Sanaa ya Vita (Art of war)

justin mwanshinga

Senior Member
May 22, 2014
179
619
The art of war (sanaa ya vita)

Maisha ni vita, mapambano yoyote ni kama vita.

Kumbuka kuwa:
1. Ushindi mkubwa ni ule ambao hauitaji vita yoyote.

2. Wapiganaji wanaoshinda wanashinda kwanza halafu waende vitani, wakati mashujaa walioshindwa wanaenda vitani kwanza na kisha wanatafuta kushinda

3. Ikiwa unajua adui na unajijua mwenyewe, hauitaji kuogopa matokeo ya vita mia. Ikiwa unajijua mwenyewe lakini sio adui, kwa kila ushindi uliopatikana pia utapata kushindwa. Ikiwa humjui adui wala wewe mwenyewe, utashindwa katika kila vita.

4. Katikati ya machafuko, pia kuna fursa .

5. Anayetaka kupigana lazima ahesabu kwanza gharama.

6. Hakuna noti zaidi ya tano za muziki, lakini mchanganyiko wa hizi tano husababisha sauti zaidi kuliko inavyoweza kusikika.

7. Vita vyote vinategemea udanganyifu.

8. Ni rahisi kumpenda rafiki, lakini muda mwingine somo gumu kulisoma ni kumpenda adui.

9. Hasira inaweza kubadilika kwa wakati kuwa furaha ... Lakini ufalme ambao umewahi kuharibiwa hauwezi kutokea tena.

10. Fursa huzidisha kadri zinavyokamatwa.

Hiki ni kitabu chenye maarifa, mbinu, hila na mikakati ya kivita (waweza apply kimapenzi, kimaisha ya kawaida n.k) kinachosemekana kuwa kiliandikwa na mbobezi wa mbinu za kivita nchini China “Sun Tzu” karne ya tano B.C.

Kitabu hiki kina sura 13, kila sura ikiwa mahsusi kwa ajili ya kipengele cha kivita. Sura hizi zimetafsiriwa na watu tofauti hivyo kuwa na vichwa kadha wa kadha. Hapa kuna maneno yanayoshabihiana kwa ukaribu na kujumuisha tafsiri tofauti.

Kabla ya kuanza, fahamu Sun Tzu alikua kamanda wa namna gani?.

Katika karne ya nne Sun Tzu alikua Jenerali katika kipindi cha vita (472–221 BC) nchini China. Kipindi hiki vita vilikua kila kukicha kupigania sehemu na mali za falme ya Chou (Chou Empire) iliyoanguka. Kiongozi mmoja alimkebehi Sun Tzu atumie mbinu zake kufundisha wanawake 180 kuunda jeshi lenye nidhamu. Kati ya wanawake hawa 180, kulikuwa na suria (concubines) wawili wa kiongozi huyo.

Sun Tzu akawagawa wanawake hao 180, na kuweka Suria kama kiongozi wa kila kikundi. Sun Tzu kisha akaamrisha zoezi jepesi na kuhakikisha wameelewa cha kufanya. Hata hivyo, alivyoamuru zoezi kuanza, wanawake hao wakaanguka kwa kicheko. Akasema, kushindwa kufuata amri mara ya kwanza inawezekana kuwa maelezo aliyoyatoa hayakueleweka vyema, hivyo atarudia. Akajaribu tena, matokeo yakawa yale yale, kicheko.

Sun Tzu akasema, kushindwa kufuata amri kwa vikundi hivi kwa mara ya pili ni kosa la makamanda wao, kisha akaamuru kukatwa vichwa “suria” wale wawili kama mfano kwa wengine. Baada ya hapo wanawake wale wote walifuata amri kama walivyoamrishwa bila chembe ya cheko wala kebehi.

