Samuel sitta, nisingeshiriki karamu ya wenye dhambi

Herbalist Dr MziziMkavu

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
43,073
Reaction score
34,844
attachment.php

Mheshimiwa Samuel Sitta.
Kwako mheshimiwa Samuel Sitta.

Ni matumaini yangu kwamba sasa unajipongeza kwa kufanikisha kazi uliyopewa ya kuliongoza Bunge Maalum la Katiba ya kuhakikisha akidi inatimia ili kupitisha rasimu ya katiba inayopendekezwa.

Najua una furaha sana kwa hilo, upo kwenye karamu ya kufurahia ushindi kiasi kwamba itakuwa

vigumu sana kwa lofa kama mimi kukutana na wewe hasa katika kipindi hiki ambacho unaamini kasi na viwango vyako vimedhihirika. Hata hivyo, hilo halinizuii kufikisha ujumbe wangu kwako.

Mimi si Mbunge wa Urambo Mashariki kama wewe, sikuzaliwa Desemba 18, 1942 wala sijamuoa mwanamke mwanasiasa, Magreth Sitta aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikali kama wewe.
Mimi ni mwananchi wa kawaida tu, lofa, hohehahe nisiye na mbele wala nyuma.

Sijawahi kuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wala sijawahi kujipatia umaarufu mkubwa na kupendwa na wengi kutokana na kuruhusu mijadala ya ufisadi bungeni kama ulivyo wewe. Sijawahi kuibua kashfa kubwa kama ya Richmond na kusababisha baadhi ya vigogo wang’atuke kwenye nyadhifa zao.

Sina nia wala sitegemei kuja kugombea urais wa nchi hii kama wewe, mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa. Sijawahi kujisifu kwamba mimi ni mtu wa viwango na kasi, mimi ni mlala hoi tu.

Sijawahi kuitumia nchi hii katika nyadhifa mbalimbali kuanzia nilipokuwa shule, kwa zaidi ya miaka 40

nikigusa karibu awamu zote za uongozi kama wewe, mimi si Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wala sijawahi kuota ndoto kwamba nitakuja kuwa Spika wa Bunge Maalum la Katiba! Narudia tena, mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa, hohehahe nisiye na ndoto za kuja kuwa mwanasiasa.

Hata hivyo, ningekuwa mimi ndiyo nipo kwenye nafasi yako, hakika nakuapia nisingeshiriki kwenye karamu ya wenye dhambi kama wewe. Nisingeshiriki hata kidogo kuchakachua maoni ya mwenyekiti wa tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya, Jaji Joseph Warioba kama wewe.

Nisingerudia kukusanya upya maoni kwa wananchi wakati nikijua fika kuwa hiyo siyo kazi yangu.

Nisingebadilika ghafla kama wewe, kutoka kuwa shujaa wa kutegemewa kama ulivyokuwa kipindi ulipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na kuwa adui wa demokrasia kama ulivyo sasa.

Nakuhakikishia nisingeshiriki kabisa karamu ya wenye dhambi, kwa kulazimisha wajumbe wa bunge maalum la katiba, hata kwa vitisho waipigie kura ya ndiyo rasimu ya katiba inayopendekezwa huku nikijua waziwazi kwamba nimeshiriki kunyofoa vipengele vyote muhimu ambavyo wananchi walivipendekeza ili kupata katiba bora.

Nisingefikia hatua ya kuwatusi viongozi wa dini ambao walikuwa wakinionesha waziwazi kwamba nilichokuwa nakifanya kwenye bunge maalum la katiba hayakuwa matakwa ya Mungu bali ya watu wachache wenye dhambi.

Kwa kuwa najua kwamba katiba ndiyo ‘injini’ ya maendeleo ya taifa lolote, ningekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba maoni ya wananchi ndiyo yanayoingia kwenye katiba bila kuchakachuliwa. Ningethibitisha kwa vitendo kwamba mimi ni mtu wa kasi na viwango!

Nisingekubali kuongozwa na tamaa ya kuja kuwa rais wa nchi hii kiasi cha kulipua mchakato mzima wa kupata katiba kwa maslahi yangu na chama changu kwa sababu ningejua kwamba umri umeshanitupa mkono (Una miaka 71 sasa) lakini wapo wanangu, wajukuu na ndugu zangu wengi na

watu wanaoniamini ambao wanaisubiri kwa hamu katiba mpya itakayowakomboa, baada ya ile ya awali kushindwa kuwatatulia kero zao kwa zaidi ya miaka hamsini sasa.

