Samuel Sitta Anatisha-According to Rai!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Samuel Sitta Anatisha-According to Rai!!!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mdondoaji, Aug 9, 2010.

 1. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #1
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  *Ahamishia Ofisi ya Spika wa Bunge Urambo Mashariki
  *Thamani yake yamduwaza Kikwete, asema nchi itafilisika

  Na Waandishi Wetu


  MBUNGE wa Urambo Mashariki, mkoani Tabora, Samuel Sitta, amedhihirisha kwamba yeye ni mtu wa viwango vya hali ya juu, baada ya kuomba Serikali imjengee Ofisi ya Jimbo, yenye hadhi sawa na Ofisi ya Spika iliyoko katika jengo la Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, iliyoko Dodoma.

  Ofisi hiyo, ambayo ilizinduliwa na Rais Jakaya Kikwete wiki iliyopita, inaelezwa kuigharimu Serikali zaidi ya Sh milioni 500, kama zitajumlishwa gharama za ujenzi pamoja na samani (furniture) zilizomo ndani ya ofisi hiyo, maalumu kwa ajili ya mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki.


  Haikuweza kufahamika ni kwanini Sitta, ambaye pia ni Spika wa Bunge linalomaliza muda wake, aliamua kujenga ofisi mpya wakati tayari anayo Ofisi ya Mbunge katika jengo la mkuu wa wilaya ya Urambo.


  Rai limeelezwa kwamba kila mbunge, katika mwaka wa fedha wa 2009/2010, alitengewa Sh milioni 65 kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya mbunge jimboni kwake, lakini mbunge wa Urambo Mashariki yeye aliamua ajenge ofisi yenye hadhi ya nafasi yake ya Uspika.


  Habari zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya watu walioshuhudia hafla ya uzinduzi wa ofisi hiyo uliofanywa na Rais Kikwete wiki iliyopita, zinasema hata Rais alishitushwa na hadhi ya ofisi hiyo, kiasi cha kujikuta akitamka kwamba ‘kama kila mbunge atataka ajengewe ofisi ya kiwango hiki, basi wabunge wataifilisi nchi hii.'


  Jengo la ofisi hiyo ya jimbo, mbali na kuwa na ofisi ya mbunge, inayo pia ofisi ya msaidizi wa mbunge, katibu muhtasi, watumishi wengine wasaidizi (technical staff), chumba maalumu cha watu mashuhuri (vip lounge) na ukumbi wa mikutano unaoweza kuwakusanya watu 30 wakiwa wamekaa kwenye viti.


  Rai limefanikiwa kupata baadhi ya nyaraka za mawasiliano baina ya Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, Ramadhani Khijjah, zinazoelezea uhamishwaji wa fedha kutoka katika vifungu vya maendeleo (fungu 42) kwenda fungu Na 85 cha RAS Tabora ili zikafanye kazi ya ujenzi wa ofisi hiyo.


  Kwa mujibu wa nyaraka hizo, Juni 11 mwaka jana, Dk Kashililah alimwandikia barua Khijjah, akijibu barua ya Katibu Mkuu huyo yenye kumb. Na. C/AB/422/01 ya Mei 13, 2009, ambayo ilielekeza kutenga fedha kwenye Fungu 42: Mfuko wa Bunge, kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa ofisi ya mbunge wa Urambo Mashariki.


  Katika barua hiyo, Dk Kashililah anamuomba Katibu Mkuu Hazina, kuhamisha Sh milioni 200 kutoka Fungu 42 kwenda Fungu 85: Mkoa wa Tabora "kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa ofisi ya mbunge wa jimbo la Urambo Mashariki."


  Kwa mujibu wa barua hiyo, fedha hizo ziliombwa ‘kwa ajili ya kukamilisha ujenzi' na si kuanza ujenzi, hali inayotafisiriwa na wachambuzi wa mambo ya ujenzi kwamba wakati kiasi hicho cha fedha kikiombwa, tayari mradi huo ulikwishatumia kiasi kingine zaidi ya hicho, kuanzia ujenzi wenyewe, usanifu na uchoraji wa ramani ya jengo.


