Nyota Njema
Senior Member
- Nov 18, 2010
- 148
- 16
Ni vigumu kusukuma gari ukiwa ndani.....
kweli kabisa,lakini vipi kama nje kuna mvua?
kwanini usijikinge ndani ya gari bovu afu utoke baadae kulisukuma mvua ikiisha?
Mwenye Haki, hutafuta haki mpaka aipate haijalishi kaangushwa mara ngapi, akiinuka lake ni moja tu Haki. Na Upiganiaji wa haki ni mchakato yaani tendo endelevu lisilokoma wala kukomeshwa na mtu yeyete mpata kinachotafutwa kipatikane. Usiogope, yupo kwa ajili ya watanzania.
Sidhani kama inalipa kuendelea kuhangaika na huyu Sitta maana ni mtu anayedhani kuwa ana nafasi ya kupata madaraka makubwa ndani ya CCM kupitia mtandao aliopo ndani ya chama hicho, ikibidi urais, hivyo hawezi kufikiria kuja CDM, labda itokee kuwa kabanana sana na hana jinsi.Sitta ni mtu mzima, huu ushauri wala hakustahili kupewa bali angekuwa ameshachukua hatua siku nyingi sana hata kabla wadau hamjaanza kumfikiria na kumshauri kama kweli ni alikuwa mpiganaji wa kweli, huyu naye ni opportunists kama walivyo wengine wengi ndani ya CCM, Mwakyembe, Magufuli, Tibaijuka, n.k. , just few to mention!Wadau naomba msisahau jinsi huyu mzee alivyomkejeri Dr. Slaa wakati wa kampeni kuwa JK sio saizi yake bali yeye (Sitta). Pamoja na kejeri hiyo ya kijinga, lakini bado Slaa alimpa ushauri wa kutokuukubali uteuzi aliopewa wa uwaziri wa EA. Sasa kama kakataa kupokea ushauri wa mtu makini kama Dr. Slaa, je atapokea huu ushauri wenu? Tusubiri kwanza ajeruhiwe halafu atatia akili!N.B: Kama kweli Sitta ni mpiganaji, kwa nini baada ya kutishiwa kunyang'anywa uanachama wa CCM wakati anasimamia mjadala wa Richmond, aliamua kufunika kombe ili kuwanusuru mafisadi na chama chake akidai kuwa maazimio yote 23 ya kamati teule ya Bunge yameshatekelezwa na serikali?
Kusaliti wenzio ndiyo kutafuta haki, nadhani mara mbili inatosha huyu ni wa kustaafu tu siasa!
CHADEMA ndiko nyumbani kwa wapambanaji wa Kweli.Si kwa Sitta tu na hata kwa watu wasafi kwenye vyama vingine.Mwenye hulka ya Kifisadi hawezi kukaa ndani ya CHADEMA kwa Raha.Hiyo ndiyo Reality
Chadema ipi? Hii iliyoingiliwa na mafisadi au nyingine? Msitubabaishe hapa, the difference is the same!
Kusaliti wenzio ndiyo kutafuta haki, nadhani mara mbili inatosha huyu ni wa kustaafu tu siasa!
Kusaliti wenzio ndiyo kutafuta haki, nadhani mara mbili inatosha huyu ni wa kustaafu tu siasa!
Naamini Sita ni Mpambanaji, lakini pia kama ni mtu safi hataogopa katu kuachana na CCM lakini kama ana madudu ambayo yamesikika pia! anaogopa watamchafua, ila sio vibaya kutubu pale ulipojikwaa na kuendeleza mazuri yaliyopo, karibu Chadema mkuu Samweli Sitta.
popote alipo anaweza kutetea mtanzania, si lazma awe cdm.