Sanchez akataa kupanda ndege kwenda kuongea na city | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sanchez akataa kupanda ndege kwenda kuongea na city

Discussion in 'Sports' started by Dj Khalid, Jun 23, 2011.

 1. Dj Khalid

  Dj Khalid Member

  #1
  Jun 23, 2011
  Joined: Mar 3, 2010
  Messages: 54
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  [​IMG]

  Alexis Sanchez ameipiga chini Manchester City baada ya kukataa kupanda ndege kwenda kufanya mazungumzo ya kujiunga na Matajiri wa Premier League kwa dili lenye thamani ya £30 million.
  Superstar huyo kutoka Chile ambaye kwa sasa yupo katika kambi ya timu ya taifa inayojiandaa na michuano ya Copa America alipewa ruhusa na klabu yake ya Udinese kwenda jijini Manchester kufanya mazungumzo na City baada ya timu hiyo inayomilikiwa na matajiri wa kiarabu kuwashinda Man United na Barcelona.
  Lakini Sanchez baada ya kuambiwa na klabu yake aliwaambia City sio chaguo lake hivyo ajiunge na United au aongee na Barca kujua mipango yao.
  Tukio la Sanchez kuikataa City lilitokea katika uwanja wa ndege wa Santiago ambapo waandishi wa habari walikuwa wamekusanyika kuangalia Sanchez akipanda ndege kuelekea England, lakini walikuja kugundua mchezaji amekataa kwenda uwanja wa ndege kuelekea Eastlands.
  Sanchez alidhani kuwa anakwenda kuzungumza na mabingwa wa ulaya Barcelona, lakini ofa ya Barca ambayo ilihusishwa kutolewa kwa mchezaji Jeffren ilikataliwa na Udinese ambao waliamua kuichangamkia ofa nzuri ya City.
  Kwa sasa usajili wa winga huyo ambaye ameamua kuingilia suala la usajili wake, upo wazi zaidi kwa vilabu vya United na Barca kupigania saini ya mchezaji huyo.
  Inasemekana kuwa Barca walikuwa wanataka kutoa £22 million na kutoa mchezaji mmoja kati ya Bjoan Krkicc, Thiago Alcantara na Jeffren ambao wote walikataa kujiunga na Udinese.
  Man United ambao wenyewe walitoa ofa ya £27 million cash, sasa wanapewa nafasi kubwa ya kushinda vita ya kumsaini winga huyo kutoka Chile.
   
Loading...