia moyo na kukuonesha njia pale mambo yanapokuwa magumu.
Katika jamii zetu hakuna mazingira hayo, katika kazi zetu hakuna mazingira hayo. Huku kumejaa mazingira ya kukatishana tamaa na kushawishiana kuenda na maisha kama yanavyowapeleka watu.
[h=1]Utapata wapi mazingira haya mazuri?[/h] Kama kweli umejitoa kufikia mafanikio makubwa na kama kweli umeamua kuachana na sababu zote ambazo umekuwa ukijidanganya kwamba zinakuzuia kufikia mafanikio, kuna mazingira mazuri sana ya wewe kuweza kufikia mafanikio.
Endelea kusoma hapa ili kujua jinsi ya kupata mazingira mazuri;
Sasa Ni Muda Wa Wewe Kuchukua Hatua, Usipofanya Leo, Hutofanya Milele. « AMKA MTANZANIA
 
Back
Top Bottom