Sanaa ya uchoraji - Cyper255 (special thread)

Mchoraji Cyper255

JF-Expert Member
Nov 21, 2012
1,758
6,087
Uchoraji-ni-sanaa-ya kupaka rangi kwenye uso wa-karatasi,-kitambaa,-ubao,-metali,-mwamba au penginepo. Tokeo la uchoraji huitwa picha.

Karibu kwenye uzi huu kuona picha mbalimbali zilizochorwa kwa mkono.

Toa Maoni au Ushauri kukuza Sanaa ya Uchoraji Tanzania. Kama wewe ni mchoraji pia, Ruksa kuweka kazi yako hapa.

• NAOMBA USHIRIKIANO.
 
Hahahha mie hata nyumba sijui chora ila napenda zile picha za pale mwenge
 
Tuenze na hii picha ya Nyerere niliyoichora muda kidogo.

Karibuni sana. Nitakuwa naweka na michoro ya watu wengine pia.
 
Attachments

  • 1444849466539.jpg
    1444849466539.jpg
    80.5 KB · Views: 1,475
Hahahha mie hata nyumba sijui chora ila napenda zile picha za pale mwenge

Hakuna anaeshindwa kuchora. Unakumbuka kipindi upo shule, chekechea na std I-III tulivyokuwa tunachora. Tuliweza japo sio perfect.
 
Ahahahha!!! Wapo waliokuwa wanapata tabu inapokuja suala la kuchora vitu. Nakumbuka tulipokuwa tunapewa kazi ya kuchora darasani lazima nile sh.10 Za watu.
 
Napenda sana sanaa ya uchoraji.

Ila mimi kuchora sijui kabisa, roho inaniuma sana

Kwanza karibu. Na nimefurahi kuona unapenda Sanaa ya uchoraji. Usikate tamaa hakuna kinachoshindikana chini ya jua. Unaweza kujifunza taratibu na ukajua.
 
Kwanza karibu. Na nimefurahi kuona unapenda Sanaa ya uchoraji. Usikate tamaa hakuna kinachoshindikana chini ya jua. Unaweza kujifunza taratibu na ukajua.
Ahsante.

Nashukuru sana kwa kupeana moyo kama hivi.

Mbali na kujifunza kipaji nacho kiwepo.

Wewe kazi zako nazikubali sana tangu kwa mara ya kwanza nilipoziona hapa hapa JF ulipoweka link ya kazi zako.

Safi sana
 
Hii ni picha niliyojichora Mimi mwenyewe.

Unaweza kutazama shading ya light Ilivyokaa.
 
Attachments

  • 1444923465305.jpg
    1444923465305.jpg
    35.6 KB · Views: 1,128
Ahsante.

Nashukuru sana kwa kupeana moyo kama hivi.

Mbali na kujifunza kipaji nacho kiwepo.

Wewe kazi zako nazikubali sana tangu kwa mara ya kwanza nilipoziona hapa hapa JF ulipoweka link ya kazi zako.

Safi sana

Ndio kaka. Kipaji ni kitu cha muhimu zaidi. Ila KUIPENDA sanaa pia ni jambo la msingi.
Nashukuru sana kwa kuappriciate kazi Kaka.
 
Nias ametisha sana.

Amemtoa ARIANA GRANDE vile vile.

Sio siri nyie watu mnaweza

attachment.php
 
Back
Top Bottom