  Pamoja na barua hiyo, ipo barua nyingine ya Juni 4, mwaka huu, ambayo Katibu wa Bunge, Dk Kashililah alimwandikia Katibu Mkuu Hazina, akiomba kuhamishwa Sh milioni 72 kutoka katika fungu hilo la 42 kwenda fungu 85 kwa ajili pia ya ‘kukamilisha ujenzi wa ofisi ya mbunge wa Urambo Mashariki.


  "Mradi huo (ofisi ya mbunge wa Urambo Mashariki) haukuweza kukamilika kutokana na upungufu wa fedha zilizopelekwa kupitia Fungu 85: RAS Tabora. Ili kuweza kukamilisha kazi hiyo, naomba kuhamisha kiasi cha Sh 72,000,000 kutoka Fungu 42: Mfuko wa Bunge kwenda Fungu 85: RAS Tabora. Fedha hizo (Sh milioni 72) zihamishwe kutoka vifungu vya maendeleo ambazo hazikuweza kutolewa kutokana na kuchelewa kutekelezwa kwa miradi iliyokusudiwa," inasema sehemu ya barua hiyo ya Dk Kashililah.


  Dk Kashililah amekiri kuwapo kwa mawasiliano hayo baina yake na Katibu Mkuu wa Hazina pamoja na uhamishaji wa fedha hizo kutoka Mfuko wa Maendeleo wa Bunge ili zikatumike kujenga ofisi hiyo, akisema mradi huo ni sehemu ya miradi ya maendeleo ya Bunge.


  Juhudi za kumpata Katibu Mkuu Hazina jana hazikufanikiwa baada ya mtu mmoja katika ofisi yake, aliyejitambulisha kuwa Katibu Muhtasi wake, kuliambia Rai kwamba Katibu huyo, kwa wakati huo tuliopiga simu, alikuwa Ikulu.


  Mbali na mamilioni hayo ya Shilingi yaliyotumika katika ujenzi wa ofisi ya mbunge huyo, samani za ofisi (furniture) zilizonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya ofisi, zimeigharimu Serikali Sh 100,931,300.00.


  Msambazaji wa samani hizo, ambaye alipatikana kwa utaratibu wa wazi kabisa wa zabuni ni M/S Mariedo Home Decor. Huyo naye anatiliwa shaka na baadhi ya wadadisi wa mambo, akidaiwa kuwa mshirika wa karibu wa mbunge wa Urambo Mashariki.


  Shaka hiyo, inatokana na ukweli kwamba katika wazabuni wanne waliokuwa wameorodheshwa na Bodi ya Zabuni ya Bunge, M/S Meriedo ndiye aliyekuwa mtu ghali sana, pengine mara mbili ya wengine.


  Kwa mujibu wa fomu ya ulinganisho wa bei za Wazabuni (Comparison of Technical Aspects Against Quoted Price), Wazabuni wanne waliokuwa wameteuliwa, bei zao zikiwa katika mabano, ni pamoja na M/S Living Room (Sh 64,769,960.00), M/S Quality Furniture and General Appliance (Sh 49,967,760.00), M/S Mariedo Home Décor (Sh 100,931,300.00 na M/S Alea Industries Ltd (80,462,624.00).


  Miongoni mwa mahitaji muhimu katika ofisi ya mbunge huyo, ambayo yanalazimika kununuliwa na Serikali, ni pamoja na kompyuta ndogo (Laptop) ya inchi 17, mashine ya kudurufu karatasi (printer), Televisheni kubwa na ungo wake (Flat Screen TV with Dish), kioo kikubwa na vidude vya kutundikia koti ofisini (Coat hanger).


