Sasa ni muda muafaka wakukiri wasiojulika, wametushinda!

Dr Adam Francis

JF-Expert Member
Joined
Aug 12, 2011
Posts
464
Reaction score
687
Swala la watu wasiojulikana lilipoanza kusikika nchini ilionekana kuwa ni changamoto ambayo kwa uimara wa intelijensia yetu, ingepata mwarobaini ndani ya muda mfupi. Katika hali ya kushangaza matukio yanayofanywa na wasiojulikana badala ya kupungua, yamekuwa yakiongezeka kwa idadi na umadhubuti mpaka sasa yamekuwa ni janga la kitaifa.

Matukio ya mwanzo, kama lile la Mo Dewji, yalikuwa na sura ya kuvizia na kujifichaficha, lakini sasa hivi wasiojulikana hawavizii na kujificha tena, wanaweza wakasimamisha basi la abiria, eneo kama Tegeta ndani ya jiji la Dar es salaam, wakamshusha mtu kama mzee Kibao na kesho mkamkuta ametupwa akiwa marehemu.

Hebu fikira, kama makundi ya watu yanaweza kuchukuliwa ndani ya viunga vya mahakama maarufu kama Kisutu, tena ulinzi ukiwa umeimarishwa, wakapakiwa kwenye magari, na baadaye kukutwa Ununio na Mabwe pande wakiwa wamevunjika miguu, nawaliofanya hayo ukaambiwa ni watu wasiojulikana, Je ni mtanzania gani yupo salama mbele ya wasiojulikana?

Si ajabu sasa tunasikia Rev, Fr, Kitima ameshambuliwa na wasiojulikana ndani ya eneo la baraza la maaskofu kama ilivyokuwa kwa Tundu Lisu kupigwa risasi ndani ya makazi ya viongozi Dodoma. Kinachotisha zaidi ni kuwa, kama wasiojulikana wanaweza kutekeleza jaribio la mauaji ndani ya eneo lenye ulinzi la baraza la maaskofu, ikitokea wakiitaka roho ya mtu kama mm siitakuwa ni swala kuchinja kuku tu!

Tunasimuliwa humu mitandaoni kuwa Benny Saanane, Deusdedith Soka na hivi karibuni la Mdude Nyagali kuwa walikamatwa na watu wasiojulikana na hawajulikani walipo. Aidha jeshi la polisi katika taarifa zake rasmi, nalo limethibitisha kuwa watu hawa haijulikani walipo.

Kwa uzoefu tulioupata wa matukio ya watu wasiojulikana, ukisikia ndugu yako amekamatwa ni vyema mkaanza kumtafuta vichakani, misituni na kwenye fukwe za bahari maana hayo ndio maeneo ambayo watu wasiojulikana hupenda kutelekeza miili ya watu waliowatesa au kuwaua.

Binafsi sitaki kuamini kama wasiojulikana ni mkono wa dola, ila Ikiwa sisi kama nchi tumeshindwa kuwajua na kuwadhibiti wasiojulikana basi ni vyema tuombe msaada kutoka kwa mataifa mengine yaje kutusaidia kuwatafuta na kuwadhibiti wasiojulikana ili tunusuru uhai wa watu wetu. Hatuwezi kuwa na nchi ambayo wasiojulikana wanaua na kuwatia vilema watu wetu halafu tunaizoea hali hiyo kana kwamba ni hali ya kawaida.

Uhai wa mtu ndio zawadi kubwa zaidi mtu aliyopewa na Mungu wake iwe baraka kwake na kwa familia yake. Mtu anapouawa, hapotezi marehemu tu, bali wazazi, watoto, mwenza na wategemezi wa huyo mtu wanapoteza pia. Nawasihi wasiojulikana kuwa na moyo wa huruma. Ikiwa sisi watanzania tumewakosea basi watusamehe, ili tuendelee kuishi maisha yetu kwa amani.
 
Ndugu wasiojulikana ni polisi. Wala hakuna haja ya kuzunguka.
Kuna vikosi ambavyo vinapokea maagizo na kutekeleza. Polisi kama polisi hawezi amka nyumbani kwake na kwenda kuteka au kupiga mtu. Ni kwamba kuna watoa oda au maagizo kwamba flani afanywe nini.
 
