Sarafu ya sh 500 haina ubora!

Inawezekana ikawa kweli sarafu hizo zimetoka lakini bado hata haziko kwenye mzunguko. Swali linakuja mtoa mada amewezaje kujua hizi sarafu hazina ubora, ni za chuma ila zina layer ndogo ya fedha, alizichuna au alijuaje hebu funguka ututoe shaka!
 
Shukrani sana kwa somo hili adhimu. Mwenye akili, macho na masikio na aelewe hili. Keep them coming!
 
Hebu tulieni, tukishaanza kuzitumia tutajua. Acha kutulisha matango pori
 
Inawezekana ikawa kweli sarafu hizo zimetoka lakini bado hata haziko kwenye mzunguko. Swali linakuja mtoa mada amewezaje kujua hizi sarafu hazina ubora, ni za chuma ila zina layer ndogo ya fedha, alizichuna au alijuaje hebu funguka ututoe shaka!

Mkuu, huhitaji kuwa na hiyo sarafu ndio ujue ubovu wake. Ukiambiwa muundo wake waweza kutumia common sense ukagundua kwamba hizo sarafu ni kanyaboya.
 
Hebu tulieni, tukishaanza kuzitumia tutajua. Acha kutulisha matango pori

Wewe mwenyewe ndio una akili za kitango pori. Unahitaji elimu gani kujua kwamba madini ya chuma yakipambana na oksijeni hutoa kutu? Au hujui kwamba sarafu hizo zimetengenezwa kwa madini ya chuma? Acha upotoshaji mkuu.
 
Yaani hasiraaa afu sina la kufanya. Inauma sana
 

aiseee ubarikiwe na bwana
 
No No No mie niwaulize hivi kwanini hizi coin zinapoteza thamani haraka,mfano hakuna karanga ya 50.pia hakuna chungwa ya 100!...wataalam tuelezeni vizuri sio kuwa thamani ya pesa yetu kwisha habari?

Kwa uzoefu wangu mdogo nilionao, kila inapobadilishwa noti kuwa sarafu basi thamani ya shilingi hushuka. mfano kumbuka tu toka siku za nyuma ukianzia na ile noti ya mia ilikuwa na nguvu sana, ikaja sh 50, 20 na noti ya sh 10. kila thamani ya Tsh iliposhuka, nafasi ya noti ilichukuliwa na sarafu na noti kupandishwa, ndogo toka sh 10 kuwa 20, 50, 100 mpaka 500. Baadaye mabadiliko yaliendelea na noti ya juu zaidi kuwa sh 10,000 ambayo tumedumu nayo kwa muda mrefu.
 
Why ,one year before or after g election . Hii biashara huwa ina take place.
Wanaingiza pesa kwenye mzunguko bila kutoa.., wanaleta inflation na kuongeza ugumu wa maisha. wanachofanya hapa ni kuziba pengo lililosababishwa na laxity kwenye ukusanyaji kodi.
 

Kweli kabisa mkuu, na tutashuhudia ugumu wa maisha ukiongezeka mara dufu. MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA sasa yatakuwa bora zaidi.
 
mbona unaweweseka? wewe unadhani ni nani wa kulaumiwa wakati yeye ndiye kiongozi mkuu wa nchi? unadhani BoT walifyatua hizo sarafu feki bila kumshirikisha mkuu wa nchi?
unanichekesha siyo kila kitu unamlaum mkuu wa nchi wanaweza wakampa, idea akakubali but wanakotengeneza hawezi kujua wanatengenezaje ni sawa na mzazi mwenye malezi mazuri na mwanaye akiwa nyumbani anakuwa okey akirudi shule ana imitate mob psychology anaharibikiwa mpaka mzazi anashangaa mi nadhani wa kulaumiwa ni bot
 
Sidhani kama Kikwete anahusika hapa.
Anahusika mkuu, nyie mnataka ahusike moja kwa kwa moja, lakini kwa kusamehe mambo kama yale ya EPA, RICHMOND, N.K. huoni anawapa confidence mafisadi? Zamani enzi za mwl. ungesikis Rais amekasirika na kumwachisha kazi mtu, huyu mbona hajawahi kukasirika?
 

Mkuu, naona unajaribu kumtetea Rais wako....unakumbuka jinsi alivyowasamehe wezi wa EPA? Ni kosa la nani hilo? Tena wakampa bilion 33 akazitia mfukoni mwake?

Usishangae na hawa matutusa wa BoT huenda ameishawasamehe kwa uamuzi wao huu wa kiuendawazimu.
 

CC: maisha na pesa
 
Last edited by a moderator:
Noti hazikuwa na ubora sasa na hizi sarafu nazo zinategemewa kuwa hivyo. Tusiojua tusubiri tuone itakuwaje zikitoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…