Samuel Sitta Anatisha-According to Rai!!!

Kama si Mdondoaji na JF nisingesoma upuuzi huu wa kifisadi leo!!! Acha Mi nalie na aliyeleta thread hii machoni kwangu vinginevyo niliisha sahau kijalida kile cha mafisadi!

Slaa for Presidency.
 
Hii ni real collection of events.

Je Mheshimiwa Sitta ana imani atakuwa mbunge wa Urambo wa kudumu na spika wa Bunge wa kudumu?, maana hio ni ofisi ndogo ya spika na pia mbunge wa Urambo.

Amkeni Urambo electorate!
 
Kweli mfa maji haachi kutapatapa. Naona kuna mtu yuko hoi maji yanamzidi nguvu. Time will tell!!!
 
Source: Rai
Mmmh!
Mmiliki: RA
Kumbeee!!

Mwingine huyu, "source" siyo RAI, RAI ni "outlet". Rai wamemnukuu hata President ambaye naye pia hajakanusha kunukuliwa. Haya ni matumizi mabaya ya mali za umma bila kujali nani ametoa habari. Ulitakuwa kuhoji kwa nini pesa za kujengea barabara, hospitali na mashule zimehamishwa kutoka fungu lililokuwa limepangiwa na bunge kwenda kujenga ofisi ambayo tayari alikuwa nayo anyway?
 
Kweli mfa maji haachi kutapatapa. Naona kuna mtu yuko hoi maji yanamzidi nguvu. Time will tell!!!

Inawezekana but usisahau Sitta naye ni fisadi kwani amefanya ufisadi wa kutisha katika serikali ya awamu ya pili na ya kwanza. Hakuna mtu asiyefahamu mahekalu yake na pesa alizokuwa nazo. La msingi ni umakini wa taarifa.
 
Jamani Sita hajasema ni yake kama Sita bali ni mali ya serikali, kama akianguka basi ataitumia anayekuja au inaweza kutumiwa kwa shughuli zingine na serikali. Inaweza hata ikawa part ya ikulu ndogo na kutumiwa na raisi akija kikazi wilayani.
 
Kama umeamua kumtetea basi mtetee kwa maswali yote yaliyoulizwa. Usijibu swali moja tu, kwa mfano mbona haujaeleza kwa nini amenunua fenicha za milioni 100, wakati fenicha hizohizo zingepatikana kwa milioni 40? Umeambiwa Ikulu ndogo haipo Urambo?
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom