unaohiajikaRais aseme hatuna ugomvi na Rwanda halafu Cabinet minister tena wa wizara ya EAC anakubali kuna ugomvi kati ya wanasiasa hawa wawili yaani Kikwete na Kagame !
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema ugomvi wa wanasiasa katika jumuia hiyo hauwezi kuathiri shughuli za kibiashara na uchumi wa Tanzania kwa kuwa wafanyabiashara wanaangalia faida zaidi katika shughuli zao.
Sitta alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua athari za kiuchumi zitakazopatikana baada ya kuwapo kwa taarifa ya wafanyabiashara wa Rwanda kutaka kupitisha mizigo yao katika bandari ya Mombasa badala ya ile ya Dar es Salaam.
Alisema kuwa taarifa ya wafanyabiashara wa Rwanda kuazimia kutumia bandari ya Mombasa si za ukweli na kwamba wanaofanya hivyo ni wale waliokosa zabuni mbalimbali ambazo pia hakuzitaja ni zabuni ya nini.
Mimi ninachojua suala la hapa ni uchumi. Huu ugomvi wa wanasiasa wawili hauwezi kuwakimbiza wafanyabiashara na ukiangalia wanaopitisha mizigo ni wafanyabiashara na si serikali zinazolumbana, alisema.
Aliongeza kuwa migongano baina ya nchi na nchi haiepukiki hususan zilizo jirani na kuita hali hiyo ya mpito huku akisisitiza kuwa maelewano baina ya Tanzania na Rwanda yatarejea muda si mrefu.
Waziri Sitta alisema umbali kati ya Mombasa na Kigali ni kilometa 2300 na kutoka Dar es Salaam hadi Kigali ni kilometa 1400, suala alilodai wafanyabiashara wataangalia umbali katika kutafuta faida ya kazi wanazozifanya.
Alieleza kuwa mkakati mwingine wa kuwafanya wafanyabishara wazidi kuitumia bandari ya Dar es Salaam ni kupunguza vizuizi vya njiani kutoka 15 vya sasa hadi vitatu.
Alisema kuwa na vizingiti vingi barabarani ni tatizo huku akiwashangaa askari wanaosimamisha magari yenye lakiri ambazo hawawezi kuzifungua na kueleza hali hiyo ni kero kwa madereva na wafanyabiashara.
Juzi, msemaji wa Chama cha mizigo nchini (Tatoa) Elias Lukumay, aliiambia kamati ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi za Rwanda na Uganda zimekubaliana kutumia bandari ya Mombasa kutokana na urasimu unaodaiwa kuwepo katika bandari ya Dar es Salaam.
Alisema nchi hizo zimekubaliana kuanza kutumia bandari ya Mombasa kuanzia Septemba mwaka huu.
Uamuzi huo wa Rwanda na Uganda unatafsiriwa kuwa unatokana na msigano wa kisiasa ulioibuka hivi karibuni baina ya Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame wa Rwanda baada ya ushauri wake wa kumtaka Kagame akutane na waasi kwa ajili ya kujadili amani ya taifa lao
unaohiajika
hiyo mbona inaeleweka ni kweli kwamba hakuna ugomvi kati ya tz na rwanda ila ni kutokuelewana kwa wanasiasa wakuu wa nchi mbili hizi........................................that is too obvious mkuu sita hajatofautiana na bosi wake hapo ni uelewa tu
ucnilazimishe nikubali unachoamini wewe, acha niwe mshamba kuliko kuwa mjumbe ndiyo ..............hayo ni maelezo kwa mujibu wa uelewa wako.........natambua positions za marais na flags wanazobeba so nilichoandika nakielewa na nakiamini upo hapoAcha ushamba. Kutoelewana kati ya marais wawili maana yake ni kuwa hizo serikali mbili hazielewani. Marais wawili wakigombana huwa hawarushiani ngumi na mateke bali huamuru majeshi ya nchi hizo na kuanza kupigana, yaani huo ni ugomvi wa nchi na nchi. Kikwete anapoitwa rais anakuwa anawakilisha nchi na wananchi wake na siyo familia yake tu na hivyo huongea kwa niaba yetu. kwa hiyo hata ushauri alioutoa kule addis alifanya hivyo kwa niaba ya serikali anayoingoza na watu wake.