Narudia tena, nisingeongozwa na tamaa ya madaraka, upendeleo kwa chama changu wala maslhai ya mtu au watu fulani, la hasha! Ningesimamia haki katika ukamilifu wake na rasimu ambayo

ingepatikana, ingekuwa ni mawazo ya wananchi wote na siyo uhuni kama uliofanyika sasa kupata rasimu ya katiba inayopendekezwa.

Ningeongozwa na hofu ya Mungu na nisingewaangusha wananchi ambao kwa kipindi kirefu waliniona mpiganaji ninayesimamia maslahi yao na taifa kwa jumla na kamwe nisingeshiriki karamu ya wenye dhambi kama ilivyotokea kwenye Bunge Maalum la Katiba.

Kwa bahati mbaya mimi nitabaki kuwa mimi na sitaweza kuwa wewe lakini kama ningekuwa mimi kwenye nafasi yako, kwa jinsi hali ilivyo sasa, narudia tena kusema bila kumung’unya maneno kwamba nisingeshiriki kwenye karamu ya wenye dhambi kama wewe, ningesimamia ukweli, haki na demokrasia bila kumpendelea wala kumkandamiza mtu yeyote.
Wasalaam! Chanzo.GBP
 
Attachments

  • sitta.jpg
    sitta.jpg
    21 KB · Views: 4,005
hata kama sita alifikiri kuondoa vipengele vyote vilivyo pendekezwa na wananchi kungemsaidia yeye kupitishwa na ccm kugombea urais naona hapa kafanya kosa kubwa kwani tuliokuwa tunamwona anafaa tumetumedhihirisha bila shaka kuwa hafai kabisa kwani maslahi ya nchi hii kwake si kitu isipokuwa urais tu.
 
Yes. Umeweza eleza hisia zako kwa namna nzuri sana.Kumbe JF bado watu makini mpo. Mimi nilikuwa nimekata tamaaa baada ya kuona jf imevamiwa na dogs. Nasikia ni vijana wa Lumumba. Lakini aliyewaajiri nadhani alitumia kanuni ya kupima IQ maana wote wana kiwango cha chini sana.
 
Watu makini wako wengi na sio jf tu, na ndio maana hawa magamba wanatumia kila njia kuhakikisha watu makini hawana nafasi kabisa kuonyesha umakini wao. Wanatumia every dirty trick kuhakikisha mambo na mfumo unabaki hivi hivi hata kama itamaanisha wao kwenda kinyume na viwango walivyokwisha jiwekea mwanzo.

Yes. Umeweza eleza hisia zako kwa namna nzuri sana.Kumbe JF bado watu makini mpo. Mimi nilikuwa nimekata tamaaa baada ya kuona jf imevamiwa na dogs. Nasikia ni vijana wa Lumumba. Lakini aliyewaajiri nadhani alitumia kanuni ya kupima IQ maana wote wana kiwango cha chini sana.
 
Now we know him better gt it he is villain, he is a 🐍, he is a wolf 🐺 hidden in a lamb's skin. Thank you mchakato wa katiba.
 
attachment.php

Mheshimiwa Samuel Sitta.
Kwako mheshimiwa Samuel Sitta.

Ni matumaini yangu kwamba sasa unajipongeza kwa kufanikisha kazi uliyopewa ya kuliongoza Bunge Maalum la Katiba ya kuhakikisha akidi inatimia ili kupitisha rasimu ya katiba inayopendekezwa.

Najua una furaha sana kwa hilo, upo kwenye karamu ya kufurahia ushindi kiasi kwamba itakuwa

vigumu sana kwa lofa kama mimi kukutana na wewe hasa katika kipindi hiki ambacho unaamini kasi na viwango vyako vimedhihirika. Hata hivyo, hilo halinizuii kufikisha ujumbe wangu kwako.

Mimi si Mbunge wa Urambo Mashariki kama wewe, sikuzaliwa Desemba 18, 1942 wala sijamuoa mwanamke mwanasiasa, Magreth Sitta aliyewahi kushika nyadhifa mbalimbali serikali kama wewe.
Mimi ni mwananchi wa kawaida tu, lofa, hohehahe nisiye na mbele wala nyuma.

Sijawahi kuwa spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wala sijawahi kujipatia umaarufu mkubwa na kupendwa na wengi kutokana na kuruhusu mijadala ya ufisadi bungeni kama ulivyo wewe. Sijawahi kuibua kashfa kubwa kama ya Richmond na kusababisha baadhi ya vigogo wang'atuke kwenye nyadhifa zao.

