"Sasa kwanini Bunge likatwe meno ya kuisimamia serikali..? Kwanini mhimili hii inaingiliana ??

Francis12

JF-Expert Member
Sep 30, 2016
7,533
22,276
Bunge la sasa linaathiriwa na vitu 3 vikubwa sana...

1. "Udhaifu wa kiti cha spika (spika, naibu spika, wenyeviti wa bunge)" ... wamekuwa ni watu wanaoendeshwa na matakwa, itikadi na mrengo yao kisiasa.. siyo kanuni na taratibu za uendeshaji wa Bunge letu...,

2. "Ushabiki wa kiitikadi wa vyama vya siasa" .. kila chama kikihitaji kuonyesha itikadi yake dhahiri.. na kuitetea hadharani.. ni hatari kutetea itikadi bungeni.., na hii inasababishwa na Taifa kutokuwa na itikadi maalum na kukosa agenda ya kitaifa.

3. "Wabunge wengi kutoka upande wa wabunge wa CCM wanaamini kuwa wabunge wa CHADEMA (chama kikuu cha upinzani nchini) na upinzani kwa ujumla wake ni maadui zao na siyo wapinzani".. wanasahau kuwa nchi yetu inaamini katika mfumo wa kidemokrasia wa vyama vingi.., wanasahau kwamba, kazi ya upinzani bungeni.. ni kuikosoa serikali na kuisimamia kuhakikisha nchi inakwenda kwenye mstari mnyoofu.

Bunge letu limekosa meno sasa.. ni dhahiri serikali imeweka safu yake ya uongozi katika mhimili huu mmojawapo wa dola..., Bunge lina kazi kubwa ya kuisimamia serikali.., sio kuishangilia serikali na kuwa "watetezi" wa serikali, hiyo sio kazi ya bunge, asilani-abadani..

Ni vipi sasa serikali itasimamiwa kama kila kitu kitakuwa ni "ndiyo mzee" na wabunge wamefungwa midomo?? Bunge kama mhimili unaojitegemea.. haupaswi kuingiliwa majukumu yake na mhimili mwingine.. Kazi ya Bunge ni;

》Kutunga Sheria.
》Kuisimamia serikali.
》Kuwawakilisha wananchi.

Sasa kwanini Bunge likatwe meno ya kuisimamia serikali..? Kwanini mhimili hii inaingiliana katika utendaji na kupangiana majukumu?? Wananchi "watawakilishwa" vipi kama tu bunge litakosa namna ya kutenda kwa uwazi, ukweli na dhima ya dhati ya uwajibikaji!?
 
Ushabiki wa kiitikadi wa vyama vya siasa" .. kila chama kikihitaji kuonyesha itikadi yake dhahiri.. na kuitetea hadharani.. ni hatari kutetea itikadi bungeni.., na hii inasababishwa na Taifa kutokuwa na itikadi maalum na kukosa agenda ya kitaifa.
 
Bunge linaendeshwa kwa maelekezo kutoka Ikulu.Wabunge wa CCM walivyokuwa kwao chama kwanza maslahi ya pembeni
 
Back
Top Bottom