Sura zake ni kama ifuatavyo;

Sura 1: Detailed Assessment & Planning
Sura hii inatazama mambo makuu matano (njia, misimu, ardhi ya eneo, uongozi na usimamizi). Kwa kuelewa na kufuata mambo haya kamanda anaweza kujua nafasi ya ushindi. Kushindwa kuelewa na kufata haya kutasababisha kushindwa. Kitabu kinasisitiza kuwa vita si jambo dogo kwa taifa, hutakiwi kuanza bila kufikiri kwa kina. Fikiri kwa kina, elewa tatizo kwa mapana. Kufeli kupanga, ni kupanga kufeli.

Sura 2: Waging War
Sura hii inaeleza umuhimu wa kushinda vita haraka na kwa kuhakikisha gharama za vita ni ndogo ili kuepusha kudorora kwa uchumi. Kushinda vita lazima uwe na rasilimali za kutosha, kama ni biashara basi uwe na mtaji wa kutosha. Usirefushe mambo, shinda vita mapema, vita virefu ni gharama na hupunguza motisha na kuongeza hatari ya kufanya makosa. Ikiwezekana kumshinda adui bila kupigana ni vema zaidi. Katika vita pongeza wapiganaji wako, katika biashara jali wafanyakazi wako. Hakikisha kila mtu anaona faida katika mapambano.

Sura 3: Offensive/Attack Strategy
Hii inaeleza kwamba chanzo cha nguvu sio “ukubwa” bali “Umoja” wa jeshi husika na mambo makuu matano yanahakikisha ushindi ni pamoja na “kushambulia, mkakati, ushirikiano, jeshi na miji”. Vuruga mipango ya adui yako. Hakikisha adui hapati mwanya wa kuunganisha nguvu na makundi mengine. Kumshinda adui bila kupigana ni vyema Zaidi.

Sura 4: Military Tactical Disposition
Hii inaeleza umuhimu wa kulinda ngome uliyopo mpaka pale unapoweza kusonga mbele kutoka hapo ulipo kwa usalama. Inafundisha umuhimu wa kuelewa fursa za kimkakati “strategic opportunities” na kutokutoa fursa kwa adui. Kuwa makini na makosa ya adui, hiyo ndiyo mianya kwako ya kushinda kwa nguvu ndogo na gharama kidogo.

Sura 5: Strategic Military Power/Force
Inaeleza umuhimu wa muda na ubunifu katika kujenga kasi na nguvu ya jeshi uendapo vitani. Tumia nguvu kadiri uwezavyo kushinda. Ubunifu lazima uendane na mazingira halisi na kutumika sambamba na mbinu za uhakika.

Sura 6: Weak Points and Strong
Hii inaeleza ni kwa namna gani nafasi ya jeshi lako inatokana na mwanya katika mazingira yanayosababishwa na udhaifu wa adui. Shambulia wakati na mahala ambapo adui yako hayuko tayari, ama hategemei shambulizi na hana nafasi ya kujitetea. Linda ngome ambazo haziwezi kushambuliwa na shambulia ngome ambazo hazina ulinzi ama ni ngumu kulindwa. Kuwa wa kwanza kushambulia. Kuwa na mikakati mbadala. Jifunze kumshitukiza adui.

Sura 7: Military Combat Manoeuvres
Inaeleza hatari za mapambano ya ana kwa ana na namna ya kushinda mapambano haya unapokutana nayo. Mlaghai adui yako. Wasiliana na toa maelezo yanayoeleweka kwa wapiganaji wako.

Sura 8: Nine-Tactics Variation and Adaptability
Inaeleza umuhimu wa kuwa “flexible” katika mbinu zako unapopambana na adui. Pia Inaeleza jinsi ya kuendana na mazingira yanayobadilika.

Sura 9: Army on the March
Inaeleza hali tofauti unapozuru ardhi ya adui yako na namna ya kukabiliana na wakati huu. Inaangalia pia namna ya kutathmini nia za wengine. Jenga nidhamu katika mapambano.

Sura 10: Terrain and Situational Positioning

Inaangalia maeneo makubwa 3 (umbali wa eneo, vizingiti na hatari za eneo) na aina 6 za “strategic positions” ambazo zinatokana na maeneo hayo matatu. Nafasi zote 6 zina faida na hasara zake. Usijiingize katika mapambano usiyoweza kushinda. (Rejea sura 1). Jifahamu mwenyewe, mfahamu na kumwelewa sana adui yako. Elewa kama upo katika nafasi ya kuanzisha shambulizi, una njia ya kutokea mambo yakikuzidi?