ucnilazimishe nikubali unachoamini wewe, acha niwe mshamba kuliko kuwa mjumbe ndiyo ..............hayo ni maelezo kwa mujibu wa uelewa wako.........natambua positions za marais na flags wanazobeba so nilichoandika nakielewa na nakiamini upo hapo
WAZIRI wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Samuel Sitta, amesema ugomvi wa wanasiasa katika jumuia hiyo hauwezi kuathiri shughuli za kibiashara na uchumi wa Tanzania kwa kuwa wafanyabiashara wanaangalia faida zaidi katika shughuli zao.
Sitta alitoa kauli hiyo jana Ikulu jijini Dar es Salaam wakati akijibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua athari za kiuchumi zitakazopatikana baada ya kuwapo kwa taarifa ya wafanyabiashara wa Rwanda kutaka kupitisha mizigo yao katika bandari ya Mombasa badala ya ile ya Dar es Salaam.
Alisema kuwa taarifa ya wafanyabiashara wa Rwanda kuazimia kutumia bandari ya Mombasa si za ukweli na kwamba wanaofanya hivyo ni wale waliokosa zabuni mbalimbali ambazo pia hakuzitaja ni zabuni ya nini.
Mimi ninachojua suala la hapa ni uchumi. Huu ugomvi wa wanasiasa wawili hauwezi kuwakimbiza wafanyabiashara na ukiangalia wanaopitisha mizigo ni wafanyabiashara na si serikali zinazolumbana, alisema.
Aliongeza kuwa migongano baina ya nchi na nchi haiepukiki hususan zilizo jirani na kuita hali hiyo ya mpito huku akisisitiza kuwa maelewano baina ya Tanzania na Rwanda yatarejea muda si mrefu.
Waziri Sitta alisema umbali kati ya Mombasa na Kigali ni kilometa 2300 na kutoka Dar es Salaam hadi Kigali ni kilometa 1400, suala alilodai wafanyabiashara wataangalia umbali katika kutafuta faida ya kazi wanazozifanya.
Alieleza kuwa mkakati mwingine wa kuwafanya wafanyabishara wazidi kuitumia bandari ya Dar es Salaam ni kupunguza vizuizi vya njiani kutoka 15 vya sasa hadi vitatu.
Alisema kuwa na vizingiti vingi barabarani ni tatizo huku akiwashangaa askari wanaosimamisha magari yenye lakiri ambazo hawawezi kuzifungua na kueleza hali hiyo ni kero kwa madereva na wafanyabiashara.
Juzi, msemaji wa Chama cha mizigo nchini (Tatoa) Elias Lukumay, aliiambia kamati ya Bunge ya Bajeti kuwa nchi za Rwanda na Uganda zimekubaliana kutumia bandari ya Mombasa kutokana na urasimu unaodaiwa kuwepo katika bandari ya Dar es Salaam.
Alisema nchi hizo zimekubaliana kuanza kutumia bandari ya Mombasa kuanzia Septemba mwaka huu.
Uamuzi huo wa Rwanda na Uganda unatafsiriwa kuwa unatokana na msigano wa kisiasa ulioibuka hivi karibuni baina ya Rais Jakaya Kikwete na Paul Kagame wa Rwanda baada ya ushauri wake wa kumtaka Kagame akutane na waasi kwa ajili ya kujadili amani ya taifa lao
Rais aseme hatuna ugomvi na Rwanda halafu Cabinet minister tena wa wizara ya EAC anakubali kuna ugomvi kati ya wanasiasa hawa wawili yaani Kikwete na Kagame !
Anaongea kama vile anamaanisha Mwenyekiti wa kijiji huko Malampaka ya hapa Tanzania anagombana na Mwenyekiti wa kijiji huko Rutiringarire nchini RwandaIna maana Sitta hafahamu kuwa hawa wanasiasa wawili ndio nchi zenyewe?