Serikali yetu tukufu imeruhusu Wanyonge kufanya biashara ya Umachinga holela na wasibughudhiwe wala kusumbuliwa na yeyete. Amini usiamni hiki ni kitanzi kwa Watanzania wapenda Ustaarabu.
Barabara za waenda kwa Miguu zimezibwa hivyo waenda kwa miguu wanapita njia ya Magari hatimaye kufyekea miguu yao na bodaboda.
Maeneo ya Shule za Serikali mahala pengine karibia kabisa na dirisha la darasa pamegeuka Soko la machinga (mfano mzuri ni pale Tabata Shule ya Msingi iliyo karibu na Dar West Club) Watoto usikivu umepotea madarasani. Huo ni mfano wa shule moja tu lkn hali ni mbaya sana karbia shule zote za maeneo ya Mijini.
Pale Mwanza ndio usiseme ile shule ya Sekondari imegeuzwa kuwa Stand ya Muda baada ya Nyegezi Stand kufungwa kwa muda, machinga wamevamia mpaka eneo la assemble. Inauma, inaudhi, inakera lkn ndio Kila Kiongozi anaogopa kutema kitumbua.
Upande wa Mitaro ya barabara ndio usiseme kabisaaa, yoooote inazibwa ili juuu yake Machinga ajenge kizimba chake kwa mwamvuli kwamba asiguswe wala kusumbuliwa na yeyote. Wauza embe, nanasi, miwa nk wametapakaa kila kona na wakimaliza biashara zao uchafu mwaaaa mitaroni. Sasa mitaro imejaaa na MAFURIKO yapo kila konaaaaa mvua ikinyesha. Mweeee Mhe. Rais katika hili hapana Kiongozi wangu tunataabika na kuharibu Miundombinu tuliyojenga kwa gharama kubwa.
Madhara ya ufanyaji biashara holela pia yamehatarisha wafanyabiashara wengine wakubwa kuathirika na kufunga biashara zao na kuinnyima serikali Mapato yaliyotokana na VAT nk, lkn pia Wataliii hawapendi kutembelea Nchi zisizokuwa na Mpangilio maalumu na hivyo kusababisha misongamano inayohatarisha nyendo zao wawapo kwenye eneo husika, aysee Kariakooo hapafai hata kwa dkk 1 machinga hao hao na vibaka hao haooooo katika hili Mhe. Makonda nakupongeza ingawa juhudi zako zilizimwa.
Kwa haya machache niishie kwa kusema wenye ushawishi kwa Mhe. Rais mwelezeni sasa imetosha hawa Machinga wametushika Shanga kiunoni na kalio ndio wanalipapasa kabisaaaa.(Madhara wanayosababisha hayalingani na elfu 20 ya Vitambulisho vyao).