Hapo tulipofika si haba Mahmoud Qassim.Juhudi zote zilizofanywa na kila mmoja wetu zimetufikisha hapa.Kama tuaendelea na kufika tunakotaka kufika ni bora kwetu sote,Maximo akwemo ndani.
Katika uchambuzi mwingi wengi wetu tumesahu kuwa Brazil ni nchi inayoheshimika kwa soka na imechukua kombe la dunia mara nyingi.Sikumbuki mahali mabapo kocha wa Brazil alikuwa foreigner!
Je tungempa Charles Boniface Mkwasa timu hii angeweza kutufikisha hapo tulipofika? I doubt kwa sababu kuna tofauti kati ya Mkwasa na Maximo! That's what makes the difference!Hii ni pamoja na all the support rendered!JK hakuwa na mawazo ya Mkwasa wala Mziray kwa sababu alijua what the team needed most.
Hata kama tutafungwa au kufunga leo hii kauli yangu ni hii,kwamba tumejitahidi na tumefanya vizuri kwa sababu tuna Coach mzuri plus the support of the whole nation.
Ama kweli waTanzania ni hodari kwa kupenda maendeleo ya haraka bila ya kuwekeza. Hivi kweli mnaweza kumlaumu Maximo kwa haya maendeleo "madogo" tuliyonayo kwenye soka?
Unapolinganisha soka ya Tanzania na ulaya hautendi haki. Ulaya wenzenu wanaanza kupikwa toka wakiwa wadogo. Kuna shule kibao za soka ambazo zinawafundisha watoto. Hao akina lampard, Torres na wakali wengineo wamepikwa kisoka toka wakiwa wadogo. Hebu angalia hapa TZ nini kinaendelea. Watu mpira wanafundishwa "ukubwani". Wakiwa wadogo na hata mchangani wanacheza mpira wakufundishwa na "kocha mbabaishaji" tu. Unategemea mtu kama huyo hata akikuwa atajua soka kweli?
Tufike mahala tukubali kuwa ili kuwa na timu nzuri basi inabidi kwanza mfumo wa soka ubadilike. Timu zianze kutengenezwa toka za watoto. Wapate makocha wenye taaluma ya ukocha wawajengee misingi mizuri then wakiwa wakubwa matunda yao yataonekana.
UBORA WA NYUMBA UNATEGEMEA MSINGI WAKE
Kweli kuwa MAXIMO anapenda fomesheni ya ku-defence zaidi
Hata akiondoka na hao jamaa waache kuvuta bangi bila hivyo hata aikja kocha gani mambo ni yaleyale
I think Maximo should go now...Tunahitaji ujuzi wa Kocha mwingine,hasa kutoka Ufaransa,makocha wa kifaransa wana uzoefu sana na soka la Afrika,pia watatusaidia kuwauza wachezaji wetu Ufaransa,otherwise daima tutakuwa wasindikizaji tu huku tukijisifia tumecheza vizuri(ilhali tumetolewa)....Hivi mkataba wake unaisha lini????
Una ushahidi wanavuta bangi?
Kuwa soccer analyst sio lazima uende shule ya soka ni kama vile kuwa Kocha wa soka si lazima uwe ulicheza mpira zamani ingawa kuna faida ya kukijua kitu ndani nje.
Maximo ni kocha mzuri, na ametufikisha sehemu nzuri tunakubali. Lakini je, tunapenda haya mafanikio nusunusu?
Hivi nyie mnaosema Maximo aendelee, huwa mnakwenda kuiona Taifa stars ikicheza uwanja wa Taifa au hata kuiona kwenye TV?
Uwezo wa Maximo tuuangalie zaidi kwa mbinu za wachezaji uwanjani. Kwakweli uwezo wa timu yetu kubadilisha mchezo uwanjani ni mdogo mno na hilo ni jukumu la Kocha. Kocha huyu, mbrazili Marcio Maximo ameshindwa kabisa. Kumbukeni kwenye mechi yetu ya CAN qualifying dhidi ya Mauritius. Jamaa wa Mauritius hawakuwa na uwezo wowote uwanjani nasi tulikosa mbinu za kuwafunga licha ya kuhemea lango lao na kupata kona zaidi ya 17. yaani hatukuweza kubadilisha mchezo na tukaishia kwa sare pale national stadium. Licha ya wao kucheza pungufu ya mtu mmoja kwa muda mwingi wa mchezo.
Maximo ameshindwa kutengeneza nguvu ya timu pale tunapopata goli kabla ya wapinzani wetu hakika hatuwezi kulinda goli kabisa. Na hilo ni jukumu la kocha. Kumbuka mechi kati ya Taifa Stars na Senegal pale Kirumba Mwanza(1:1); Taifa stars na Cameroun pale Yaounde (1:2), lile bao la pili la Cameroun ni upuzi mtupu. Taifa Stars na Ghana hapa Dar(1:1), na sasa Taifa stars dhidi ya Zambia(1:1). Hiyo ni kazi ya kocha ambayo ameshindwa kuifanya kwa muda mrefu kabisa. Timu haiwezi kulinda bao chini ya ukocha wake.
Mafanikio haya tunayoyaona ni mafanikio ya kimorari. Watanzania tuna Morari na wachezaji pia. Kipindi hiki cha Maximo, timu inapata kila kitu fedha, muda, vifaa vya mazoezi n.k. Hivi mnakumbuka Kocha Zakaria kinanda au Mshindo Msolwa walikuwa wanapewa timu wiki moja kabla ya mashindano? Mnakumbuka wachezaji wa taifa kambi yao ilikuwa jeshi la Wokovu pale Kurasini? Hakukuwa na Morari kabisa.
Hivyo kwa sapoti hii anayopewa Maximo akipewa Kocha kama King Kibadeni au Mziray anaweza kufanya makubwa zaidi. Maximo na aondoke tu!!! Hana jipya, uwezo wake umefikia kikomo.
Kumbukeni Simba ilipokuwa na sapoti ilifika fainali kombe la CAF (1993) chini ya kocha mzalendo.
Tunahitaji kocha mpya Tanzania ambaye ataanzia pale Maximo alipoishia.