Sarafu bandia za 200 ni dili la nani hili?

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,634
697,845
Tumezoea kuona ama kusikia noti bandia lakini si sarafu bandia.. Kwa sehemu kubwa sana noti bandia zimedhibitiwa japo ni biashara inayoenda na kurejea kila wakati

Sasa naona hawa wenye hii biashara yao wamepunguza kwenye noti na kuhamia kwenye sarafu..Pengine kutokana na sababu kadhaa
1. Noti banda ni rahisi sana kutambulika hata kwa mtu asiye mzoefu sana lakini sarafu ni ngumu mpaka inapoanza kuchakaa

2. Ufuatuliaji was noti bandia ni mkubwa kuliko sarafu bandia

3. Alama za usalama kwenye noti ni nyingi kuliko kwenye sarafu

4. Mzunguko wa noti sio mkubwa kama wa sarafu ambazo unaweza kuzizungusha mpaka mtaani uswahilini kabisa..

Kuna hawa wauza chenchi ni vema biashara hii ikafuatiliwa kwakuwa inawezekana nyuma ya pazia wanaweza wakawa wanatumika kusambaza sarafu bandia
Kuna hawa wachezesha kamari za kamari za sarafu ambao kwa maramoja unaweza kuwakuta mpaka na sarafu za shilingi milion 3 ama zaidi.. Hawa huwa na nyaraka za bank kuu wanakoenda kuchukua chenchi lakini je haiwezekani wakawa wanazichanganya na za kwao bandia?

Hawa hata uwakute na mzigo mkubwa wa chenchi huwezi kuwachukulia hatua kwakuwa wana vibali na nyaraka toka mamlaka husika.. Lakini je ni nani anahakiki walizonazo ndio kiwango walichopewa bank kuu?

Kuna uwezekano mkubwa huko kwenye kamari za sarafu ndii mlango wa kupitishia sarafu bandia na kuziingiza kwenye mzunguko.... Hili lifanyiwe kazi

Nawakilisha! 2023
20230401_092051.jpg
 
Nawakilisha ikiwa leo ni siku ya wajinga duniani tarehe 1, April 2023View attachment 2572735
Hujaeleweka upo kwenye April fool au ni kweli hiyo habari uliyoleta?

Uwasilishaji wako hauendani na April fool, ni story IPO kiuhalisia kabisa.
 
Sasa mtu atengeneze tshs 200 ya bandia - material ya kutengeneza Kuna faida yoyote atapata kweli? Nafikiri ni Yale madubu michezo ya kichina ndo inaharibu hizo coin
Material bandia na yasiyo na ubora takikana yapo
 
Pamoja na kusababisha upungufu mkubwa wa sarafu kwenye mzunguko wa fedha na pia kusababisha uchakavu mkubwa wa sarafu zenyewe hivyo kuongeza gharama za kubadilisha sarafu. Sarafu badala ya kutumika zimejaa ndani ya mashine za kamari na Meza za pool table.

Serikali kupitia benki kuu iwaagize hawa wamiliki wa mashine za kamari na pool table kutengeneza token maalum zitakazonunuliwa kwa fedha taslimu siyo lazima sarafu na atakayeshinda kamari awe na uwezo wa kubadili hizo token kuwa fedha.
 
Kiuhalisia huwezi kutengeneza sarafu fake ya 200,gharama halisi yahiyo sarafu ni zaidi ya hapo,hata noti ya 2000 fake kuitengeneza ni gharamw zaidi ya hicho kiwango
 
Kama watu wanaweza kutengeneza madini feki sidhani kama hili linashindikana
 
Back
Top Bottom