Sanda yangu nilishaandaa siku nyingi

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
ALLY Salum [48] anayedaiwa kuwa fundi ujenzi mkazi wa Yombo Buza, amekufa baada ya kujinyonga kwa kutumia kamba ya mkonge kutokana na kuzidiwa na wivu wa mapenzi .
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, David Misime alisema kuwa marehemu huyo alikutwa amekufa juzi, majira ya saa 8.00 mchana nyumbani kwake.
Alisme Ally kabla hajachukua uamuzi wa kujinyonga aliacha ujumbe maalum uliofanya ajinyonge yeye mwenyewe.

Alisema ujumbe huo ulionyesha dhahiri kuudhiwa na mke wake baada ya kuona mabadiliko yakitabia juu yake

Ujumbe aliouacha ulisomeka , “nimeamua kujinyonga kwa hiyari yangu kutokana na mke wangu kushauriwa na mama Salehe kutoka nje ya ndoa, hivyo namuachia ukumboi aendelee na hizo starehe zake, ila naomba mke wangu asibughudhiwe.

“Mali nilizochuma naye zibaki mikononi mwake, asinyang’anywe na mtu yeyote wala ndugu yangu yoyote, napenda kuwajulisha nilikuwa na mke mwingine mdogo yupo maeneo ya Kimbiji Kigamboni, Sanda yangu nilishaandaa siku nyingi ipo kwenye sanduku,” ulieleza ujumbe huo.

Polisi wanaendelea na upelelezi huku maiti imehifadhiwa hospitali yaTemeke.

Katika tukio jingine, MTOTO wa kike [1] ameokotwa akiwa hai na wapita njia huko maeneo ya Yombo Vituka jijini Dar es Salaam.

Mtoto huyo alitupwa na mtu asiyejulikana na wasamalia wema waliopita eneo hilo walimuona na kumuokotwa nakumkuta akiwa hai

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Bw. David Misime, ilisema kuwa mtoto huyo aliokotwa juzi majira ya saa 2.15 usiku.

Alisema mtoto huyo alikutwa akiwa amefungwa na kufunikwa na kitenge na kulazwa katika njia hiyo.

Taarifa ilipoifikia polisi mtoto huyo amechukuliwa na amehifadhiwa katika Hospitali ya Temeke kwa uangalizi zaidi.
 
angalieni hiyo barua asiwe ameandika mke wa marehem!

imekaa kimaslahi zaidi hii barua. Watalaamu wa mwandiko wachunguze uskute mke kaingia dili na wauaji wakamtundika marehemu as if kajinyonga mwenyewe na kujiandikia huo ujumbe. Dunia imeharibika sana.

RIP Salum.
 
yaah ni kweli sasa hv kila mbongo akili imechangamka!
imekaa kimaslahi zaidi hii barua. Watalaamu wa mwandiko wachunguze uskute mke kaingia dili na wauaji wakamtundika marehemu as if kajinyonga mwenyewe na kujiandikia huo ujumbe. Dunia imeharibika sana.

RIP Salum.
 
angalieni hiyo barua asiwe ameandika mke wa marehem!

...of course barua imekaa kimtego sana. Mume mwerevu ambaye anamtuhumu mkewe kutoka nje ya ndoa asingeruhusu mali zake zitumike kuhonga wanaume wengine na kutoa wasia kwamba mali akabidhiwe mkewe! Ila hilo la sanda ndio limeniacha hoi sana. Alijiandalia mapema sana.
 
nimeshawahi shuhudia mzee mmoja pale songea alijitengenezea jeneza akaliweka chumbani kwake!
...of course barua imekaa kimtego sana. Mume mwerevu ambaye anamtuhumu mkewe kutoka nje ya ndoa asingeruhusu mali zake zitumike kuhonga wanaume wengine na kutoa wasia kwamba mali akabidhiwe mkewe! Ila hilo la sanda ndio limeniacha hoi sana. Alijiandalia mapema sana.
 
ukitaka kupima uthamani wa mtu kwa sasa angalia kule loliondo kwa babu mtu analetwa yupo hoi hajiwezi mpaka anafariki watu hawataki kupisha foleni kisa tu wanataka kuwahi wakati mwenzao anapoteza maisha tanzania ya sasa kila mtu anajiangalia mwenyewe
Kama ndiyo hivi basi kazi ipo kweli kweli maana thamani ya mtu siku hizi haipo kabisa!.
 
Back
Top Bottom