  Aidha, kwenye korido ya kuingilia ofisini kwake, inahitajika seti moja ya viti vya bustanini, stuli 4 na meza ndogo ya bustanini, wakati ukumbi wa mikutano unahitaji kuwekewa meza ya mikutano na viti 24, huku vikihitajika pia viti vya dharura sita pamoja na dawati dogo moja.


  Katika moja ya madokezo kati ya Mkurugenzi wa Utawala wa Wilaya ya Urambo (DAD) na wataalamu wake, katika kujadili aina ya samani na gharama zake zinazohitajika kununuliwa kwa ajili ya ofisi hiyo, imeandikwa:


  "Baada ya kushirikiana na Msaidizi wa Spika, na kutokana na ‘taste' ya Mh Spika, gharama ya ununuzi wa samani ni Sh 69,560,000.00 kutoka kwa M/S Mariedo Home Décor. Gharama hizi hazihusishi items zifuatazo: Air Condition, Laptop, kompyuta, photocopy mashine, Fax Machine, Printer na Generator ya 20kv."


  Ofisi hiyo ya mbunge wa Urambo Mashariki, ilizinduliwa hivi karibuni na Rais Jakaya Kikwete, siku chache baada ya kuhutubia Bunge na kuahirishwa, kabla ya kuvunjwa rasmi Agosti Mosi mwaka huu.


  Watanzania walio wengi, walioshuhudia hafla ya ufunguzi huo kwa macho na au kupitia matangazo ya vituo vya televisheni nchini, walionyeshwa kushitushwa na ukubwa na ubora wa ofisi hiyo, kiasi cha baadhi ya watazamaji hao kupiga simu chumba cha habari cha gazeti hili, wakisema: "Kumbe Serikali hii ina fedha nyingi, haiwezekani ofisi ya mbunge ifanane na ukumbi wa Bunge Dodoma."


  Wengine walikwenda mbele zaidi na kuhoji: "Kwa nini mbunge, na hasa majimbo ya Urambo awe na ofisi ya gharama kubwa ya namna ile wakati wakazi wa Urambo ni masikini wa kutupwa ikilinganishwa na wilaya nyingine nchini?"


  Mtazamo: Kama ni kweli basi nchi inakoelekea ni kubaya na it is time Chama chengine kiingie katika utawala tumechoka na huu ubadhirifu. Ila kama siasa chafu duh kampeni zimeanza!!!
   
 2. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #2
  Aug 9, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 184
  Trophy Points: 160
  Sera ya sisiemu ni kuwa kipindi kama hiki wanaccm lazima waungane kuupiga upinzani? I am wondering hapa nani ni ccm na nani ni upinzani kati ya Samwel Sitta na Rostam Aziz (na magazeti yake)
   
 3. Lyampinga

  Lyampinga Senior Member

  #3
  Aug 9, 2010
  Joined: Apr 13, 2008
  Messages: 143
  Likes Received: 52
  Trophy Points: 45
  Siasa chafu zenyewe hizi... RAI hata bure sitaki kulisikia.. This is a vile and vindictive campaign
   
 4. R

  Ramos JF-Expert Member

  #4
  Aug 9, 2010
  Joined: May 13, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Duh!!!
   
 5. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #5
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,555
  Likes Received: 4,683
  Trophy Points: 280
  Hivi Rai ni gazeti au ni kipeperushi?
   
 6. Elusive

  Elusive JF-Expert Member

  #6
  Aug 9, 2010
  Joined: Nov 26, 2008
  Messages: 223
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Yetu macho na maskio!!!!!!
   
 7. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #7
  Aug 9, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Tuache ushabiki unaokosa uchambuzi. Kwa nini tunashambulia gazeti na siyo kuchambua yaliyoandikwa?

