Ni ngumu sana kuripoti taarifa za kiuchumi....., kwa kweli sijakuelewa. Kwa mbali nimeelewa hivi, sarafu ya Africa kusini (RAND) imeshuka hadi kufikia RAND 14 kwa USD1, hii ni kutokana na mdororo wa ukuaji wa uchumi wa taifa la china uliosabisha wawekezaji kuuza mali zao. Sijui kama nimekupata sawia: Maswali ni haya
Wawekezaji hao wapo china au south africa? kama wapo china mbona sioni direct link? China wameshusha dhamani ya hela yao kwa makusudi, hii inaweza athiri mataifa mengi duniani, lakini kwa nini iwe zaidi south africa? Inategemewa hata US na Europe zitaathirika kwa viwango tofauti (sababu zipo).
Ushauri, weka source ili tupate taarifa kamili kutoka kwa waandishi wa habari za kiuchumi.