Turudi nyuma kidogo kutafuta ushahidi kwa serikali imekuwa ikipanga mikakati ya kuvuruga taarifa na elimu ya uraia inayokusudiwa kwenda kwa wanachi.
MCHAKATO MAJIMBONI:
Katika uchaguzi wa 2010 kipindi hiki kilichorushwa na TBC kilikuwa maarufu sana. Ccm chini ya Makamba ikapiga marufuku wagombea wake kushiriki, baada ya uchaguzi Tido Muhando alifukuzwa kazi na tangu siku hiyo TBC iliyokuwa maarufu ikwawa kipaza sauti cha Ccm na kufifia mpaka leo ni shida kukuta mtu anaangalia TBC.
MPANGO WA KUZUIA MATANGAZO YA BUNGE:
Baada ya Bunge la 10 kuwaka moto kutokana na hoja za wabunge wa upinzani, serikali ikaja na hoja ya kuzuia matangazo ya moja kwa moja ili yahaririwe kwanza. Watu wakapiga kelele sana kwamba mpango huo haukubaliki na wakauliza serikali inaficha nini. Kwa taarifa mpango huo haujafa maana bunge lina mpango wa kuanzisha Tv na Redio ili kurusha wanachotaka wao.
KUKATWA KWA MATANGAZO LISSU AKIWAKILISHA MAONI YA WACHACHE BMK:
Nadhani mnakumbuka TBC walivyokata matangazo Tundi Lissu akiwakilisha maoni BMK. Ukawa walikomaa mpaka bunge likahairshwa, kesho yake walilazimika kurusha upya hotuba ya Lissu baada ya mbinyo wa Ukawa.
KAULI YA SITTA BMK:
Baada ya iliyokuwa tume ya mabadiliko ya katiba kuendesha mdahalo wakati bunge likiendelea, Sitta alimtaka waziri wa habari Mkangara kufuatilia vyombo vinavyotoa muda wa hewani kueneza "uchochezi"!
Ukiunganisha ushaidi huu unapata jibu kwa malalamiko ya wananchi kwamba hata tukio la Warioba lilipangwa, ila kama kawaida yao walikosea kupanga maana hakukuwa na haja ya Makonda kuwasindikuza vijana wake kuja kufanya vurugu. Au labda Mungu alipanga kuwaumbua.