  1.Ni kweli ofisi hiyo ni ya milioni 500?
  2.Ni kweli pesa zimehamishwa kutoka fungu la maendeleo kujenga ofisi hii?
  3. Ni kweli kwamba mkandarasi wa samani aliyechaguliwa alipata tenda hii kwa njia za kifisadi?
  4. Je ni kweli ofisi hii imegharimu kiasi hiki kwa sababu tu mbunge wa Urambo Mashariki ni spika? Je Spika wa Bunge lijalo akiwa Mh. wa Lindi Mjini naye atajengewa ofisi hii ya milioni 500?
  5. Katibu wa Bunge ana nguvu gani za kisheria za kutengua maamuzi ya wabunge wa jamhuri ya Muungano? Na kama nguvu hizi za kisheria kweli anazo kuna maana gani ya kuwa na bunge?

  Kuna maswali mengi sana yanahitaji majibu hapa badala ya kulishambulia gazeti la rai.
   
 8. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #8
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Ndio maana nikasema ikiwa kuna ukweli ni taarifa ya msingi yenye kuwa na manufaa kwa jamii but kama ni majungu na fitina then watanzania sasa hivi hatufati kama maji ya mto.
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  ..nimekuwa nikiwaambia kwa muda mrefu kwamba Samuel Sitta ana historia ya ufisadi tangu akiwa waziri wa ujenzi, waziri wa ustawishaji makao makuu dodoma,...lakini wengi akaendelea kupuuza.

  ..kujenga ofisi ya gharama kiasi hicho wakati wananchi hawana zahanati, shule, mabweni,maabara,maktaba, .. ni UBINAFSI na KUFURU.
   
 10. minda

  minda JF-Expert Member

  #10
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 2, 2009
  Messages: 1,070
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  ulikuwa umelala na sasa umeamka usingizini?
  hii habari ni posti ya siku nyingi na tulishajadili ikafungwa; sasa kwa nini utuletee tena? au ndo unakazia ulichotumwa towashi mwema?
   
 11. m

  mmakonde JF-Expert Member

  #11
  Aug 9, 2010
  Joined: Dec 26, 2009
  Messages: 967
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Unajiuliza Kamati za Bunge ziko wapi kuruhusu huu upumbavu??????????
  JK atakubali vipi jambo hili?

  Jamani tunba matatizo gani ?Hakuna logic kabisa ,kwa spika kujengewa ofisi jimboni mwake.

  Nani ataiokoa nchi hii?Tsh 500m zingeweza kununua vitanda na mashuka hopitalini hapo wilayani.

  T U M E K W I S H A
   
 12. M

  Mkulima mimi JF-Expert Member

  #12
  Aug 9, 2010
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 233
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  hayo maswali uliouliza ndio watu wanahoji! Aliye andika ili kupata credibility ya source! Kama chanzo hakiaminiki hata habari haiminiki. Maana kabla hatujachangia tutaulizana yakweli haya! Tutajadili tusicho amini?
   
 13. Eliphaz the Temanite

  Eliphaz the Temanite JF-Expert Member

  #13
  Aug 9, 2010
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 2,835
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Ni habari ya RAI jamani! Tupa kwenye dustbin ama wape mamantile wafungie vitumbua
   
 14. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #14
  Aug 9, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,050
  Likes Received: 3,958
  Trophy Points: 280
  jamani ofisi kama hiyo halafu akikosa uspika inakuwaje? spika anayefuatia naye ajenge ofisi kama hiyo pia jimboni kwake?
   
 15. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #15
  Aug 9, 2010
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 12,221
  Likes Received: 7,340
  Trophy Points: 280
  Si hawa RAI ndio wa RA/EL sasa tukikubali hadithi hii kwanini ile inayomhusu Slaa tuikane!!
  Angalia timing ya habari, baada ya kumkosa kura Za maoni [kama selelii] wamekuja na jipya.Wanajua kuwa next speaker anaweza kuwa huyu kwasababu key members wa mtandao wapo hati hati.
  RA na EL hawa watu ni hatari sana!
   