Swala la watu wasiojulikana lilipoanza kusikika nchini ilionekana kuwa ni changamoto ambayo kwa uimara wa intelijensia yetu, ingepata mwarobaini ndani ya muda mfupi. Katika hali ya kushangaza matukio yanayofanywa na wasiojulikana badala ya kupungua, yamekuwa yakiongezeka kwa idadi na umadhubuti mpaka sasa yamekuwa ni janga la kitaifa.

Matukio ya mwanzo, kama lile la Mo Dewji, yalikuwa na sura ya kuviazia na kujifichaficha, lakini sasa hivi wasiojulikana hawavizii na kujificha tena, wanaweza wakasimamisha basi la abiria, eneo kama Tegeta ndani ya jiji la Dar es salaam, wakamshusha mtu kama mzee Kibao na kesho mkamkuta ametupwa akiwa marehemu.

Hebu fikira, kama makundi ya watu yanaweza kuchukuliwa ndani ya viunga vya mahakama maarufu kama Kisutu, tena ulinzi ukiwa umeimarishwa, wakapakiwa kwenye magari, na baadaye kukutwa Ununio na Mabwe pande wakiwa wamevunjika miguu, nawaliofanya hayo ukaambiwa ni watu wasiojulikana, Je ni mtanzania gani yupo salama mbele ya wasiojulikana?

Si ajabu sasa tunasikia Rev, Fr, Kitima ameshambuliwa na wasiojulikana ndani ya eneo la baraza la maaskofu kama ilivyokuwa kwa Tundu Lisu kupigwa risasi ndani ya makazi ya viongozi Dodoma. Kinachotisha zaidi ni kuwa, kama wasiojulikana wanaweza kutekeleza jaribio la mauaji ndani ya eneo lenye ulinzi la baraza la maaskofu, ikitokea wakiitaka roho ya mtu kama mm siitakuwa ni swala kuchinja kuku tu!

Tunasimuliwa humu mitandaoni kuwa Benny Saanane, Deusdedith Soka na hivi karibuni la Mdude Nyang'ali kuwa walikamatwa na watu wasiojulikana na hawajulikani walipo. Aidha jeshi la polisi katika taarifa zake rasmi, nalo limethibitisha kuwa watu hawa haijulikani walipo.

Kwa uzoefu tulioupata wa matukio ya watu wasiojulikana, ukisikia ndugu yako amekamatwa ni vyema mkaanza kuwatafuta vichakani, misituni na kwenye fukwe za bahari maana hayo ndio maeneo ambayo watu wasiojulikana hupenda kutelekeza miili ya watu waliowatesa au kuwaua.

Binafsi sitaki kuamini kama wasiojulikana ni mkono wa dola, ila Ikiwa sisi kama nchi tumeshindwa kuwajua na kuwadhibiti wasiojulikana basi ni vyema tuombe msaada kutoka kwa mataifa mengine yaje kutusaidia kuwatafuta na kuwadhibiti wasiojulikana ili tunusuru uhai wa watu wetu. Hatuwezi kuwa na nchi ambayo wasiojulikana wanaua na kuwatia vilema watu wetu halafu tunaizoea hali hiyo kana kwamba ni hali ya kawaida.

Uhai wa mtu ndio zawadi kubwa zaidi mtu aliyopewa na Mungu wake iwe baraka kwake na kwa familia yake. Mtu anapouawa, hapotezi marehemu tu, bali wazazi, watoto, mwenza na wategemezi wa huyo mtu wanapoteza pia. Nawasihi wasiojulikana kuwa na moyo wa huruma. Ikiwa sisi watanzania tumewakosea basi watusamehe, ili tuendelee kuishi maisha yetu kwa amani.
Wasiojulikana: Government of Tanzania - UVCCM -
OPerator: UVCCM Police
Model Of Operation: MAFIA
Boss: Amiri Jeshi MKuu - Don Carleone
Carlo Rizi: Mchengerwa
Sonny (Santino): Abdul
 
Back
Top Bottom