Sina nia wala sitegemei kuja kugombea urais wa nchi hii kama wewe, mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa. Sijawahi kujisifu kwamba mimi ni mtu wa viwango na kasi, mimi ni mlala hoi tu.

Sijawahi kuitumia nchi hii katika nyadhifa mbalimbali kuanzia nilipokuwa shule, kwa zaidi ya miaka 40

nikigusa karibu awamu zote za uongozi kama wewe, mimi si Waziri wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki wala sijawahi kuota ndoto kwamba nitakuja kuwa Spika wa Bunge Maalum la Katiba! Narudia tena, mimi ni mwananchi wa kawaida kabisa, hohehahe nisiye na ndoto za kuja kuwa mwanasiasa.

Hata hivyo, ningekuwa mimi ndiyo nipo kwenye nafasi yako, hakika nakuapia nisingeshiriki kwenye karamu ya wenye dhambi kama wewe. Nisingeshiriki hata kidogo kuchakachua maoni ya mwenyekiti wa tume ya kukusanya maoni kuhusu katiba mpya, Jaji Joseph Warioba kama wewe.

Nisingerudia kukusanya upya maoni kwa wananchi wakati nikijua fika kuwa hiyo siyo kazi yangu.

Nisingebadilika ghafla kama wewe, kutoka kuwa shujaa wa kutegemewa kama ulivyokuwa kipindi ulipokuwa Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano na kuwa adui wa demokrasia kama ulivyo sasa.

Nakuhakikishia nisingeshiriki kabisa karamu ya wenye dhambi, kwa kulazimisha wajumbe wa bunge maalum la katiba, hata kwa vitisho waipigie kura ya ndiyo rasimu ya katiba inayopendekezwa huku nikijua waziwazi kwamba nimeshiriki kunyofoa vipengele vyote muhimu ambavyo wananchi walivipendekeza ili kupata katiba bora.

Nisingefikia hatua ya kuwatusi viongozi wa dini ambao walikuwa wakinionesha waziwazi kwamba nilichokuwa nakifanya kwenye bunge maalum la katiba hayakuwa matakwa ya Mungu bali ya watu wachache wenye dhambi.

Kwa kuwa najua kwamba katiba ndiyo ‘injini' ya maendeleo ya taifa lolote, ningekuwa mstari wa mbele kuhakikisha kwamba maoni ya wananchi ndiyo yanayoingia kwenye katiba bila kuchakachuliwa. Ningethibitisha kwa vitendo kwamba mimi ni mtu wa kasi na viwango!

Nisingekubali kuongozwa na tamaa ya kuja kuwa rais wa nchi hii kiasi cha kulipua mchakato mzima wa kupata katiba kwa maslahi yangu na chama changu kwa sababu ningejua kwamba umri umeshanitupa mkono (Una miaka 71 sasa) lakini wapo wanangu, wajukuu na ndugu zangu wengi na

watu wanaoniamini ambao wanaisubiri kwa hamu katiba mpya itakayowakomboa, baada ya ile ya awali kushindwa kuwatatulia kero zao kwa zaidi ya miaka hamsini sasa.

Narudia tena, nisingeongozwa na tamaa ya madaraka, upendeleo kwa chama changu wala maslhai ya mtu au watu fulani, la hasha! Ningesimamia haki katika ukamilifu wake na rasimu ambayo

ingepatikana, ingekuwa ni mawazo ya wananchi wote na siyo uhuni kama uliofanyika sasa kupata rasimu ya katiba inayopendekezwa.

Ningeongozwa na hofu ya Mungu na nisingewaangusha wananchi ambao kwa kipindi kirefu waliniona mpiganaji ninayesimamia maslahi yao na taifa kwa jumla na kamwe nisingeshiriki karamu ya wenye dhambi kama ilivyotokea kwenye Bunge Maalum la Katiba.

Kwa bahati mbaya mimi nitabaki kuwa mimi na sitaweza kuwa wewe lakini kama ningekuwa mimi kwenye nafasi yako, kwa jinsi hali ilivyo sasa, narudia tena kusema bila kumung'unya maneno kwamba nisingeshiriki kwenye karamu ya wenye dhambi kama wewe, ningesimamia ukweli, haki na demokrasia bila kumpendelea wala kumkandamiza mtu yeyote.
Wasalaam! Chanzo.GBP

Namuogopa sitta kama UKOMA.... anataka kwenda Ikulu...@ the age of 71, Ikulu kuna biashara gani, mpaka atumie nguvu kubwa kiasi hiki - hadi kutukana viongozi wa dini eti ni wapuuzi. Je atalipaje....!!!
 