 16. fige

  fige JF-Expert Member

  #16
  Aug 9, 2010
  Joined: Jul 4, 2010
  Messages: 376
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  siku hizi kuna kitu kinaitwa value for money labda na yenyewe inakidhi kama majengo ya viongozi wa bot.juzi watu walisafishwa bila kujali maisha ya walalahoi kwani m 500 na b 6 ipi kubwa ?
   
 17. K

  Kwame Nkrumah JF-Expert Member

  #17
  Aug 9, 2010
  Joined: Dec 2, 2008
  Messages: 887
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Rudia tena kusoma, gazeti limemnukuu Katibu wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Katibu huyo hajakanusha yaliyoandikwa mpaka sasa.
   
 18. k

  kasimba123 JF-Expert Member

  #18
  Aug 9, 2010
  Joined: Apr 18, 2010
  Messages: 1,318
  Likes Received: 188
  Trophy Points: 160
  hii ilishajadiliwa MODS hebu icheki maana ilishafungwa hii
   
 19. Mtazamaji

  Mtazamaji JF-Expert Member

  #19
  Aug 9, 2010
  Joined: Feb 29, 2008
  Messages: 5,972
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Habari naiamini. 80%

  ukweli ni kuwa wabunge watanzania wanataka waonekane kama miungu watu.

  Sibishi sana sababu sitalivyokuwa anakazania kusema bunge la viwango. Hakuwa na maana ya viwango vitakavyokuwa na manufaa kwa wanachi sana.viwango anavyopigia debe zaidi ni viwango vya maslahi ya wabunge na viwango vya heshima ya kutukuka wanayotakiwa kupewa.Tumeona Samwel Sitta alivyofanikisha kupandisha marupu rupu ya wabunge na bado ansema ni madogo ukilinganisha na ya wabunge wa jumiya ya madola. Sijui kama angelinganisha na pato la taifa au GGD kama angeona ni madogo.

  Hivi kazi ya mbunge na kazi ya RPC, Ofisa elimu wa mkoa au wilaya, Mganga mkuu wa mkoa au wilaya ipi ni muhimu.?
  Hivi ofisi ya mbunge na Ofisi ya RPC, Ofisi ya ofisa kilimo wa mkoa au wilaya, ni ipi inatakiwa kuwa na viwango vya juu?
  Hivi katika siku 365 za mwaka mbunge atakayetumia ofisi yake muda mrefu ataitumia kwa siku ngapi?

  Kwa nini wabunge wasitumie mashangingi yao kama mobile office? Tunahitaji wabunge creative wanaoweza kutimia minimal resources efficiently

  Basi kama wanamua kuponda maliza serikali ovyo ovyo wafanye japo katika njia ya kiraffiki kidogo
  Mko wa Tabora una misitu ya mbao ngumu .wabunge wanatakiwa watumie locoal supplier na ikiwezekana hata kama ni viwanda vidogo vidogo. Wabunge wanaimba kila siku tununue bidhaaa za nyumbani yet wao suti zao zote ni za italy.
  Wanasaidiaje kukuza. Ajira za majimboni kwao kama si mikoa yao.

  Je kuna local carpenter maarufu Urambo au Tabora aliyeshindwa kutengeza stuli au viti vya kukalia wageni.? Yaani hata stuli?

  Je wageni wa spika katika ofisi ndogo wakilalia samani zilozotengenezwa na wanauambo au tabora watachubuka makalio?


  CAG ATAKUJA KUKEMEA UOZO HUU UKISHAFANYIKA LABDA KIPINDI HICHO SITTA NI ...............
  Napendekeza CAG aliangalie hili sijui kama sheria zinamruhusu. katika mamboa nayotakiwa kuagalia tunataka tuone attendence na guest register za ofisi hizi za wabunge.
   
 20. Fisherscom

  Fisherscom JF-Expert Member

  #20
  Aug 9, 2010
  Joined: Mar 13, 2008
  Messages: 1,423
  Likes Received: 239
  Trophy Points: 160
  Source: Rai
  Mmmh!
  Mmiliki: RA
  Kumbeee!!
   
Loading...