Sura 11: The Nine Battlegrounds/Situations
Inaeleza hali tofauti katika vita na namna ya kiongozi wa vita atakavyozikabili. Unaweza kufananisha hii na mazingira tofauti katika maisha. Mahali ulipo panakupa “advantage” wewe, adui au wote. Usipigane vita nyumbani, Soma Zaidi hapa

Sura 12: The Fire Attack

Inaeleza matumizi ya silaha na hususani matumizi ya mazingira uliyopo kama silaha. Inaangalia maeneo matano kama ya mashambulizi kupiga adui, aina tano za mashambulizi ya kimazingira na namna ya kukabiliana na mashambulizi hayo. Unaweza kutumia moto kumdhoofisha adui yako kama vile kuchoma kambi walipo wanajeshi, kuchoma ghala, kuchoma dhana za usafirishaji, kuchoma silaha na kurusha moto kati ya majeshi ya adui.

Sura 13: Intelligence and Espionage
Inaangalia umuhimu wa kuwa na vyanzo vya kuaminika vya taarifa na aina tano za vyanzo vya intelijensia (majasusi ndani ya ngome yako,majasusi ndani ya ngome ya adui, kutumia majasusi waliotumwa na adui kwa faida yako, majasusi wenye kufanya mambo wazi wakiwa na nia ya kulaghai umma na adui, na wale wanaoleta taarifa kutoka kwa ngome ya adui. Inaeleza pia namna ya kusimamia kila kitengo. Wekeza katika intelijensia. Zuia intelijensia ya adui kujipenyeza katika ngome yako.

Baadhi ya Mafunzo;

1. Epuka vita/mapambano kadiri unavyoweza

2. Anzisha mapambano ambayo una uhakika wa kushinda

3. Ulaghai ni sehemu ya vita, onekana dhaifu ambapo una nguvu, onekana mwenye nguvu ambapo una udhaifu, ukiwa karibu muaminishe adui kwamba uko mbali, ukiwa mbali muaminishe kwamba ukaribu

4. Kama adui anakushinda nguvu, mwepuke

5. Tambua wakati wa mapambano na wakati wa kutulia.

6. Mbinu za kivita ni kama mkondo wa maji, hushuka chini kutoka milimani, epuka mahala penye nguvu, shambulia mahala dhaifu.

7. Jifunze kuwa tayari kwa mapambano hata wakati ambapo kunaonekana hakuna chembe ya uwezekano wa shambulizi

8. Kama kiongozi, jali timu yako lakini usiendekeze udhaifu, uoga, hasira na kupenda sifa.

9. Weka marafiki zako karibu, maadui zako karibu Zaidi

10. Kwenye kila mtafaruku, kuna mwanya.

11. Shambulia kama moto, kuwa imara kama mlima

12. Hakikisha adui hapati nafasi ya kupumzika

13. Muaminishe adui yako kwamba hatofaidika kwa kukushambulia, hii itapunguza ari yake

14. Jiamini

___________________
Tusiumize wala kuumizana.
Maisha ndio hayahaya .
Tuishi tukitenda yaliyo ya haki na kwa upendo.

Follow me.
mwanshinga Jr - facebook, twitter & instagram
 
Ile spirit kabisa ya kitabu ambayo ndiyo iliyonivutia kusoma hiki kitabu
Ni.
Vita ni kitu hatari sana KWA taifa lolote, ni kitu kitakacho amua Kama taifa litaendelea kuwepo au litapotezwa, vita ni Jambo la kufa na kupona..
hivyo vita vinabebwa na Mambo makuu matano,
1.Nidhamu na utii
Hii ni kutii sheria na maagizo bila kujali kuwa maisha yako yapo hatarini
 

Similar Discussions

4 Reactions
Reply
Back
Top Bottom