Nakumbuka wakati wae issue ya richmond kuna kiongozi alisema kwa uchungu kuwa au shida ni uwaziri mkuu nikadhani ni jazba tu. Kumbe huyu mzee six ana tamaa kubwa sana ya madaraka na yuko tayari kufanya chochote ili mradi lake litimie. Asante mchakato wa katiba umetuwezesha kuwajua wasiotufaa.
 
2nd october 20140 itabaki vichwani mwa watu wenye akili kuwa ni siku ambayo watanzania tulisalitiwa, tulipokwa haki yetu ya kuamua aina na mfumo wa utawala tunaoutaka, tulifanywa wajinga na mazuzu kwa ghiliba ya watu wachache na waroho wa madaraka.

Watanzania wa leo si wajinga tena.
 
Hakuna jina limfaalo Sita kwa sasa maana tukimwita mhuni, wahuni wengi madhara yao huwa si kama ya Sita. Tukimwita mwizi, wevi wa kawaida huwa hawaibi pesa nyingi kama hizi alizoiba Sita na wenzake. Tukimwita mhaini, wahaini hupindua serikali, lakini Sita amepindua mamlaka ya wananchi.

Huyu Sita hakuna hata adhabu imfaayo. Akigombea tukamnyima kura, hata watu wema kuna wakati wanakosa kura. Akiwekwa jela, hata wevi wa kuku wapo jela. Tukiamua anyongwe, kuna walionyongwa kwa kuua hata mtu mmoja tu lakini Sita ameua Taifa lililotarajiwa. Sita anafaa kupewa adhabu gani? Mungu ndiye ajuaye.
 
Haishangazi, Mzambia atakuwa NA uchungu gani NA Tanzania ?????
 
Mkuu Mzizimkavu umenena,na si hayo tu mheshimiwa alipewa ulinzi wa kumlinda kutokana na umairi wake wa kupambana na ufisadi,sishangai sana. kwani Kwenye biblia kuna kipengere kinasema ''nilikupanda mbegu safi ya mzabibu ,umageukaje basi kuwa mzabibu mwitu machoni pangu?
Kwa mjibu wa biblia si ajabu mzabibu kugeuka na kuwa mzabibu mwitu.Labda unapotaka kuingia ikulu lazima ubadilike kama ulikuwa mwema uwe mwovu na kama ulikuwa mwovu uwe mwema.kati ya hayo mojawapo linamtokea mzee wetu.
 
Hili la kutukana viongozi wa dini,naona ameasi hata sakramenti ya ndoa takatifu kwani alifungishwa ndoa na hao hao aliowakashfu hivyo na ndoa yake ni batiri.isitoshe yeye ni muumini mwenye haki ya kushiriki meza ya Bwana,je atapigaje magoti kushirikishwa na wale aliowadharau hadharani? Bila shaka atakuwa anakula hukumu yake mwenyewe.
 
Hakuna jina limfaalo Sita kwa sasa maana tukimwita mhuni, wahuni wengi madhara yao huwa si kama ya Sita. Tukimwita mwizi, wevi wa kawaida huwa hawaibi pesa nyingi kama hizi alizoiba Sita na wenzake. Tukimwita mhaini, wahaini hupindua serikali, lakini Sita amepindua mamlaka ya wananchi.

Huyu Sita hakuna hata adhabu imfaayo. Akigombea tukamnyima kura, hata watu wema kuna wakati wanakosa kura. Akiwekwa jela, hata wevi wa kuku wapo jela. Tukiamua anyongwe, kuna walionyongwa kwa kuua hata mtu mmoja tu lakini Sita ameua Taifa lililotarajiwa. Sita anafaa kupewa adhabu gani? Mungu ndiye ajuaye.

LOL maneno mazito sana haya. umeniongezea hasira gafla.
 
Hili la kutukana viongozi wa dini,naona ameasi hata sakramenti ya ndoa takatifu kwani alifungishwa ndoa na hao hao aliowakashfu hivyo na ndoa yake ni batiri.isitoshe yeye ni muumini mwenye haki ya kushiriki meza ya Bwana,je atapigaje magoti kushirikishwa na wale aliowadharau hadharani? Bila shaka atakuwa anakula hukumu yake mwenyewe.
Halafu watu wakizeeka huwa wanakuwa wacha MUNGU lakini huyu amezeeka lakini amekua mcharuko.
 
Back
Top Bottom