Biashara ya fedha za zamani kulikoni?

Filosofia ya Rorya

JF-Expert Member
Sep 20, 2021
3,214
3,587
Wenye taaluma ya Fedha humu tunaomba maarifa toka kwenu kuhusu uhalali kisheria wa kuchuuza sarafu na noti za zamani.

Wachuuzi wanazo leseni za hizi benki/bureau dechange za pembezoni mwa barabara?

Kama hawana je, sheria za nchi zinawataka kurasimisha hiyo biashara kwa kuwa na leseni?

Kama uchuuzi huu siyo halali kisheria je, benki zinaruhusiwa kuwapa hizi ela?

Je, wanazitoa wapi?

Je, bado ziko kwenye mzunguko kwamba hazikurudishwa benki zote?

Je, sarafu na noti za zamani zikiondolewa kwenye soko la fedha na soko la mitaji huwa zinatunzwa benki kuu au zinaharibiwa?

Je, yawezekana wachuuzi hawa kama hawazipewi na benki zinazozihodhi yawezekana wanazipata kwa watu wanaochapisha ela bandia?
 
Mbona umeandika sana??

Kama mada yako inatokana na lile tangazo lisemalo 'ninanunua pesa mbovu na pesa za kigeni nanunua";

Ni hivi, wale ni matapeli!

Ukimuuzia noti au pesa za kigeni, let say kw bei ya 9,000/= kwa kila noti, anachukua namba yako ya simu Kisha anaondoka.

Akifika, ile namba anampa tapeli mwenzake kwa hiyo namba yako inajulikana na A na B.

The A anapiga simu kwamba anahitaji pesa mbovu let say kila noti ya elfu kumi mbovu atanunua kwa elfu 20, na anahitaji noti 100.

Wewe utapagawa kwamba noti 100x20,000=2,000,000. So utapataje noti 100?

Ghafla B (tapeli wa pili) anapiga simu kwamba anazo noti 100 na mnaelewana bei let say 100X15,000=1,500,000, baadaye A anakuambia uongeze 100 tena ziwe 200.

Na wewe unampigia B kwamba aongeze 100 then unatafuta hela hata kwa kukopa then hesabu inakuwa hivi mfano utanunua noti 200x15,000=3,000,000 toka kwa B tapeli, kwa lengo la kuuza kwa A (tapeli) kwa bei ya 4,000,000 then faida ni 1m.

Sasa basi, ukishampatia B hiyo milioni 3 na anakupatia noti mbovu ama hakupi (whatever), wote A na B wanakublock kwenye simu na huwapati tena maana kwa pamoja wameshakuuzia noti mbovu 200 za elfu 10,000 kwa bei ya 15,000 kila moja na umewapatia 3,000,000/=.
 
Back
Top Bottom