Unao uhakika? Au unaropoka tu. Tena bora ungechangia na si kuanzisha mada ambayo hauna uhakika hata chembe. Acha kupotosha umma kwa mambo ya udaku na kufikirika. Hujui lolote kuhusu unachoongea
Sijakupata vizuri...Mkandala akatae kuyapitisha? Anajipenda? Itabidi ajiulize mara mbilimbili kama alistahili kuwa VC wa UD kabla hajaanza kuiletea zengwe serikali. Analijua hili vizuri na hawezi kujifanya hamnazo!Katika kile kinachoonekana kama kufanikisha mipango ya kuyaidhinisha kwa lazima Matokeo mapya ya Kidato cha Nne,Serikali imedhamiria kutumia ipasavyo nafasi ya kutokuwepo kwa Prof .Rwekaza Mukandala kuyapitisha.
Prof.Mukandala ,ambaye ni Mwenyekiti wa NECTA na Makamu Mkuu wa UDSM, hayuko nchini kwasasa.Taarifa rasmi zinaoonesha kuwa Prof.Mukandala yuko nchini Marekani kuhudhuria Mahafali ya mtoto wake ambaye anahitimu katika chuo kimojawapo nchini humo.
Huku yeye akitarajiwa kurejea nchini mwishoni mwa juma lijalo,Serikali imeapa kuyapitisha na kuyaidhinisha matokeo hayo bila ya uwepo wa Mwenyekiti wa NECTA. Yuko kigogo mmoja wa NECTA ambaye amepangwa kukaimu Uenyekiti wa NECTA kwa ajili ya kupitisha matokeo hayo mapya tu.
Prof.Mukandala,akiungwa mkono na Katibu Mtendaji waNECTA,Dr.Joyce Ndalichako,tangu mwanzo wa mchakato wanapinga kusahihishwa au hata kupangwa upya kwa Matokeo ya Kidato IV-2012 kwa kile wanachosema kuwa Serikali ilishiriki kuyaidhinisha ya mara ya kwanza na hivyo haiwezi kuyabadili.
Katika siku za hivi karibuni,kumekuwa na mvutano mkali kati ya Maafisa Waandamizi wa NECTA na wale wa Serikali juu ya upangwaji upya wa matokeo hayo. Serikali inasisitiza kuwa matokeo hayo lazima yabadilishwe ili kukidhi haja ya Taifa kupata elimu bora.
Mengi yatajitokeza na mtayajua waungwana wote wa Tanzania!
Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
Hujaifahamu hoja yangu! Hata kama serikali na NECTA walikaa na kukubaliana, hoja ya msingi ni kwamba haikuwa sahihi! Katika lugha ya "sikubali sikubali" ni kwamba walichofanya serikali ni kula matapishi yao lakini lugha ya kiungwana, walichofanya serikali ni kukubali udhaifu wao na kukiri kwamba walipotoka na hivyo hawana budi kurudi nyuma! Haingii akilini hata kidogo mnabadilisha GRADING kinyemela wakati watu washafanya mitihani huku hata walimu wenyewe hawafahamu kwamba grading imebadilishwa!Hili jambo linawagusa wanafunzi moja kwa moja na sio NECTA! Ukidai kwamba yaliyosemwa mengi ama sikuyasikia au sikutaka kuyatilia maanani niseme tu kwamba u're wrong; nilichoeleza kinaokana na yaliyosemwa na kuandikwa tangu sakata hili lianze....hii sio post yangu ya kwanza; nd am very sure haitakuwa ya mwisho!Nadhani kuna mengi yaliyosemwa ambayo bila shaka hukuyasikia au hutaki kuyatilia maanani. Maelezo yako ni kana kwamba kilichofanywa na NECTA ilikuwa ni maamuzi yao wenyewe.
Utaratibu waliotumia kupanga matokeo ilikuwa ni baada ya michakato iliyoendeshwa na serikali chini ya waziri wa elimu na katibu akiwa Mulugo, na hatimaye wakatoa maagizo rasmi kwa NECTA juu ya utaratibu wa kupanga matokeo.
Sasa cha ajabu watu wale wale waliotoa maagizo ya awali wanakuja na maagizo mapya yanayoashiria kupinga maagizo yao ya awali, kweli hapo utaendelea kutupa lawama kwa NECTA?
Cha ajabu kinachonishangaza, Tume iliyoundwa inaongozwa na mtu ambaye alikuwa mjumbe kwenye kikao kilichoamua kubadilisha utaratibu wa upangaji wa matokeo hayo, leo anakuja na fikra mpya ya kutengua wazo lao la awali. Nadhani haikuwa sahihi Tume kuwa chini ya aliyeshiriki kwenye kutengeneza huo utaratibu